Tafuta

2021.01.13 KATEKESI YA PAPA 2021.01.13 KATEKESI YA PAPA 

Papa Francisko:Wachanga watakuwapo siku zijazo duniani na matumaini ya Kanisa!

Akiwa katika maktaba ya Jumba la Kitume,Papa Francisko katika katekesi yake amejikita katika kiini cha Sala ya kusifu.Huu ni mwendelezo wa tafakari kuhusu sala ambapo amesisitiza umuhimu wa kusifu Mungu kila wakati hata wakati wa giza la maisha yetu,kwani Bwana ni rafiki mwaminifu ambaye hatuachi kamwe.Ni wachanga wanaompokea Yesu na Neno lake na Yesu anasifu Baba yake kwa ajili ya upendeleo wao.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika Katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 13 Januari 2021 akiwa katika Maktaba ya Kitume Vatican, ametoa nafasi ya ukuu kutoa sifa katik kuanzia na hatua ya maoni kuhusu maisha ya Yesu. Mara baada ya miujiza ambayo ili wahuhusu kwanza wafuasi wake, katika kutangaza Ufalme wa Mungu, Utume wa Masiha, yaani utume wa Yesu ulipitia katika wakati mgumu. Yohane Mbatizaji, alipatwa na shaka na kutuma ujumbe wake wakati yeye yuko gerezani amefungwa na kuuliza: “Je ni wewe ambaye ulitakiwa kuja au tunapaswa kusubiri mwinginne? (Mt 11.3).  Hii ni kwa sababu alihisi ndani mwake huzuni bila kujua uhakika kama amekosea kutangaza. Katika maisha daima kuna wakati wa giza, wakati wa usiku wa kiroho na Yohane alipitia kipindi hiki, anasema Papa Francisko. Kulikuwa na vizingiti katika vijiji, karibu ziwa mahali ambamo Yesu alikuwa ametenda ishara za miujiza mingi (Mt 11,20-24). Na sasa ni wakati wa kukatisha tamaa, mwinjili Matayo anaeleza tendo la kweli la kushangaza. Yesu lakini hakuinua kwa Baba yake malalamiko, badala yake aliinua wimbo wa furaha kuwa “Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga” (Mt 11, 25).

Katikati y mgogoro Yesu anatoa sifa na kushukuru

Katikati ya mgogoro na katikati ya usiku wa giza la watu, kama vile Yohane, Yesu anatoa sifa na kushukuru Mungu.  Je ni kwa nini? Kwa kufafanua Papa Francisko amesema awali ya yote anasifu kwa kile ambacho yeye ni: “Baba, Bwana wa mbingu na nchi”. Yesu anafurahi katika roho yake kwa sababu anajua na anahisi kuwa Baba yake ni Mungu wa ulimwengu, na vile vile Bwana wa kila kitu kilichopo ni cha Baba, ni Baba yangu”. Kwa uzoefu huu wa kusikia Mwanae wa aliye juu ndipo inatokea sifa. Yesu anahisi kuwa mwana wa aliyejuu. Baadaye Yesu anasifu Baba kwa sababu anaongoza wachanga. Hii  kwake  Yeye binafsi anafanya uzoefu, wakati wa kuhuburi katika vijiji. Wenye akili na hekima wanabaki hivi hivi na wamefungwa, kwa maana kuhesabu, wakati wachanga, wanajifungulia na kukaribubisha ujumbe yaani Neno lake. Hili haliwezi kuwa utashi wa Baba, na Yesu anahisi furaha. Hata sisi tunapaswa kufurahai na kusifu Mungu kwa sababu ni  watu wanyenyekevu na walio rahisi wanaongozwa na  Injili. Papa Francisko ametoa mfano kwamba anawaona watu rahisi kama hawa, wanaokwenda kwenye hija, wanakwenda kusali, wanaimba, wanasifu, ni watu ambao labda wanakosa mambo mengi, lakini wanao unyenyekevu na ambao unawapelekea kusifu Mungu…

Wachanga watakuwapo siku zijazo za ulimwengu na katika matumaini ya Kanisa 

Katika wakati ujao wa ulimwengu na matumaini ya Kanisa, daima kutakuwapo wadogo, ikiwa na maana ya  wale ambao hawajioni kuwa bora zaidi ya wengine, wanao utambuzi wa vizingiti vyao, na dhambi zao, na ambao hawataki kuwa juu ya wengine na mbao katika Mungu Baba, wanajitambua kuwa wote ni ndugu, Papa Francisko amefafanua. Kwa maana nyingine katika wakati huo ambao ulionekana wa kushidwa, mahali ambapo kila kitu ni giza, Yesu anasali  na kusifu Baba. Na sala yake inatupeleka hata sisi wasomaji wa Injili kuhukumu kwa nama tofauti ya kushindwa kwetu biafsi, kuhukumu kwa namna tofauti ya hali ambazo hatuoni wazi wa uwepo na matendo ya Mungu na ambapo utafikiri kwamba ubaya ndiyo inashamiri na hakuna namna ya kuusimamisha. Katika wakati huo, Yesu alishauri sala ya kuomba. Ni katika wakati huo ambao angekuwa na sababu ya kuomba aelezwe maana yake na Baba, lakini kinyume chake alianza kusifu. Utafikiri ni kitu kinachopingana nacho lakini ndiyo ukweli uliopo. Papa amesisitiza.

Sifa inasadia sisi au Mungu?

Sifa inasaidia nani?  Kwetu sisi au Mungu? Katika andiko la liturujia ya Ekaristi inatualika kusali kwa Mungu kwa namna hii. “Wewe huna haja ya sifa zetu, lakini kwa ajili ya zawadi ya upendo wako, unatuita kukushukuru; nyimbo zetu za shukrani hazikuongezei ukuu wako, lakini zinatupatia neema ambayo inatuokoa” ( Misale ya Roma, sala ya pamoja IV). Kwa kusifu tunakuombolewa. Sala ya sifa inasaidia sisi. Katika Katekisimu, inaenelezea kuwa “sala ya sifa ni ushiriki wa hisia za moyo safi ambazo zinampenda Mungu katika imani kwa namna ya kumwona katika utukufu” (n.2639). Sambamba nayo lazima ifanyiwe uzoefu si tu wakati wa maisha yaliyojaa furaha, lakini zaidi, wakati mgumu, wakati wa giza, mahali ambapo safari inakuwa ni mpando mkali. Hata hapo ni kipindi cha kutoa sifa. Kama Yesu ambaye wakati wa giza alitoa sifa kwa Baba. Ni kwa sababu tunajifunza kwamba kwa kupitia mpando, kupitia nyayo ya shida, yenye ugumu, na hatua kali sana inafikia kuona uwanda mpya, upeo uliofunguliwa zaidi. Kusifu ni kama kuvuta oksijeni safi. Inasafisha roho, inakufanya utazame mbali bila kubaki umefungiwa katika wakati mgumu, wa giza la matatizo.

Mtakatifu Francis licha ya kuwa kipofu na mateso alitunga wimbo wa Laudato si'

Papa Francisko akiendelea amesema kuna mafundisho makuu katika sala ambayo kwa karne nani haikukosa kamwe kuwa na mapigo yake na ambayo Mtakatifu Francis alitunga wakati wa kuhitimisha maisha yake. “wimbo ndugu jua” au wa viumbe vyote. Maskini huyo hakuutunga wimbo huo wakati wa furaha, wa ustawi wa maisha yake, lakini kinyume chake alikuwa katikati ya taabu nyingi. Mtakatifu Francis ambaye tayari alikuwa ni kipofu, alihisi ndani mwake, uzito wa upweke ambao alikuwa hajawahi kujaribiwa: ulimwengu haujabadilika  tangu mwanzo wa kuhubiri kwake . Kuna ambaye bado anaendelea kutawaliwa na ugonvi, na zaidi alihisi hatua ya kifo ambacho kilikuwa karibu naye zaidi. Ingekuwa ni kipindi kwake cha kukata tamaa, na kuelezea kushindwa kwake biafsi.

Bwana ni mlinzi anayekufanya usonge mbele na kujiamini

Kinyume chake lakini Mtakatifu Francis kwa kitambo cha huzuni , kitambo cha giza alisali. Je alisali namna gani? “Laudato si mi Signore”, yaani “usifiwe ewe Bwana” au sifa iwe kwako… Alisali akisifu. Francis alisifu Mungu kwa yote, kwa ajili ya zawadi zote za uumbaji na hata kwa ajili ya kifo, ni ujasiri gani alikuwa nao hadi kuita kifo “dada”, Papa amesema. Wakati wa kipindi kigumu, Mungu anatufungulia milango ya njia iliyo kubwa kuelekea kwa Bwana na anatutakasa daima. Sifa inatakasa daima. Watakatifu wote wanatueleza kuwa inawezekana kusifu daima, katika mema na mabaya, kwa sababu Mungu ni rafiki mwaminifu. Huo ndiyo msingi wa sifa. Mungu ni rafiki mwaminifu na upendo wake haukosekani kamwe. Yeye daima yuko karibu nasi, Yeye anatusubiri daima. Kuna aliyesema kuwa “Ni mlinzi ambaye yuko karibu na wewe na anayekufanya usonge mbele kwa kujiamini”. Katika wakati mgumu na wa giza, tuna ujasiri wa kusema: Ubarikiwe ee Bwana. Usifiwe ee Bwana. Hii itatusaidia sana, Papa ameshauri na kuhitimisha katekesi yake.

KATEKESI PAPA 13 JANUARI
13 January 2021, 14:10