Tafuta

Vatican News
Ujumbe wa Siku ya Amani duniani 2021 Ujumbe wa Siku ya Amani duniani 2021 

Ujumbe wa Siku ya Kuombea Amani Duniani 2021:Utamaduni wa utunzaji kama mchakato wa amani

Katika ujumbe wa Papa Francisko wa maadhimisho ya Siku ya 54 ya Kuombea Amani Duniani kwa Mwaka 2021,unaongozwa na kauli mbiu: “Utamaduni wa utunzaji kama mchakato wa amani”.Kwa maana hiyo ujumbe umegawanyika katika vipengele tisa ambavyo mantiki msingi wake ni utunzaji kuanzia Mungu Muumbaji asili ya wito wa ubinadamu katika kutunza, Mungu mfano wa utunzaji, hadi kufikia kuwa hakuna amani bila kuwa na utamaduni wa utunzaji.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Tarehe 17 Desemba 2020  Papa Francisko ametoa ujumbe kwa ajili ya  maadhimisho ya Siku ya 54  ya kuombea Amani duniani, itakayoadhimshwa tarehe Mosi  Januari 2021, sambamba na Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu. Katika ujumbe huo umegawanyika katika vipendele 9 vyenye mantiki tofauti. Kipengele cha kwanza kinahusu Utamaduni  wa utunzaji  kama mchakato wa amani, cha pili  Mungu Muumbaji, asili ya wito wa ubinadamu katika utunzaji, cha tatu  Mungu muumbaji, mfano wa utunzaji, cha nne ni  utunzaji katika kazi ya Yesu, cha tano ni  utamaduni wa utunzaji katika maisha ya wafuasi wa Yesu, cha sita ni  Misingi ya mafundisho jamii ya Kanisa kama msingi wa utamaduni wa utunzaji , cha saba  ni Dira kwa ajili ya kupindua kwa pamoja, nane ni  kuelimisha utamaduni wa utunzaji  na kipengele cha mwisho  kinafafanua kuwa hakuna amani bila utamaduni wa utunzaji. Papa Francisko katika kuanza kufafanua kipengele cha kwanza kama utangulizi wa ujumbe huo katika mwanzo wa mwaka, anapendelea kutoa salam kwa wakuu wa Nchi na serikali, wahusika wa Mashirika ya Kimataifa, viongozi wa kiroho na waamini wa dini mbali mbali, wanawake na wanaume wenye mapenzi mema. Kwa wote anawatakia matashi mema ili mwaka  uweze kuwa na maendeleo ya ubinadamu katika mwelekeo wa  njia za udugu, haki na amani kati ya mtu, jumuiya, watu na mataifa. Mwaka 2020 umekuwa na mgogoro wa kiafya wa Covid-19, uliobadilisha sekta nyingi ulimwenguni, na kuongezea mgogoro kati yao na  ambazo tayari zipo kama vile mabadiliko ya tabianchi, uhaba wa  vyakula, uchumi na uhamiaji na kusababisha mateso makubwa na mahangaiko. Papa Francisko anafikiria awali ya yote wale walipoteza wanafamilia zao, mtu mpendwawa, lakini pia hata wale waliobaki bila kazi.

Kumbu kumbu maalum imewaendeea madaktari, wauguzi, wanafamasia, wafungwa, watu wa kujitolea, makuhanis wasimamizi wa vikanisa na vituo vya kiafya na, vituo vingine ambao ambavyo wameendelea kutoa hduma, kwa ugumu mkubwa na sadaka, hadi wengine kufariki wakiwa wanasidia kutokana na kuambukizwa na wagonjwa. Kwa kuwapa heshima watu hao, Papa Francisko amerudia kutoa wito kwa wahusika wote wa kisiasa na sekta binafs, ili wachukue hatua zinazofaa kuhakikisha hupatikanaji wa chanjo ya kuzuia Covid-19  na katika teknolojia msingi ya  lazima kwa ajili ya kusaidia wagonjwa na wale ambao ni maskini zaidi na wadhaifu zaidi. Hata hivyo Papa Francisko amebainisha kuwa  inaumiza kuona kwamba karibu na idadi kubwa ya shuhuda za upendo na mshikamano, kwa bahati mbaya kuna aina mpya za utaifa, ubaguzi, ubaguzi wa rangi hata vita na migogoro ambayo inazidisha vifo na uharibifu. Haya na mengine ambayo yameonekana katika safari ya ubinadamu, katika mwaka ambao umpeta, yameonesha umuhimu wa kutunzana mmoja na mwingine na kazi ya uumbaji ili kujenga jamii yenye msingi wa uhusiano wa kidugu. Kutokana na hayo yote Papa Francisko anabainisha kuwa amechagua ujumbe huu kwa mada ya “utamaduni wa utunzaji kama mchakato wa amani. Kwa maana hii, utamduni wa kutunza kwa ajili ya kuondoa utamaduni wa kutojali, kubagua, dhidi ya ugomvi ambao leo hii unaonekana sana.

Katika kipengele cha pili kuhusu Mungu Muumbaji, ni asili ya wito wa ubinadamu katika kutunza. Papa Francisko anabainisha kuwa katika tamaduni nyingi za kidini, kuna hadithi ambazo zinasimulia asili ya mtu, uhusiano wake na Muumba, asili na viumbe vyote. Katika Biblia kwenye kitabu cha Mwanzo, kinaonesha tangu mwanzo umuhimu wa kutunza au kulinda mpango  wa Mungu kwa ajili ya ubinadamu, kwa kuangazia zaidi uhusiano kati ya mtu (Adamu) na ardhi (adamah) na katika ya ndugu. Kuzaliwa kwa Kaini na Abeli kunazaa historia ya ndugu, uhusiano ambao baadaye utatafsiriwa hasi kwa maana ya utetezi au ulinzi.  Baada ya kumuua kaka yake Abeli, Kaina alijibu Mungu hivi: “kwani mimi labda ni mlinzi wa ndugu yangu?( Mw 4,9).  Ndiyo kwa hakika Kaini ni mlinzi wa ndugu yake, Papa amebainisha. Katika simulizi hii ya kizamani iliyojaa utajiri wa kina na ishara, ilikuwa tayari imekwisha sikika leo hii kuwa kila kitu kiko katika uhusiano na kwamba, kutunza kwa dhati kwa ajili ya maisha yetu na uhusiano wetu na asili ni mambo yasiyotengenishwa na udugu, hakika na uaminifu mbele ya wengine.

Kipengele kingine cha tatu kinasema Mungu ni mfano wa utunzaji, ambapo Papa anabainisha kuwa katika Andiko Takatifu, linamwakilisha Mungu aliye zaidi ya kuwa Muumbaji, kama Yule ambaye anatunza viumbe vyake, kwa namna ya pekee, Adamu na Eva na watoto wao. Hata Kaini mwenyewe licha ya kuangukiwa na balaa kwa sababu ya uhalifu, alio utekeleza anapokea zawadi ya Muumba ishara ya ulinzi ili maisha yake yaweze kulindwa (Mw 4,15). Suala hili wakati linadhihirisha hadhi isiyo kiukwa ya binadamu, aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu linaonesha hata mpango wa Mungu kwa ajili ya kuhifadhi maelewano ya kazi ya uumbaji, kwa sababu amani  na vurugu visiweze kukaa katika nyumba moja. Jambo moja la kukumbuka ni utamaduni wa kinabii ambapo uelewa ukuu wa kibiblia kuhusu haki unajionesha kwa namna ambayo jumuiya ndani mwake inawatazama wadhaifu. Ndiyo maana Amosi (2,6-8; 8) na Isaiya (58), kwa namna ya pekee, wanapaza sauti zao kwa ajili ya haki kwa maskini ambao pamoja na  kuathirika kwao na ukosefu wa nguvu, wanasikilizwa na Mungu tu ambaye anawatunza wao, (Zab  34,7; 113,7-8).

Papa Francisko katika kipengele cha nne amejitika juu ya utunzaji katika  utume wa Yesu. Maisha na shughuli za Yesu imejikita kwenye ncha ya maonesho ya upendo wa Baba kwa ubinadamu (Yh 3,16).  Katika Sinagogi ya Nazareth, Yesu alijionesha kama Yule ambaye Bwana amempaka mafuta, na kumtuma apeleke habari njema kwa maskini, awatangazie wafungwa uhuru wao na vipofu wapate kuona  na kuwaweka uhuru walio mateka (Lk 4,18). Kwa maana hiyo mchungaji mwema anatunza kondoo wake (Yh 10,11-18; Ez 34,1-31); Ni Msamaria mwema ambaye anainamia mtu aliyejeruhiwa, anamfunga majeraha na kumtunza yeye (Lk 10,30-37). Katika hitimisho la utume wake, Yesu anauweka utunzaji wetu kwa kuutoa juu ya msalaba na kutukomboa na utumwa wa dhambi na kifo namna hiyo. Kwa njia ya zawadi yake hiyo ya maisha na sadaka yake, Yeye alifungua njia ya upendo na anamwambia kila mmoja “Nifuate”. Hata wewe fanya hivyo ( Lk 10, 37).

Papa Francisko akiendelea na ujumbe huu wa  siku ya amani kwenye kipengele cha tano kisemacho utumaduni wa utunzaji katika maisha ya wafuasi wa Yesu, anabainisha kwamba, matendo ya huruma, ya kiroho na kimwili yalikuwa ni kiini katika huduma ya upendo wa Kanisa la kwanza. Wakristo wa kizazi cha kwanza, walikuwa wanajikita katika kushirikishana ili hasiwepo kati yao mwenye kuhitaji. (Mdo 4,34-35) na walikuwa wanajitahidi kuifanya jumuiya kuwa kama nyumba ya ukarimu, iliyofunguliwa kwa kila hali ya binadamu, iliyo tayari kubeba walio wadhaifu zaidi. Ndiyo ikajitokeza ukawaida ya kujitoa kwa ajili ya kuwashibisha maskini, kuzika wafu, kulisha yatima, wazee na waathiriwa wa majanga ya asili na kama vile manusura. Na wakati wa kipindi kilichofuata, hasa wakristo walipoanza kupoteza kidogo ukarimu na mwamko, baadhi ya Mababa wa Kanisa walisisitiza kwamba mali binafsi imewekwa na Mungu kwa ajili ya wema wa pamoja. Umasikini wa kipindi kile ukatoa nguvu mpya katika huduma ya Caritas kikristo.  Historia inakumbusha idadi kubwa ya ufadhili (…). Zilhaguliwa taasisi nyingi kwa ajili ya kutoa faraja kwa ubinadamu uaoteseka katika mahospitali,  nyumba za kutunza maskini, vituo vya watoto yatima na nyumba za kutunza wagonjwa mahututi, nk.

Na katika kipengele cha sita  kinahusu Misingi ya mafundisho jamii ya Kanisa kama msingi wa utamaduni wa utunzaji. Papa Francisko anabainisha kuwa asili ya ushemasi, ilijitajirisha kutokana na Mababa na kuuishwa kwa njia ya karne nyingi, katika shughuli za upendo wa shuhuda nyingi angavu za imani na ndiyo ikawa moyo unaodunda wa Mafundisho ya Kanisa, kwa kuwatolea watu wote wenye mapenzi mema kama tunu ya urith msingi, mantiki na maelekezo ambayo yanachota hali halisi ya utunzaji. Hii ni katika kuhamsasisha hadhi ya kila binadamu, mshikamano na maskini, wasiokuwa na mlinzi, kukuza wema wa pamoja na kutunza kazi ya uumbaji.

Papa Francisko katika kipengele cha saba kinafafanuliwa kwa kirefu, kikiwa na kinaonesha dira kwa ajili ya kupindua kwa  pamoja. Katika kipindi ambacho kinatawaliwa na utumaduni wa ubaguzi na mbele ya ukosefu wa usawa, ndani ya Mataifa na kati ya wengine, Papa Francisko ametaka kuwaalika wahusika wa Mashirika ya Kimataifa na Serikali, ulimwengu wa uchumi na ule wa kisayansi wa mawasiliano jamii na Taasisi za elimu ili kuchukua mikononi mwao ile dira ya misingi aliyoikumbusha kwa ajili ya kupindua  pamoja  katika machakato wa utandawazi, yaani kupindua kweli ubinadamu.  Papa Francisko katika hili anatama wahamiaji. Watu wamelazaimika kukimbia, kuacha nyuma yao si tu nyumba zao binafsi lakini pia hata historia ya familia na mizizi ya utamaduni. Sababu za migogoro mingi lakini matokeo yake daima ni yale yale yaani ni  uharibifu na mgogoro wa kibinadamu. Lazima kusimama na kujiuliza: ni kitu gani kimepelekea ukawaida wa migogoro ya ulimwengu? Na zaidi ni jinsi gani ya kuwa na uongofu wa mioyo yetu na kubadilisha akili yetu kwa ajili ya kutafuta kweli amani katika mshikamano na udugu? Ni asilimali ngapi zimepotea kwa ajili ya silaha kwa namna ya pekee zile za kinyuklia, rasilimali ambazo zingeweza kutumiwa kwa ajili ya kipaumbele zaidi katika kuhakikisha usalama wa watu, uhamasishaji wa wat una ule wa maelfu fungamani ya watu, mapambano dhidi ya umaskini na uhakika wa mahitaji ya kiafya. Hata hivyo kwa upande huo, yameoneshwa kwenye mwanga  matatizo ya ulimwengu wa sasa kama janga la Covid-19, na mabadiliko ya tabianchi. Uamuzi wa ujasiri ungekuwa wa kubadilisha fedha ambazo badala ya kunua silaha na mahitaji ya kijeshi, ukawa mfuko wa ulimwengu ili kuweza kuchangia maendeleo ya Nchi zilizo maskini zaidi.

Katika kipengele cha nane kinahusu kuelimisha utamaduni wa utunzaji, Papa Francisko anasisitiza kuwa  uhamasishaji wa utumaduni wa kutunza unahitaji mchakato wa elimu na dira msingi kijamii ambayo inajikita katika lengo hili na chombo aminifu kwa mantiki tofauti zinazohusiana na hayo. Kwa maana hiyo Papa Francisko ametoa baadhi ya mifano kama vile anaandikia,  daima kuwepo na ushirikiano na familia na sekta nyingi za elimu ambazo ni shule, vyuo vikuu na vingine ambavyo vinavyafanana kwa ajili ya mantiki hiyo, na vingine vya mawasiliano kijamii. Elimu ya kutunza inazaliwa ndani ya familia kiini  asili na msingi wa jamii, mahali ambamo ni kujifunza kuishi katika uhusiano na kuheshimiana. Aidha Papa anatoa mfano mwingine kwamba Dini kwa kwa ujumla na viongozi wa kidini kwa namna ya pekee wanayo nafasi nzuri sana katika kueneza kwa waaminu wote na kwa jamii nzima thamani ya mshikamano, katika kuheshimu tofauti, kukaribisha na katika kutunza walio wadhaifu. Kwa wale wote ambao wanatoa huduma ya watu, katika mashirika ya kimataifa, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali, matendo ya  kitume katika elimu na wale ambao kwa namna nyingine kwa jina fulani, wanajitoa kwenye nyanja ya elimu na katika utafiti. Kwa maana hiyo  Papa Francisko amepyaisha kuwatia moyo ili waweze kufikia matazamio ya elimu iliyo wazi zaidi na jumishi. Yenye uwezo kusikiliza kwa uvumulivu, kuwa na mazungumzo ya kujenga na uelewa mkubwa.

Kwa kuhitimisha katika kipengele cha  tisa  Papa Francisko anabainisha kuwa hakuna amani bila kuwa na utamaduni wa utunzaji. Utamaduni wa utunzaji, jitihada za pamoja na kuunga mkongo na kushiriki kulinda na kuhamasisha hadhi na wema wa wote, kama ilivyo tabia ya kuwa na nia, kuzingatia, huruma, upatanisho na uponyaji, kuheshimiana na kukubalika, hufanya njia ya upendeleo wa kujenga amani, katika kukaribishana na kujenga njia ya ujenzi wa amani. Katika sehemu nyingi ulimwenguni Papa amesisitiza, inahitajika michakato ya amani ambayo ipelekee kuponesha majeraha. Kuna haja ya kuwa wahunzi wa amani walio tayari kuanzisha michakato ya uponyaji na kuhamasisha makutano na shauku. Kama wakaristo tunazingatia mtazamo unaolekezwa kwa Bikira Maria nyota ya bahari na Mama wa Matumaini. Kwa pamoja tushirikiane ili kuelekeza katika upendo na amani, udugu na mshikamano, wa kusaidiana kwa pamoja na kukaribishana. Tusiangushwe na vishawishi vya kutojali wengine hasa walio wadhaifu zaidi, tusizoee kugeuza mtazamo mahali pengine, badala yake jitihada zetu kila siku za dhati ziwe kwa ajili ya kuunda jumuiya yenye kuwa na ndugu ambao wanakaribishana na kutunzana mmoja na mwingine.

UJUMBE WA SIKU YA AMANI 2021

 

17 December 2020, 15:59