Tafuta

2021.10.01  Sala ya Malaika wa Bwana 2021.10.01 Sala ya Malaika wa Bwana 

Papa Francisko:Mungu ni huruma &tulikombolewa bure!

Kwa kuzama Yesu ndani ya maji yam to Yordani ni kuonesha jinsi Mungu anavyoshinda ubaya wa ulimwengu kwa kujishusha na kubeba dhambi zetu.Na ni njia ambayo sisi tunaweza kufanya kwa ajili ya kuwainua wengine,bila kuwahukumu,bilakuwaogopesha,bali kwa kuwakaribia,kutesekanao na kushirikishana nao upendo wa Mungu.Ubatizo ni utambulisho wa kikristo unaotukomboa bure.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatian

Dominika tarehe 10 Januari 2021 katika siku kuu ya ubatizo wa Bwana, Papa Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, ametoa tafakari yake akiwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume Vatican. Akianza tafakari hiyo, amesema “leo tunaadhimisha siku kuu ya ubatizo wa Bwana. Siku chache zilizopita tumeacha Mtoto Yesu aliyetembelewa na Mamajusi na leo tunamkuta ni mtu mzima akiwa katika mto wa Yordani. Liturujia inaturusha juu hadi kufikia miaka 30, miaka therathini ambayo tunajua jambo moja kwamba ilikuwa ni maisha yaliyofichika ambayo Yesu alipitia akiwa ndani ya familia; baadhi ya miaka ya kwanza akiwa Misri, kama muhamiaji akikimbia mateso ya Herode; mingine akiwa Nazareth, akijifunza kazi ya Yosefu na katika familia kwa kutii wazazi, kusoma na kufanya kazi. Papa Francisko ameongeza kusema, inashangaza kuona sehemu kubwa ya wakati wake katika ardhi hii, Bwana alipitia namna hii, kwa kuishi maisha yake ya kila siku bila kuonekana. Kwa kufafanua zaidi amesema tufikirie Injili zinasema miaka mitatu tu akihubiri, ya kutenda miujiza na mambo mengi. Miaka mingine ni maisha yaliyofichwa ndani ya familia. Ni ujumbe mzuri kwa ajili yetu, unaonesha ukuu wa kila siku, umuhimu wa mtazamo wa macho mbele ya Mungu kwa kila ishara na wakati wa maisha hata kile kilicho rahisi na kilichofichika.

Maisha ya kuhubiri kwa Umma

Baada ya miaka therathi ya maisha yaliyofichika Yesu alianza maisha yake kwa umma.  Alianzia hasa na ubatizo katika mto Yordani. Lakini Yesu ni Mungu. Je ni kwa nini Yesu anabatizwa? Ubatizo wa Yohahe ulikuwa ni ibada ya toba, ulikuwa ni ishara ya mapenzi ya kuongoka, ili kuwa bora kwa kuomba msamaha wa dhambi binafsi. Yesu kwa hakika hakuwa na haja.  Kiukweli Yohane Mtabatizaji alitafuta kupinga, lakini Yesu akasisitiza. Je ni kwa nini? Ni kwa sababu anataka kukaa na wadhambi, na kwa maana hiyo anajiweka kwenye mstari na wao na kutimiza ishara hiyo.  Anafanya hivyo kama watu wake, kama usemavyo wimbo “alikaribia akiwa miguu peku na roho tupu”. Roho iliyo wazi ya  kutofunika lolote, hivyo kama mdhambi. Ndiyo ishara ambayo anafanya Yesu. Alitelemka katika mto ili kuzama katika hali yetu sisi. Ubatizo kwa hakika una maana hiyo ya kuzama.

Mungu anajishusha na kubeba dhambu zetu

Katika siku ya kwanza ya huduma, Yesu anajionesha hivi mpango wake. Yeye anatueleza kuwa hawezi kutuokoa akiwa juu, kwa uwepo wa ukuu au tendo la nguvu, au amri. Kwani Yeye anatuokoa kwa kuja kukutana na kuchukua dhambi zetu binafsi. Na ndiyo tazama jinsi Mungu navyoshinda ubaya wa ulimwengu kwa kujishusha na kubeba ndani dhambi zetu. Na ni njia ambayo sisi tunaweza kufanya kwa ajili ya kuwainua wengine, bila kuwahukumu, bila kuwaogopesha nini cha kufanya, bali kwa kuwafanya kuwa karibu, kwa kuteseka, kushirikishana upendo wa Mungu nao. Yeye Mwenyewe alisema kwa Musa: “Ni watu gani wana miungu iliyo karibu zaidi yangu nilivyo karibu nanyi. Ukaribu ni mtindo wa Mungu kwa ajili yetu.

Huruma ndiyo uso wa Mungu kwetu sisi

Baada ya ishara hii ya huruma ya Yesu, ilitokea jambo maalum kwani mbingu zilifunguka na kuonesha haruma ya  Utatu. Roho Mtakatifu alishuka kama njiwa (Mk 1,10) na Baba akamwambia Yesu: “Wewe ni mwanangu mpendwa (Mk 1,11). Mungu anajionesha inapotokea huruma; Papa amehimiza na kusema kwani Mungu anajionesha msamaha wake kwa namna hiyo katika huruma na kwa sababu ndiyo uso wake.  “Yesu alijifanya mtumishi wa wadhambi na akatangazwa kuwa ni Mwana; alijishusha chini yetu na Roho akashuka juu yake.  Upendo unaita upendo. Hii ina maana hata kwa ajili yetu, kwa kila ishara ya huduma, kwa kila shughuli yoyote ya huruma ambayo inatimizwa, Mungu anapendekeza na kuwa na mtazamo juu ya ulimwengu, na ndivyo hata sisi tunapaswa” amesisitiza Papa Francisko.

Tulikombolewa bure na Mungu anasubiri milango ifunguliwe aingie

Lakini, hata kabla ya kufanya chochote, maisha yetu yanaoneshwa na huruma ambayo imekaa kwetu. Tulikombolewa, lakini bure. Wokovu ni wa bure. Ni ishara ya bure, ya huruma ya Mungu kwetu. Sakramenti hii hufanyika siku ya Ubatizo wetu, lakini hata wale ambao hawajabatizwa hupokea huruma ya Mungu kila wakati, kwa sababu Mungu yuko pale, anasubiri. Anasubiri milango ya mioyo ifunguke. Yeye hukaribia”. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema “Mama ambaye tunamwomba atusaidie kulinda utambulisho wetu, yaani utambulisho wa kuwa na huruma na ubatizo ambao ndiyo msingi wa imani na ya maisha”.

10 January 2021, 15:34