Tafuta

MEXICO:MADHABAHU YA MARIA MAMA YETU WA GUADALUPE MEXICO:MADHABAHU YA MARIA MAMA YETU WA GUADALUPE 

Il Papa Celam:Mkutano wa Kanisa ni ishara ya Kanisa moja la watu

Sisi sote ni wafuasi wa kimisionari wa kutoka nje ndiyo kauli mbiu ambayo imewakilisha katika Mkutano wa Kanisa barani Amerika ya Kusini na visiwa vyake katika Madhabahu ya Maria wa di Guadalupe,chini Mexico itkayoongozwa mkutano kuanzia tarehe 21 hadi 28 Novemba mwaka huu.Papa Francisko amelezea kuwasindikiza na kusisitizia umuhimu wa mtazamo wa Watu wa Mungu na sala.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya Video katika fursa ya Tukio la kuwakilishi  Mkutano kwa njia ya mtandao, Mkutano  wa Kanisa la Amerika ya Kusini na Visiwa vya Caribbien. Dominika tarehe 24 Januari 2021 katika Madhabahu ya Mama yetu wa Guadalupe, msimamizi wa Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien wamewakilisha mpango wa mkutano kuanzia tarehe 21 hadi hadi 28 Novemba 2021 kwa kuongozwa na mada” sisi sote ni wafuasi wa kimisionari wanaotoka nje”. Mwanzo walikuwa wametazamia hufanyike wakati wa kiangazi mwaka huu, lakini sasa wameahirisha kwa sababu ya janga, ambapo mkutano huo utakuwa na lengo la kutafakari kwa kina juu ya changamoto za ara  lao, kuhimiza kwa upya jihada za kichungaji na kutafuta njia mpya katika maono ya kisinodi kwa muungano wa Papa Franciso katika njia waliyoelekezwa mnamo 2007 wakati wa mkutano wa Aparecida. Kwa ajili ya asili ya kisinodi, mkutano wa kwanza wa kikanisa utakuwa na mchakato wa kusikiliza Watu wa Mungu na ushiriki wa walei, watawa kike na kiume, mashemasi, waseminari, makuhani, maaskofu, makardinali na watu wenye mapenzo mema.

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video aliomtumia Askofu Mkuu Miguel Cabrejos Vidarte, wa jimbo kuu katoliki la Trujillo, rais wa Baraza la Maaskofu wa Peru na wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini (CELAM) anasisitiza juu kusindikizwa kwa watu wa Mungu na kwa sala  Papa Francisko anaonesha nia ya kuwa nao katika wakati huo wa maandalizi hadi mwezi Novemba. Anasisitizia thamani ya Mkutano Mkuu ujao na kwamba usisubiriwe kama ule uliopita wa mwisho wa ahuko Aparecida, na ambao kwa namna moja unatakiwa uwape mafunzo  zaidi, lakini badala yake  mkutano ujao uwe ni Watu wa Mungu katika mchakato wa safari na walei wote, watawa wa kike na kiume, makardinali, maaskofu mapade, ambao kwa pamoja wanasali, wanazungumza, wanafikiri, wanajadili na kutafuta mapenzi ya Mungu.

Katika kuonesha ukaribu huo, Papa ameelekeza Askofu Mkuu Vidarte na Baraza lote la Celam, mantiki mbili ambazo zinaweza kuwasindikiza katika kipindi hicho ambacho kinafungua peo za matumaini. Ya kwanza imefupishwa katika kielelezo cha “Pamoja na watu kwa mantiki kwamba Mkutano wa Kikanisa ni ishara ya Kanisa bila kubagua. Kwa maana hiyo Papa anahimiza Mkutano huo Kanisa usiwe wa  wasomi, waliojitenga na watu waaminifu wa Mungu. Pamoja na watu, wasisahau, kuwa wao wote wanafanya kuwa sehemu moja ya watu wa Mungu, wote ni sehemu yake, na watu hawa wa Mungu ambao hawana makosa katika kuamini, kama Mtaguso unavyoeleza kwamba ndio unawapatia uwepo wao. Papa abainisha kuwa nje ya watu wa Mungu hao, ndipo wasomi wanaibuka, wasomi walioangazwa na itikadi au moja na nyingine na hiyo sio Kanisa, amesisitiza. Kanisa linajitoa katika kuumega mkate, Kanisa linajitoa kwa kila mtu, bila kumbagua yeyote. Mantiki ya pili ambayo Papa Francisko amesisitiza katika Kanisa la Amerika ya Kusini wakati wa mchakato wa maandalizi ya tukio hilo muhimu ni sala. Papa anasema “Bwana yupo katikati yetu. Na Bwana aweza kusikia kutoka pale maombi na akawa na sisi. Kwa kuhitimisha amepyaisha ukaribu wake wa sala na kuwatakia matashi mema ya kuendelea kwa ujasiri.

25 January 2021, 17:46