Tafuta

Vatican News
2021.01.2: 9Mahakama Kuu ya Rufaa ya Kipapa “Rota Romana”, imezindua rasmi Mwaka wa Mahakama 2021. 2021.01.2: 9Mahakama Kuu ya Rufaa ya Kipapa “Rota Romana”, imezindua rasmi Mwaka wa Mahakama 2021.  (Vatican Media)

Papa Francisko azindua Mwaka wa Mahakama ya Rota Romana!

Katika hotuba ya Papa kwa majaji wa Mahakama ya Rota Romana amependa kurejea katika hotuba ya mwaka uliopita kwa namna ya pekee mada ambayo inagusa sehemu ya maamuzi katika ubatilishwaji wa ndoa.Kwa upande moja kuna ukosefu wa imani yakuangaza inatakiwa katika muungano wa wanandoa.Maaskofu ni majaji hawawezi kunawa mikono katika michakato hiyo majimboni.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Ijumaa, tarehe 29 Januari, Mahakama Kuu ya Rufaa ya Kipapa “Rota Romana”, imezindua rasmi Mwaka wa Mahakama 2021, ambapo wamekutana na Papa Francisko. Katika hotuba yake amesema Familia njema, wema wa familia, lazima uwe ndiyo kovu cha cha kujikta nacho katika mchakato wa kuubatilisha ndoa, hasa wakati ubatilishwaji huo unaombwa na mwenzi na haukukubaliwa na mwingine na kuna watoto katikati yake. Papa Francisko amesisitiza hili katika kwa uzinduzi huo ambao umekuwa wa kiutamaduni huku akiwaomba majaji, kuanzia na maaskofu, ambao waliitwa na Papa kuwa majaji katika mchakato wa kesi fupi za ubatilishwaji,  naili wafanye kazi wote wakiwa na ufahamu wa kichungaji. Katika hotuba yake Papa ametaja kuachwa kwa utaratibu wa mchakato wa hukumu inayofuata mara mbili katika kesi za ubatili wa ndoa, na kwa hivyo kesi fupi, ambayo ilikuwa kama jambo jipya, na badala yake ni ya asili kwa sababu askofu  anakuwa  jaji.

Mageuzi yalipingwa vikali ni kwa sababu ya pesa

Katika kuendelea na hotuba Papa amesimulia kwamba anakumbuka kuwa muda mfupi baada ya kuchapishwa mchakato wa kesi fupi, askofu mmoja alimwita na kumwambia alikuwa na shida, kwamba msichana  mmoja alitaka kuolewa kanisani lakini na alikuwa ameolewa kwa kulazimishwa. Mashuhuda walisema alilazimishwa, na kwamba ndoa ilikuwa batili. Na yeye akamuuliza kama anayo kalamu mkononi mwake?  Na akamwambia “Ti saini”. Wewe ndiye hakimu bila historia”. Papa anaongeza kusema kuwa mageuzi haya na kuhusu mchakato wote mfupi yana upinzani mwingi, na kwamba baada ya kutangazwa amepokea barua, na wengi, karibu wote  walikuwa mawakili ambao labda walikuwa wanapoteza wateja wao. Kuna shida ya pesa, amesisitiza Papa. Huko Uhispania wanasema: “pesa hucheza kama tumbili”. Na pia aliona katika majimbo mengine, kwa huzuni, upinzani wa baadhi ya makasisi wa mahakama  na kwamba kuna ambaye katika mageuzi haya alipoteza nguvu fulani, kwa sababu alitambua kuwa jaji hakuwa yeye, bali askofu. Papa  Francisko amesisitiza kwamba Monsinyo Pinto ameweza kupata kura kwa umoja, ambayo ilimpatia fursa ya kutia saini.

Askofu lazima asaidiwe lakini yeye ndiye hakimu hawezi kunawa mikono

Papa Francisko  akiendelea na hotuba hiyo amezungumzia hukumu mara mbili  kuwa  Papa Lambertini yaani (Benedikto XIV), alitoa hukumu hiyo mara mbili kwa sababu ya shida za kiuchumi katika baadhi ya majimbo, na pia akasisitiza hapa kwamba “jaji ni askofu: lazima asaidiwe na makamu wa kimahakama, na mtetezi wa haki, lakini yeye ndiye hakimu hawezi kunawa mikono, na kurudia kwa  hilo ndio ukweli wa kiinjili”.

Ushauri wa kusoma Wosia wa Amoris Laetitia katika mwaka wake

Papa Francisko katika  hotuba ndefu, iliyotolewa akiwa ameketi kwa sababu ya maumivu ya mguu ambao umemsababishia hata kuacha  shughuli kadhaa, Papa amerejea, juu ya jitihada ya  kufanya mang’amuzi. Katika Mwaka wa Familia ya Wa Amoris Laetitia, Papa anaomba kujikita kusoma Wosia huo uliotolewa mwishoni mwa  sinodi mbili juu ya familia kama chombo cha kichungaji, na kinahusu kipengele cha 241. Kipengele hicho kinaelezwa juu ya yote kutenganisha ambapo wakati mwingine kunaweza kuwa muhimu kimaadili, lakini kiukweli ni suluhisho kali. Kwa kifupi, ni kulinda familia kwanza kabisa. Na, hata kabla ya hapo, kulinda matunda ya familia, ambayo ni watoto.

Familia ni matokeo ya ndoa iliyofananishwa na Muumba

Mwaka jana, Papa alizingatia hitaji la kuinjilisha wenzi wa ndoa, wakati mnamo 2019 alisisitiza umuhimu wa kujiandaa kwa ndoa. Katika hotuba ambayo ni mwendelezo wa asili wa ile ya miaka iliyopita, Papa amezingatia zile ndoa ambazo zinashindwa, na jinsi hii inavyoathiri familia njema. Kwa sababu, Papa ameelezea, kuwa kulikuwa na hata mazungumzo ya ukweli kwamba uzuri wa familia unaweza kuwakilisha kichwa cha ubatili, lakini basi uwezekano huu ulifungwa ipasavyo, na hivyo kuimarisha sura ya kitaalimungu  ya familia, kama matokeo ya ndoa  iliyofananishwa na Muumba.  Papa Francisko vile vile  anakubali, “kwa sababu uzuri wa familia hauwezi kuzingatiwa kama mmoja  ya viongozi wa ubatili , lakini ni kila wakati na kwa hali yoyote lile tunda lililobarikiwa la makubaliano ya ndoa; haiwezi kuzima kwa ukamilifu na tamko la ubatili, kwa sababu kwamba familia haiwezi kuzingatiwa kama mali iliyosimamishwa, kwani ni tunda la mpango wa kimungu, angalau kwa watoto waliozalishwa”.

Utume wa majaji ni huduma iliyojaa maana ya kichungaji

Papa Francisko kwa majaji wa Rota, anawaomba wasishindwe kutoa ushahidi juu ya wasiwasi huu wa kitume wa Kanisa, wakizingatia kuwa wema wa watu hauhitaji kubaki bila kufanya kazi mbele ya athari mbaya zinazoweza kutokea za uamuzi juu ya ndoa za ubatili. Aidha amesisitiza hitaji la kufanya sababu za ubatili kuwa huru kadiri inavyowezekana, na kuwakumbusha majaji juu ya hitaji la kufungua upeo wa utunzaji huu mgumu lakini usiowezekana wa wachungaji, ambao unahusu wasiwasi wa watoto, kama waathiriwa wasio na hatia  katika  hali nyingi ya mipasuko, talaka au miungano mipya ya kiraia, huku akisisitiza kwamba utume wa majaji ni huduma iliyojaa maana ya kichungaji, na kiukweli sio kitendo baridi cha uamuzi tu wa kisheria.

Umakini upewe familia

Papa Francisko ameomba umakini upewe kwa familia, na amewasihi maaskofu kufungua mada, kwa sababu ni suala  la kuendelea na ukakamavu na kukamilisha safari muhimu ya kikanisa na ya kichungaji, inayolenga kutowaacha waamini wanaoteseka kuingilia kati viongozi wa serikali, kwa hukumu ambazo hazikukubaliwa na zilizowasibu. Inahitaji kuwa na  mawazo ya ubunifu wa upendo, na kwa sababu hiyo Papa anaamini kuwa ipo dharura ya  haraka sana kwamba wahudumu wa Maaskofu, hasa makasisi wa mahakama, waendeshaji wa huduma ya kichungaji wa familia na zaidi mapadre wote wa maparokia, wafanye juhudi kufanya mazoezikwamba huduma ya ulinzi, kusindikiza mwenzi  aliyeachwa na labda ana watoto, ambao wanateseka kutokana na  maamuzi, hata ikiwa ni sawa na halali, ya ubatili wa ndoa .

Shukrani kwa mkuu wa Rota Romana

Mwisho wa hotuba, amemsalimia Monsinyo Pio Vito Pinto, mkuu wa Rota, ambaye atafikisha miaka 80 na kustaafu: “Mkuu wetu mpendwa amesema Papa Francisko - atakuwa kijana wa miaka 80 katika miezi michache, na atalazimika kutuacha, ningependa kumshukuru kwa kazi ambayo amefanya na ambayo kila wakati haieleweki zaidi ya yote ningependa kumshukuru Monsinyo Pinto kwa uthabiti aliokuwa nao wa kufanya marekebisho ya michakato ya ndoa. Pia namshukuru Monsinyo Pinto kwa shauku yake katika kufundisha katekesi juu ya mada hii. Yeye huzunguka ulimwenguni akifundisha hivyo: yeye ni mtu mwenye shauku, lakini mwenye shauku kwa sauti zote, kwa sababu hata yeye pia ana tabia yake hiyo! Ni namna hasi, kwa kusema hivyo juu ya  shauku. Lakini atakuwa na wakati wa kujirekebisha…, sisi sote tunazo! Ningependa kumshukuru! Ninatafsiri makofi kama makofi ya hasira (kicheko)….Asante sana, Monsinyo  Pinto! Asante! (Makofi)… amehitimisha Papa Francisko hotuba yake ndefu.

29 January 2021, 16:38