Tafuta

2020.01.25 Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo nje ya Ukuta 2020.01.25 Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo nje ya Ukuta 

Ratiba ya Maadhimisho ya Papa kwa mwezi wa Januari na Februari

Imetoleawa ratiba ya maadhimisho ya Papa Francisko kwa mwezi wa Januari hadi Februari.Zaidi ya Misa ambazo Papa ataongoza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,pia tarehe 25 Januari Papa atakwenda katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo nje ya Ukuta kwa ajili ya Masifu ya jioni,ikiwa ni fursa ya kufunga Wiki ya Maombi kwa ajili Umoja wa Wakristo.

Msimamizi wa maadhimisho ya kiliturujia ya kipapa, Monsinyo Guido Marini, ametoa kalenda ya matukio ya maadhimisho yatayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa mwezi huu na mwezi Februari, kuanzia Januari tarehe 24 ijayo. Jumapili ya tatu katika kipindi cha kawaida cha mwaka ni Jumapili ambayo, kulingana na yale yaliyotangazwa katika Barua ya Kitume ya Aperuit Illis ya 2019, imetolewa kwa ajili ya kufanya tafakari na utangazaji wa Neno la Mungu, na kwa maana hiyo Papa Francisko ataongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican kuanzia saa 4.00 asubuhi.

Siku itakayofuata, Jumatatu tarehe 25 Januari katika tukio la Siku kuu ya Uongofu wa Mtakatifu Paulo na mwisho wa Wiki ya 54 ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo, Papa Francisko ataaongoza Masifu ya Pili ya jioni saa 11.30 jioni, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paul Nje ya Kuta, Roma sherehe ambayokiutamaduni inajikita kwenye matukio ya kiekumene

Ni tarehe moja tu, ambayo kwa mwezi Februari Papa ataadhimisha, siku ya Jumanne tarehe 2 katika Siku Kuu ya Kutolewa kwa Bwana Hekaluni sambamba na Siku ya XXV ya Watawa ulimwenguni, ambapo Papa ataadhimisha Misa takatifu, saa 11.30 jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na baadhi watawa wanaowakilisha Mashirika ya Kitawa na vyama vya kitume.

12 January 2021, 17:12