Tafuta

2021.01.14 Kardinali Eusébio Oscar Scheid, Brazil 2021.01.14 Kardinali Eusébio Oscar Scheid, Brazil 

Papa Francisko:Kardinali Scheid,alikuwa mtu mwema na mtumishi adilifu!

Wema wa Mungu kwa ajili ya Kanisa ndiyo ilikuwa njia ya maisha yake na katika shughuli za kichungaji ambazo zilionekana kwa Kardinali,Askofu Mkuu mstaafu wa Rio de Janeiro,nchini Brazil aliyeaga dunia tarehe 13 Januari 2021.Papa Francisko amekumbusha hayo katika Telegram ya salam za rambi rambi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Ukaribu wa sala na salam za rambi rambi kwa moyo wote mbao Papa Francisko ameuelezea kufuatia na kifo kilichotokea tarehe 13 Januari 2021 cha Kardinali Eusebio Oscar Scheid, nchini Brazil katika telegram aliyoelekeza kwa Askofu Mkuu wa Mtakatifu Sebastian, Rio de Janeiro, Kardinali Orani João Tempesta. Mchungaji adilifu na mkarimu na ambaye kama nembo ya kiaskofu ilivyokuwa “Mungu ni mwema” na ambayo ndani mwake ilifungasha kwa dhati wema wa Mungu kuelekeza Kanisa ambalo Kardinali Eusebio alijikita nalo; Mtumishi wa Mungu na kwa ajili ya utunzaji mkuu wa Kanisa lake amesema Papa Francisko.

Katika telegram hiyo aidha Papa ameelezea kwa kifupi kuhusu shughuli kichungaji  ya Marehemu nchini Brazil ambayo miongoni mwake  ni kwamba alitenda ndani ya majimbo ya Florianopolis na makao makuu ya jimbo la Mtakatifu Sebastian wa Rio de Janeiro. Kwa maana hiyo, Papa anatoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya zawadi msingi kama ile ya maisha na huduma yake na anatoa maombi ili aweze kupokelewa kwa furaha ya milele. Wazo la Papa katika salam hizo, hatimaye anawaelekeza wanafamilia na wote ambao wanaomboleza kuondokewa na Kardinali huyo.

Ikumbukwe Askofu Mkuu mstaafu wa Rio de Janeiro  amepambana kwa muda mrefu dhidi ya gonjwa baya la homa ya mapafu kutokana na virusi vya corona katika Hospitali ya Mtakatifu Francis wa Jacareí, nchini Brazil, alipokuwa amelazwa. Na kwa upanda wa majimbo yote wanatoa shukuru kwa kina kwa ajili ya miaka 60 ya huduma ya kichungaji na miaka 40 ya uaskofu na ambapo yeye marehemu alikuwa pia ni mtaalam wa masuala ya kichungaji ya kifamilia.

15 January 2021, 16:17