Tafuta

Papa Francisko Papa Francisko 

Papa Francisko: Mwaka 2021 uwe wa kidugu,mshikamano na amani kwa wote!

Siku ya kwanza ya Mwaka,imewekwa kwa ajili ya siku kuu ya Maria Mama wa Mungu na ndiye yeye tunamkabidhi sala na matumaini ya amani kwa ajili ya ulimwengu katika mwaka unaofunguliwa.Sambamba na Siku ya 54 ya Amani duniani Papa Francisko wakati wa sala ya malaika amebainisha kuwa wema mkuu ni zawadi ya Mungu inayotakiwa kujenga kwa umakini kwa kuwatazama wengine na kwa njia ya mazungumzo na ushirikiano kati ya watu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Sherehe ya Bikira Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu ambayo uadhimishwa kila tarehe Mosi ya kila mwaka, pia ni mwendelezo siku kuu ya  la Noeli  Mungu pamoja nasi na ambaye alijifanya mwili ili kushiriki ubinadamu wetu. Katika tafakari ya Papa Francisko kabla ya sala y Malaika wa Bwana anabainisha kuwa unaanza mwaka mpya ukiwa chini ya mtazamo wa kimama na upendo wa  Maria Mtakatifu, ambaye katika liturujia ya siku inaadhimishwa kama Mama wa Mungu. Ni kujikita katika nyayo ndefu za wakati, huku tukimkabidhi uchungu wetu na mahangaiko,  Yeye ambaye anaweza yote. Maria anatutazama kwa huruma ya kikanisa kama anavyomtazama Mwanae Yesu.  Na ikiwa tunazama Pango, tunaona kuwa Yesu hakuwa katika  kitanda cha mtoto, Papa amesema kwani walimwambia kuwa Mama alisema: “je mnaweza kinifanya nimweke kwenye mikono yangu mwanangu? Na ndivyo Mama anafanya hivyo kwetu sisi anataka kutuweka kwenye mikono yake ili kutulinda kama mtoto wake mpendwa.

Mtazamo wake wa uhakika na faraja wa Bikira Mtakatifu ni kutia moyo ili kwamba kipindi hiki tulichopewa na Bwana, kiwe ni kwa ajili ya kukua kibinadamu na kiroho, kiwe kipindi cha kuondolea mbali chuki na migawanyiko, kiwe ni kipindi cha kuhisi kuwa sote ni ndugu zaidi, kiwe ni kipindi cha kujenga na siyo cha kuharibu kwa kutunza mmoja na mwingine na uumbaji. Ni utunzaji wa jirani na kazi ya uumbaji ambayo inaongoza mada ya Siku ya Amani duniani, ambayo inaadhimishwa leo hii Papa amekumbusha. Utamaduni wa utunzaji kama mchakato wa amani”, Papa anakumbusha. Matukio ya uchungu ambayo yaeukabili ubinadamu kwa mwaka ambao umemalizika hasa wa janga, limetufundisha ni kwa jinsi gani kuna ulazima wa kushughulika matatizo ya wengine na kushirikishana mahangaiko yao. Tabia hii, inawakilisha njia ambayo inapeleka katika amani, kwa sababu iwezeshe ujenzi wa jamii ambayo inasimika mzizi juu ya uhusiano wa kidugu. Kila mmoja wetu, wanawake na wanaume wa wakati wanaalikwa kutimiza amani kila siku na kila mazingira ya maisha, kwa kumfungulia mikono ndugu mwenye kuhitaji neno la faraja  ishara ya uhuruma, na ya msaada wa mshikamano.

Katika tafakari ya siku kuu ya Bikira Mama wa Mungu sambamba na siku ya amani duniani, Papa Francisko anabainisha kuwa, inawezekana kujenga amani ikiwa tnaanza kuwa na amani ndani mwetu sisi na wale walio karibu basi, kwa kuondoa vizingiti ambavyo vinatuzuia kutunzana na wale ambao wanahitaji  mahitaji na katika shida. Hii inahusiana na kukuza hisia na utamaduni wa kutunzana, ili hatimaye kuweza kushida tofauti, ubaguzi na ushindani ambao kwa bahati mbaya inashamiri. Amani siyo kutokuwa na vita tu, lakini maisha ni maisha yaliyo na utajiri wa maana na  ambao unaundwa na kuishi katika kujikamilisha binafsi na kushirikishana kidugu na wengine. Kwa kufanya hivyo basi amani inawezekana kupatikana na  ambayo inatafutwa sana na daima iko hatarini kutokana na  vurugu, ubinafsi na na ubaya.

Bikira Maria, ambaye alimweka katika mwanga Mfalme wa amani (Is 9,6), atujalie kutoka mbinguni tunu njema ya amani ambayo kwa nguvu zetu tu hatuweza kufikia utimilifu. Awali ya yote amani ni zawadi ya Mungu, inapaswa kuombwa bila kuchoka katika sala, ikisaidiwa na mazungumzo ya uvumilivu na heshima , kujenga kwa ushirikiano wazi katika ukweli na katika haki, na daima umakini kwa watu wasio na hatia. Papa Francisko katika tafakari hiyo anahitimisa kwa matashi mema kuwa,  amani iweze kutawala katika mioyo ya watu na katika familia; katika maeneo ya kazi na mahali popote; katika jumuiya, na katika mataifa. Na sasa tunapofikiria kuwa maisha leo hii yameaundwa kwa vita na uadui na mambo mengi yanayoharibu… tunataaka amani. Na hiyo ni zawadi. Mwanzoni mwa mwaka  kwa wote Papa anawatumia heri, furana na utulivu  wa 2021.  Uwe ni mwaka wa mshikamano kidugu na amani kwa wote; mwaka uliobeba imani tarajio na matumaini, ambayo tunamkabidhi Mama mlinzi Maria, Mama wa Mungu na Mama yetu.

01 January 2021, 16:02