Tafuta

Vatican News
2020.12.31 mwaka wa jubilei huko compostela 2020.12.31 mwaka wa jubilei huko compostela 

Papa awaalika kujifungulia wengine katika mwaka wa Jubilei ya Compostela!

Umezinduliwa mwaka wa Jubilei 2021 huko Santiago ya Compostela katika Mkoa wa Galizia nchini Uhispania,ambao unajikita kutazama sura ya Mtume Yakobo ambaye masalia yake yanahifadhiwa katika Kanisa Kuu.Ni moja ya madhabahu iliyotembelewa na idadi kubwa ya mahujaji.Katika ujumbe uliotumwa na Papa anawaalika kuwa na uongofu na mshikamano kwa mahujaji katika safari.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Tarehe 31 Desemba 2020, umezinduliwa Mwaka wa Compostela, na kilele  cha Jubilei kitaadhimishwa tarehe 25 Julai katika Siku kuu ya Mtakatifu Yakobo mtume na shahidi siku itakayoangukia Jumapili mwaka 2021.  Mada iliyochaguliwa kuongoza tukio hili ni: “Ondoka katika ardhi yako! Mtume anakusubiri”. Tamko la Askofu Mkuu Julián Barrio Barrio wa Santiago ya Compostela, kwa waamini wote amezungumzia mwaka wa neema na msamaha kwa wote ambao wanashiriki. Katika mwaka huu wa tatu wa Compostela katika Milenia ya tatu ya ukristo, ujasiri wa ushuhuda wa mtume Yakobo ni fursa ya kugundua uhai wa imani na utume uliopokelewa wakati wa ubatizo amesisitiza.

Ujumbe wa Papa Francisko wakati wa funguzi wa Mlango Mtakatifu

Alikuwa ni Askofu Mkuu Julián Barrio Barrio aliyesoma ujumbe wa Papa Francisko aliowatumia katika fursa ya kufungua Mlango Mtakatifu, akieleza upendo na ukaribu wake kwa wote ambao watashiriki katika wakati huu wa neema kwa ajili ya Kanisa na kwa namna ya pekee kwa Kanisa nchini Hispania na Ulaya. Kwa kufuata nyayo za Mtume, Papa anaandika, kuwa “tuache kile kiitwacho usalama binafsi mahali ambamo tunaparamia, lakini kama lengo wazi akilini na tusiwe kama walipotea ambao wanajizungusha binafsi bila kufika mahali popote. Ni sauti ya Bwana ambayo inatuita na kama mahujaji, tupokee, tukaribishe tabia ya kusikiliza na kutafuta kutafsiri safari hiyo ya kukutana na Mungu, wengine na sisi binafsi”.

Huruma ya Mungu inasikindikiza safari yetu

Hatima ya safari yetu ni muhimu tunakoelekea na ambayo ndiyo safari ya uongofu kufuata Yesu aliye  Njia, Ukweli na Maisha anabainisha Papa huku akitaja Barua yake ya kutume “Misericordia et misera” iliyochapishwa mnamo tarehe  20 Novemba 2016,  ambapo ujumbe unatoa uhakikisho kuwa “ katika safari ya huruma ya Mungu inatusindikiza  na hata kama hali ya udhaifu ambao umetokana na dhambi unabaki laki kwa hilo ushindwa  na upendo ambao unaturuhusu kutazama wakati ujao kwa tumaini na kuwa tayari kujiweka  katika maisha yetu katika njia sahihi”.

Njia rahisi na wasindikizaji

Papa Francisko anaandika kuwa “Ili kuruhusu safari lazima awali ya yote kujiondolea na mambo ambayo yanakuletea uzito lakini pia hata maisha ambayo ni kutembea pekee na kujiaminisha wasindikizaji wasio shukiwa na mashaka, ambayo hayasaidii kumjua jirani kama zawadi ya Mungu anayo tupatia kwa ajili ya kusindikizwa katika safari hiyo”. Papa anaongeza kusema kuwa hii ina maana ya kuondokana na ubinafsi ili kuungana na wengine, ya kusuburi na kusaidiana, kushirikishana ugumu na mafanikio. Mwisho wa safari, Papa anaandika, tutajikuta na fuko ulio mtupu lakini ukiwa umejaa uzoefu uliotokana na mikwaruzo na kuwa katika maelewano na maisha ya wengine ya ndugu zetu na dada ambao wanatoka katika mantiki ya maisha na tamaduni tofauti.  Na kugundua uwajibu wetu wa kuwa wamisionari na ili kuwaita wote katika makao ya kuelekea yale ambayo tunatembea.”

Hija inatangaza imani na maisha yake

Katika ujumbe hup Papa anafafanua muhujaji kama mmoja ambaye ana uwezo wa kujikabidhi mikononi mwa Mungu kwa kuwa na utambuzi kuwa ahadi ya makao ipo tayari katika Kristo ambaye yuko karibu sana na kugusa moyo wa ndugu bila ujujuu, bila propaganda, katika mikono iliyo tayari kutoa na kupokea”. Ishara tatu ambazo zinatimizwa na mhuhujaji anapofika katika Mlango Mtakatifu, zinakumbusha sababu ya safari, anaandika Papa. Kwanza ni kutafakari Mlango wa utukufu kwa  mtazamo wa upole wa Yesu; hakimu mwenye huruma na ambaye anakaribisha katika nyumba yake. Ya pili ni mkumbatio ambao unatufikia kutoka katika picha ya Mtume Yakobo ambaye anatuonesha njia ya imani na uhakikisho wa maadhimisho ya Ekaristi. Ishara ya tatu inatualika kihisi kuwa sisi ni watu wa Mungu ambao wanaitwa kushirikishana furaha ya Injili.

Chachu ya mji wa Mtume

Mwaka Mtakatifu unaoadhimishwa ulianzishwa kunako mwaka 1122 na tangu wakati huo, umendelea kufanyika kila baada ya miaka kuanzia 6 na kuendelea. Mlango huo maadhimisho karibu  Jubilei 14 kila karne. Ufunguzi wa Mlango wa Kanisa Kuu la Santiago, mahali ambamo wanahifadhi masalia ya Mtakatifu Yakobo, mkuu wa uinjilishaji nchini Uhispania, unaongeza chachu  zaidi  katika mji wa Galizia. Sura iliyooneshwa kwenye nembo ya tukio hilo ni ishara ya ulimwengu wa safari ya hija ya Compostela, inayorudi kwenye ardhi hii na pwani zake. Msalaba wa mfano wa Santiago na mishale kadhaa inawakilisha udugu kati ya watu wa kila kabila na tamaduni zote. Wanaojikita katika hija ya safari ndefu ni mamilioni ya watu kila mwaka; na ambayo ni safari ya kwanza ya kiutamaduni ya Ulaya na urithi wa ubinadamu na ni moja wapo ya njia za zamani na muhimu zaidi ya Ukristo

 Uzuri mpya katika Kanisa Kuu

Mnamo mwaka wa 2020, safari zilisimamishwa kwa sababu ya janga la covid, lakini iliwezekana kuchukua fursa ya kipindi cha kufungwa kwa kufanyia ukarabati na  kurudisha Kanisa Kuu ambalo sasa linaangaza na taa zinazofaa zaidi na kila kitu kinaangaza na uzuri mpya. Na ni chini ya ishara ya kutafakari uzuri na matumaini, wakati hija zimeanza rasmi lakini dharura inayoendelea ya kiafya inazuia, kiukweli, kuwasili kwa wanahija hao katika Mwaka Mtakatifu inafungua milango yake.

02 January 2021, 10:38