Tafuta

2021.01.11 Wanawake katika Kanisa 2021.01.11 Wanawake katika Kanisa 

Papa:wahudumu wa masomo na huduma ya altareni hata wanawake

Papa Francisko amebebadili kifungu cha Kanoni ya sheria na kukifanya kuwa cha kitaasisi kama ilivyokuwa tayari ipo kwenye mchakato.Kuanzia sasa wanawake wanaweza rasimi kutoa huduma ya kusoma Neno na huduma ya altareni.

SR. ANGELA RWEZAULA, - VATICAN NEWS

Papa Francisko ameridhia kwa barua yake ya motu proprio, kwamba huduma ya Usomaji wa masomo(Lector) na kuhudumia altareni (Acolyte) tangu sasa vinaanzishwa hata kwa wanawake katika hali thabiti na ya kitaasisi na mamlaka maalum. Wanawake ambao wanasoma Neno la Mungu wakati wa maadhimisho ya Liturujia, wanamsaidia mshehereshaji wa Ibada au katika maandamano ya kidini na kutoa huduma yao katika altare, kama ilivyo hata kwa wahudumu wengine au wanaotoa Ekaristi, kwa hakika siyo jambo jipya, kwa maana jumuiya nyingi ulimwenguni zilikwisha anza tayari hatua hiyo iliyoidhinishwa na maaskofu.

Hadi sasa, hata hivyo, yote yote yalifanyika bila mamlaka halisi ya taasisi, kinyume na kile kilichokuwa kimenzishwa na Mtakatifu Paulo VI, ambapo mnamo mwaka 1972 alikuwa ameamua kwamba huduma hizi zihifadhiwa kwa wanaume tu. Kwa sasa Papa Francisko katika mwendelezo wa kufanya mang’amuzi yaliyotokea katika Sinodi za mwisho za Maaskofu, amependa kufanya uwepo huu wa kike kwenye taasisi katika huduma  ya Altare.

Kwa njia ya Barua yake ya Motu Pripio yenye jina “Spiritus Domini”, yaani ‘Roho wa Mungu’, na ambayo inasasisha Ile ya kwanza ya Kanoni ya Sheria ya kifungu 230 ya Haki ya Kanoni, Papa kwa njia hiyo anathibitisha kuwa wanawake wanaweza kutoa huduma hizi na kwamba zinahusishwa pia kupitia mchakato wa kitendo cha kiliturujia ambacho taasisi inawaweka. Papa Francisko amefafanua jinsi alivyopendelea kuyapokea mambo haya mengi yaliyotoka kna mamombi katika sinodi mbali mbali na kuandika kuwa  sasa  imefikia miaka hii ya mwisho ya kuwa na maendeleo ya Mafundisho ya Kanisa ambayo yanaweka nuru kwa jinsi huduma zingine zilizoanzishwa na Kanisa zina msingi wa hali ya pamoja ya kubatizwa na ukuhani wa kifalme uliopokelewa katika sakramenti ya ubatizo”

Walakini Papa Francisko “anawaalika waamini watambue kuwa hii ni huduma ya kilei, ambayo kimsingi ni tofauti na huduma rasimi ambayo hupokelewa na sakramenti yautaratibu wa kuwekwa wakfu”. Katika barua yake ya Motu Proprio, inasindikizwa na Barua aliyo mwandikia Rais wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Kardinali Luis Ladaria, mahali ambapo Papa Francisko anaelezea kwa kirefu, sababu za kitaalimungu za uchaguzi wake, kwa kuunganisha na upyaisho uliowekwa na Mtaguso wa Pili wa Vatican na dharura ya kugundua kwa upya uwajibikaji wa wabatizwa wote katika Kanisa, na kwa namna ya pekee katika mtindo wa utume wa kilei. Papa Francisko katika Barua kwa Kardinali Ladaria, baada ya kunukuu maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II, anasema kwamba “kulingana huduma ya Wakfu, Kanisa kwa vyovyote vile haina uwezo wa kuwapa wanawake wawekwe wakfu  wa kikuhani”,na kwa  kuongeza anaandika  kuwa “lakini kwa huduma ambazo hazina wakfu inawezekana, na ndiyo maana  leo inaonekana fursa, ya kushinda hifadhi hiyo”.

11 January 2021, 14:38