Tafuta

Papa Francisko:wito wa kuhamasisha mapatano ya kitaifa,Marekani!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa Francisko mawazo yake yamekwenda katika Nchi ya Marekani ambayo hivi karibunibunge lake limeamiwa na waandamanaji wa siasa kali.Anawaombea waathiriwa na mshikamano kwa waliopoteza maisha na kujeruhiwa wakati huo akitoa wito kwa mamlaka na watu wote kudumisha maana kuu ya uwajibikaji kwani vurugu ni kujiharibu daima.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika, Dominika tarehe 10 Januari 2021 mawazo ya Papa Francisko yamekwenda kwa watu wa Marekani, kwa kukitikiswa na shambulio na uvamizi wa Bunge la Washington ambalo liligharimu maisha ya watu watano. Kwa ajili ya waathiriwa hawa, Papa Francisko anawahakikishia sala yake: “Ninatoa salamu ya upendo kwa watu wa Marekani iliyotikiswa na kuzingirwa kwa Bunge hivi karibuni. Ninawaombea wale ambao wamepoteza maisha yao: watano, ambao wamepoteza katika nyakati hizo za shambulio. Narudia kusema kuwa vurugu daima ni kujiharibu. Hakuna kinachopatikana kwa kutumia vurugu na mengi hupotea”.

Jitihada za upatanisho

Baba Mtakatifu kufuatana na hilo amewageukia moja kwa moja viongozi wa Marekani akiwakumbusha juu ya majukumu yao na kujitoa kwa ajili ya upatanisho wa jamii ya Marekani: “Ninawahimiza mamlaka ya serikali na watu wote kudumisha hali ya juu ya uwajibikaji, ili kuwahakikishia watu, kuhamasisha upatanisho wa kitaifa na kulinda maadili ya kidemokrasia yanayojikita kwa kina katika jamii ya Marekani”.

Kutafuta wema wa pamoja

Papa Francisko hata hivyo kabla ya kumaliza wazo hilo la Marekani ameomba msaada wa Bikira Maria mkingiwa dhambi ili kutekeleza mchakato wa utulivu unaolenga na kutafuta wema wa wote: “Bikira Bikira asiye na doa Mlinzi wa Marekani, asaidie kuweka hai utamaduni wa kukutana, utamaduni wa huduma, na wa kutunza kama njia kuu ya kujenga wema wa pamoja  na kufanywa na kila mtu, na wale wote wanaoishi katika ardhi hiyo”.

Kutofanyika ubatizo katika Kikanisa cha Sistine kutokana na janga

Papa Francisko pia amewasalimia kwa dhati wote ambao walikuwa wameunganishwa kupitia vyombo vya habari: “Kama mnavyojua, kwa sababu ya janga hili, leo sikuweza kusherehekea ubatizo katika Kikanisa cha Sistine kama ili kawaida. Walakini, ninataka pia kuhakikisha sala zangu kwa watoto ambao waliandikishwa, kwa wazazi wao, na wasimamizi wao na pia ninawapelekea watoto wote salamu ambao katika kipindi hiki wanapokea Ubatizo, wanapokea kitambulisho cha Kikristo, wanapokea neema ya msamaha na ya ukombozi. Mungu awabariki wote”

Kipindi cha kawaida cha kiliturujia

Baada ya ubatizo wa Bwana, sikukuu za Noeli ni kuhitimishwa sikukuu zote na kwa maana hiyo Papa amekumbusha: “Kaka na dada wapendwa, baada ya kuhitimisha kipindi cha Noeli, tunaanza tena Liturujia ya kipindi cha kawaida. Tusichoke kuomba nuru na nguvu ya Roho Mtakatifu kutusaidia kuishi kwa upendo wa mambo ya kawaida kwa namna ya kuweza kufanya mambo mengine maalum ya kushangaza. “Ni upendo ambao hubadilisha: mambo ya kawaida na  kuendelea kuwa ya kawaida, lakini yanapofanyika kwa upendo huwa ya kushangaza”, Papa amebainisha na kwamha: “ Ikiwa tunabaki wazi, watulivu katika Roho, Yeye huchochea mawazo na matendo yetu kila siku”. Na ninawatakia wote Jumapili njema. Tafadhali msisahau kuniombea. Ninawatakia mlo mwema na kwaheri!

10 January 2021, 15:46