Tafuta

VATICAN MUSEUM PANDEMIC CORONAVIRUS VATICAN MUSEUM PANDEMIC CORONAVIRUS 

Makumbusho Vatican:ufunguzi kwa upya mwezi Februari

Nia ya ufunguzi kwa upya kama hali itawezekana ni Mosi Februari. Ndiyo Mkurugenzi wa Makumbusho Vatican,Bi Barbara Jatta,amezungumza na Vatican News pia ameelezea kwamba katika miezi ya hivi karibuni,watumiaji wao kwenye mitandao ya kijamii wameongezeka sana,shukrani kwa kushirikiana na Idara ya Mawasiliano na uchapishwaji wa video za moja kwa moja.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Nia ni kufungua tena Makumbusho ya Vatican mnamo tarehe 1 Februari, japokuwa hawana uhakika ikiwa hali itaruhusu, lakini wangependa kufungua milango yake. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Vatican, Bi Barbara Jatta. Katika kufafanua zaidi juu ya ufunguzi huo wa makumbusho amesema kuwa walikuwa wamesema kwamba wataendelea kufunga hadi tarehe 16 Januari, lakini hadi tarehe 15 imebidi waelezee  nia yao ya  kuongeza muda wa  kufungwa kwa siku nyingine 15 na kufungua milango labda tarehe Mosi  Februari.  Hii ni kutokana na hali halisi ya kiafya ambayo bado haijatengemaa. Na huo ni uamuzi uliochukuliwa na wakubwa wa serikali ya Vatican. Ni kusubiri tena msululu wa kilomita saba za njia ya Makumbusho ya Vatican, na zaidi kwa sababu ya idadi ndogo iliyorekodiwa katika miezi ya majira ya joto na ambayo walikuwa wako wazi. Ni mategemo zaidi kwamba wataweza kufungua miezi ijayo ikiwa utabiri uliotolewa kwamba katika miezi ijayo, haitakuwa na shida ya kiafya zaidi au ya vizingiti zaidi vya maambukizi. Kwa maana hiyo ujumbe wa kuweza kufungua tena mkusanyo wa umma unaweza kuwa mzuri, amethibitisha Bi Jatta.

Aidha amebainisha kuwa kabla ya mahojiano na Vatican News alikuwa  ameshiriki katika mkutano kwa njia ya mtandao kwenye jukwaa la Vimeo ulioongozwa na kauli mbiu “Makumbusho zaidi”: siku zijazo za Makumbusho  kati ya shida na kuzaliwa upya, mabadiliko na mambo mapya, uliyofunguliwa na waziri Dario Franceschini wa utamaduni na Utalii, Italia. Hata hivyo akielezea juu ya kiini cha mkutano kwa njia ya mtandao, wenye kauli mbiu “Makumbusho mengi, uliyoandaliwa na Idara ya Utamaduni wa  Firenze, Italia,  tarehe 15 Januari 2021 umeoneshwa pia  ufafanuzi wa miundo ya makumbusho, ambayo huongeza kazi za utamaduni wa uhifadhia  wa aina mpya za usambazaji wa maarifa kupitia utumiaji wa majukwaa na teknolojia za ubunifu.  “Tumekuwa na utekelezaji mkubwa wa ufikiaji sio tu kwenye tovuti, bali kwa njia zetu za kijamii kama vile Youtube na Instagram”  ameelezea Bi Barbara Jatta.

Ilikuwa na maana kuu  katika kipindi kigumu cha Karantini. “Eneo la Instagram kwa hakika limechangia sana na kuchapishwa kila siku video tulizo tengeneza kwa kushirikiana na Baraza la  Mawasiliano la Vatican, lakini pia kuenezwa za moja kwa moja zilizotumwa na wazo la kuweka wazi Jumba la  makumbusho kuendelea kufanya kazi licha ya kufungwa kwake. Watunzaji, wasaidizi kutoka idara za kukarabati  walielezea walichokuwa wakifanya. Matumizi ya  vyombo vya mawasiliano kijamii ni njia ambayo, kulingana na uchambuzi inafanya kazi vizuri sana wakati wa kipindi cha karantini  na kidogo kidogo wanapokuwa wamefungua. “Tunatarajia kufungua na kwamba njia zote hizo mbili zinaweza kwenda sambamba. Na ndiyo matajio. Aidha shukrani za Tiketi nzuri kiuchumi, katika nyakati za hivi karibuni ambazo wamekuwa na nyongeza ya mabano kwa vijana wa umri wa miaka 18-30 ndani ya  umma wao oli wajongelee makumbusho.

 

16 January 2021, 19:15