Tafuta

Vatican News
2021.01.30 Mkutanio wa Papa na wahudumu wa Ofisi ya Katekesi Kitaifa ya Baraza la Maaskofu Italia(CEI). 2021.01.30 Mkutanio wa Papa na wahudumu wa Ofisi ya Katekesi Kitaifa ya Baraza la Maaskofu Italia(CEI).  (Vatican Media)

Papa Francisko:Mtaguso ni magisterium ya Kanisa lazima ifuatwe!

Papa Francisko ametoa hotuba yake ambapo kwa sehemu kubwa bila kusoma amekazia magisterium ya Kanisa alipokutana na wahudumu wa Ofisi ya Katekesi Kitaifa,katika fursa ya kutimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.Papa amesisitiza umuhimu wa kutenda na kukumbusha kuwa mtaguso ni magisterium ya Kanisa na lazima ifuate.Ni mwaliko wa Kanisa la Italia kuanzisha mchakato wa mshikamano kwa ngazi ya kitaifa kijimbo na kijumuiya

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko, Jumamosi tarehe 30 Januari 2021, amekutana na wajumbe wahudumu wa  Ofisi ya Katekesi ya Baraza la Maakofu Italia (CEI). Ni katika fursa ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa ofisi hiyo. Katika hotuba yake awali ya yote amewakaribisha na kumshukuru Kardinali Guartiero Bassetti, Rais wa Baraza hilo kwa maneno yake, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Askofu Russo, na wote ambao wanahudumu katika Kanisa la Italia kwa mantiki ya Katekesi. Ameshukuru kushikirikishana nao katika kufanya kumbu kumbu ya miaka 60 tangu kuzaliwa kwa Ofisi ya Katekesi Kitaifa. Taasisi ambayo Papa amesema kabla ya kuwa chini ya Baraza la Maaskofu, ilikuwa ni chombo muhimu kwa ajili ya upyaisho wa katekesi baada ya Mtaguso II wa Vatican . Tukio hili ni fursa yenye thamani kwa ajili ya kufanya kumbu kumbu na kushukuru zawadi ambazo zimepeokelewa na kupyaisha roho ya tangazo. Kwa lengo hilo, Papa amependa kuwashirikisha mambo matatu ambayo ni matarajio yake kuwa yanaweza kuwasaidia katika kazi ya miaka ijayo.

Katekesi na Kerygma

Akianza kufafanua mambo hayo matatu, la kwanza amesema ni Katekesi na Kerygma, yaani tangazo. Katekesi ni mwangwi wa Neno la Mungu. Katika kueneza kwa imani ya Andiko, ni Kitabu na siyo ruzuku labda kama ingekuwa ya kwanza” kama inavyo kumbusha Hati msingi ya (CEI, upyaisho wa Katekes,107). Katekesi ni mawimbi marefu ya Neno la Mungu kwa ajili ya kueneza maisha na furaha ya Injili. Shukrani kwa simulizi ya Katekesi, Andiko Takatifu linageuka kuwa mazingira ambamo ni kuhisi kuwa sehemu ya historia hiyo ya wokovu, kwa kukutana na mashuhuda wa imani. Katekesi ni kujikita katika mchakato wa bega kwa bega na kusindikiza historia hii. Hii inatoa chachu ya safari ambamo kila mmoja anapata hatua yake, na ili maisha ya kikristo yasilale na wala kufanana, lakini ni kuthamanisha umoja wa kila mtoto wa Mungu. Katekesi pia ni mchakato wa mafundisho ambayo daima yanaendelea na mazungumzo na liturujia, mantiki ambayo inaanza na ishala ambazo bila kulazimisha, zinazungumzia maisha na kuweka alama ya neema. Moyo wa fumbo ni kerygma na kerygma ni mtu yaani Yesu Kristo. Katekesi ni nafasi muafaka wa kukutana binafsi na Yeye. Kwa maana hiyo lazima kuuishi uhusiano huo kibinafsi. Hakuna katekesi ya kweli bila ushuhuda wa wanaume na wanawake wenye mwili na mfupa. Ni nani hasiyekumbuka angalau moja ya katekesi. Walio kuwa wa kwanza  wa Katekesi  ni wao, wajumbe wa Injili, ambao mara nyingi walei,wanathubutu kwa ukarimu ili kushirikisha uzuri wa kuwa wamekutana na Yesu.

Katekesita ni nani?

Je katekista ni Nani? Ni yule anayelinda na kuongoza kumbu kumbu ya Mungu: Anajilisha yeye na kukesha kwa ajili ya wengine. Ni mkristo ambaye anaweka kumbu kumbu  ya huduma ya tangazo; si kwa ajili ya kujionesha, si kwa ajili ya kujizungumzia binafsi, lakini ni kuzungumza ya Mungu, ya upendo wake, na uaminifu wake ( Mahubiri Siku ya Katekesi mwaka wa Imani 29 Sept 2013). Papa Francisko ameongeza kusema kuwa kwa upande wa katekista, lazima kugusia wazazi na babu na bibi, ambao lazima warithishe imani kupitia lugha asili, yaani kilugha. Katekista hasiyejua kufundisha katika lugha ya kuzaliwa kwa vijana na watoto siyo rahisi kueleweka hivyo lugha ya kuzaliwa inazungumza  kwa undani zaidi. Papa akitoa mfano mwingine amesema jinsi ambavyo  daima anaguswa na historia ya wamakabayo wale ndugu saba. Mara mbili au tatu wanasema kuwa mama yao alikuwa akizngumza nao kwa lugha ya asili yaani kilugha. Papa amesema ni muhimu kupitisha imani ya kweli kwa njia ya lugha asili. Makatekista wanapaswa kujifunza na kuineza mafundiso  kwa njia ya lugha asili, ile lugha ambayo inatoka moyoni na wamezalia ndani ya familia,  na ndiyo iliyo karibu kwa wote. Ikiwa hakuna lugha asili Papa amethibitisha imani haiweze kurithishwa yote na vizuri!

Katekesi na wakati ujao

Jambo la pili ambalo Papa Francisko amependa kushirikishana nao ni kuhusu Katekesi na wakati ujao. Mwaka jana ilikuwa ni miaka 50 ya Hati ya Upyasiho wa katekesi ambapo Baraza la Maaskofu Italia walikuwa wanatambua maelekezo ya Mtaguso. Kwa upande huo Papa Francisko amependa kutumia maneno ya Mtakatifu Paulo VI aliyotoa wakati wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI)  hasa mara baada ya Mtaguso II kwamba: “lazima kutazama Mtaguso kwa shukrani kwa Mungu na kwa imani ya wakati ujao wa Kanisa: hiyo itakuwa katekisimu kubwa ya nyakati mpya (23 Juni 1966). Na kwa kurudi katika mada  hiyo, katika fursa ya Mkutano wa Katekesi Kimataifa, aliongeza kusema:“ Ni kazi ambayo inazaliwa bila kuchoka, na inapyaishwa bila kuchoka  kwa ajili ya katekesi ambayo inahusu matatizo yanayosonga moyo wa mtu ,ili kumpeleka katika kisima kilichofichika; zawadi ya upendo ambao unaumba na kuokoa” ( 25 Sept 1971). Kwa njia hiyo  Papa Francisko amesema “Katekesi ambayo ilitokana na Mtaguso inaendelea katika usikivu wa moyo wa mtu  na daima kwa masikio yaliyo wazi, pia daima umakini wa kujipyaisha. Na hiyo ndiyo  magisterium.

Ama unakaa na Kanisa kwa hiyo unafuata Mtaguso au ahuko na Kanisa

Mtaguso ni magisterium ya Kanisa. Ama unakaa na Kanisa na kwa hivyo unafuata Mtaguso, na ikiwa haufuati Mtaguso au unautafsiri kwa njia yako mwenyewe, kwa mapenzi yako, hauko pamoja na Kanisa. Kwa wakati huu lazima tudai, kwa ukali. Mtaguso haupaswi kujadiliwa, kuwa na zaidi ya haya ... Hapana, Mtaguso huko hivyo. Na shida hii ambayo tunapata, ya uchaguzi wa Mtaguso, imerudiwa katika historia na Mitaguso mingine”. Papa amekazia. Akiendelea amesema “Inanifanya nifikirie sana juu ya kikundi cha maaskofu ambao waliondoka baada ya Mtaguso wa I wa  Vatican, kikundi cha walei, vikundi hivyo, ili kuendelea na mafundisho ya kweli ambayo hayakuwa ya Mtaguso wa I  wa Vatican.  “Sisi ni Wakatoliki wa kweli”.  Leo hii wanawaweka wakfu  wanawake. Mtazamo mkali  wa kulinda imani bila magisterium ya Kanisa hupelekea uharibifu. Papa ametoa onyo “Tafadhali, hakuna kufanya makubaliano kwa wale wanaojaribu kuwasilisha katekesi ambayo haikubaliani na magisterium ya  Kanisa”.

Baada ya Mtaguso Kanisa Italia lilikuwa na uwezo wa kupokea ishara

Papa akiendelea amesema Kama ilivyokuwa baada ya Mtaguso, Kanisa la Italia lilikuwa tayari na uwezo wa kupokea ishara na umakini wa nyakati na kwa namna hiyo hata leo hii linaalikwa kutoa katekesi iliyopyaisha na ambayo inaongozwa na mantiki ya kichungaji, upendo, liturujia, familia, utamaduni, maisha ya kijamii,na kiuchumi…. kutoka katika mzizi wa Neno la Mungu. Kupitia kisiki cha hekima kichungaji mikakati inachanua yenye matunda ya mantiki tofauti za maisha. Katekesi ni mchakato maalum kama ulinzi wa Kanisa lenye shughuli ya kusoma ishala za nyakati na kupokea changamoto za wakati uliopo na ujao. Hatupaswi kupogopa anasema Papa kuzungumza lugha ya wanawake na wanaume wa leo hii. Hatupaswi kuogopa kusikiliza masuala yasiyo suluhishwa, udhaifu  na ukosefu wa usalama.  Papa Francisko amewatia moyo wanendelee mbele. Hawapaswi kuogopa kufanya kazi kwa njia ya zana mpya. Katika miaka ya 70,  katekisimu ya Kanisa nchini  Italia ilikuwa maalum na ilisifika; hata katika nyakati za sasa zinahitaji akili na ujasiri wa kufanya kazi na zana zilizosasishwa na ambazo zinamwonesha mtu wa leo utajiri na furaha ya kerygma.

Katekesi na Jumuiya

Papa Francisko akifafanua jambo la tatu ni kuhusu Katekesi na Jumuiya. Katika mwaka huu ambao umeguswa na kutengwa na maana ya upweke kwa sababu ya Janga , mara nyingi kumekuwa na tafakari juu ya ushiriki na ambao ni msingi wa jumuiya. Virusi vimeweza kuchimba katika kiungo hai  cha maeneo yetu hasa ya maisha na kusababisha woga, shuku, ukosefu wa imani na usalama. Janga limeweka mazoea na tabia zilizowekwa hivyo kutuchochea ili kufikiria tena namna ya kuwa jumuiya. Tumeelewa, kiukweli, kwamba hatuwezi kufanya peke yetu na kwamba njia pekee ya kutoka ndani ya shida ni bora kutoka kwa pamoja,  tukikumbatia jumuiya tunayoishi na kusadikika zaidi. Kwa sababu jamuiya sio mkusanyiko wa watu binafsi, lakini ni familia ambayo inaweza kujumuika, mahali pa kutunza kila mmoja, vijana wa wazee na wazee wa vijana, sisi wa leo  hii na wa wale watakaokuja kesho. Ni kwa kugundua kuishi hali ya kijumuiya tu kwamba kila mmoja ataweza kupata hadhi yake kikamilifu.

Huu ndiyo wakati ya wasomi na jumuiya kubwa

Katekesi ni tangazo ambalo haliwezi kuacha kuweka katikati mwelekeo wa ukuu wa jumuiya. Huu sio wakati wa mikakati ya wasomi na jamuiya kubwa. Je Jumuiya kubwa ni nini? Ni watu watakatifu waaminifu wa Mungu. Huwezi  kwenda  nje ya watu waaminifu wa Mungu, ambao kama Mtaguso usemavyo  “hawashindwi katika kuamini”. Daima ni watu watakatifu wa Mungu. Na badala yake, kutafuta ushirika wa wasomi kunafanya kutengana na watu wa Mungu, labda na fomula za hali ya juu; lakini unapoteza ushiriki wa Kanisa ambalo ni watu watakatifu waaminifu wa Mungu. Huu ni wakati wa kuwa mafundi wa jumuiya zilizo wazi ambazo zinajua jinsi ya kuthamanisha na kukuza talanta za kila mmoja. Ni wakati wa jamuiya za wamisionari, huru na zisizo tafuta maslahi yake, au ambazo hazitafuti umuhimu na faida, lakini zinatembea njia za watu wa wakati wetu, wakiinamia juu ya wale walio pembezoni.

Kanisa liwe zaidi na walisahauliwa, wasio wakamilifu 

Ni wakati wa jamuiya  ambayo inatazama kwa macho  vijana waliokata tamaa, kwamba wanakaribisha wageni na kuwapa tumaini waliovunjika moyo. Ni wakati wa jamuiya kufanya mazungumzo bila woga na wale ambao wana maoni tofauti. Ni wakati wa jamuiya ambayo, kama Msamaria Mwema, wanajua jinsi ya kukaribia wale waliojeruhiwa na maisha, ili kufunga majeraha yao kwa huruma. Papa amesisititiza wasisahau neno hili: huruma. “Ni mara ngapi katika Injili ya Yesu inasemwa: “Naye alikuwa na huruma”, “akawa na huruma”. Na kama alivyosema katika Mkutano wa Kanisa huko Firenze Italia, Papa ameongeza kusema kuwa anatamani Kanisa “liwe karibu zaidi na walioachwa, waliosahaulika, wasio kamili. […] Kanisa lenye furaha na uso wa mama, ambalo linaelewa, linasindikiza, linabembeleza”.

Hadhi ya mtu inadumishwa na udugu kati ya mwanadamu

Papa Francisko amesema kwamba kile kilichotajwa wakati ule wa ubinadamu wa Kikristo pia ni halali kwa katekesi. Hiyo inathibitisha kabisa hadhi ya kila mtu kama Mwana wa Mungu, inadumisha  ushirika msingi wa udugu  kati ya kila mwanadamu, inatufundisha kuelewa kazi, na kukaa katika uumbaji kama nyumba ya pamoja, inatoa sababu za uchangamfu na ucheshi, hata katikati ya maisha ambayo mara nyingi ni magumu sana”(Hotuba katika Mkutano wa Kitaifa wa V wa Kanisa la Italia, Firenze, 10 Novemba 2015). Papa Francisko amesema “Nilitaja Mkataba wa Firenze. Baada ya miaka mitano, Kanisa la Italia linapaswa kurudi kwenye Mkataba wa Firenze, na linapaswa kuanza na  mchakato wa Sinodi ya kitaifa, jumuiya kwa jumuiya, majimbo kwa majimbo, hata mchakato huu pia utakuwa katekesi. Katika Mkataba wa Firenze kuna maoni halisi ya njia ya kwenda katika Sinodi hii. Sasa, ni wakati wa kuanza tena. Na kuanza kutembea”. Papa Francisko anawaalika waendelee kusali na kufikiria kwa ubunifu wa katekesi ambayo inajikita juu ya kerygma, ambayo inatazama wakati ujao wa jumuia zetu, na iweze sababu daima inayosimika mzizi katika Injili, udugu na jumuishi.

HOTUBA YA PAPA KWA CEI
30 January 2021, 17:35