Tafuta

Vatican News

Papa Francisko:tushukuru kila jambo tumepewa kila kitu bure na Mungu!

Katika Katekesi ya Papa ikiwa ni ya mwisho kwa mwaka 2020, amejikita kufafanua juu ya sala ya ushurukuru.Sisi sote tumezaliwa shukrani kwa yule aliyetamani maisha yetu.Na hiyo ndiyo moja ya safu ndefu ya madeni tuliyo nayo wakati wa kuishi madeni ya kutoa shukrani kwa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ikiwa ni tarehe 30 Desemba, siku moja kabla ya kuhitimisha mwaka 2020, Jumatano asubuhi, Papa Francisko ameendelea na katekesi yake ya mwisho kwa mwaka huu kwa kujikita katika sala ya shukrani. Ameongozwa na tukio moja kutoka Mwinjili Luka. Wakati Yesu alikuwa njiani akakutana na wakoma kumi wakamwomba “Yesu, mwalimu utuhurumie” (Lk 17,13). Hii inatambulika kuwa  wagojwa wa ukoma, katika mateso ya kimwili yalikuwa yanaongezewa  hata yale ya ubaguzi kijamii na kidini, kwani walikuwa wamebaguliwa. Yesu lakini hakuhepuka kukutana nao. Na mara nyingi alikwenda zaidi ya vizingiti vilivyowekwa na sheria na kuwagusa wagonjwa. Na kuwakumbatia na kuwaponya. Katika kesi hii lakini hakuwagusa.  Kwa mbali Yesu anawaalika waende kujitambulisha kwa makuhani ambao walikuwa wamepewa jukumu kwa mujibu wa sheria kuthibitisha  uponywaji huo. Yesu hakusema tena neno lolote. Alisikiliza sala yao, kilio chao cha huruma na kuwatuma kwa haraka kwa makuhani.

Wale kumi waliamini na walikwenda haraka na wakati wanaelekea huko wakatakasika wote kumi. Makuhani walikuwa na uwezo kweli wa kutambua uponywaji wao na kuwarudisha katika maisha yao ya kawaida. Hapa ndipo linakuja jambo muhimu, Papa Francisko amebainisha. Katika kundi hili ni mmoja tu ambaye kabla ya kwenda kwa makuhani, alirudi nyuma kushukuru Yesu na kusifu Mungu kwa neema aliyoipokea. Na Yesu alitambua kuwa mtu huyo alikuwa ni Msamaria,  kwa maana walikuwa wanajulikana kama wakana Mungu wakiyahudi wa wakati ule. Yesu akasema, “je hawakutakasika wote ili kuweza kurudi nyuma na kutoa shukurani kwa Mungu ila  huyu mgeni? (17,18). Akiendelea na ufafanuanuzi huo Papa amesema, simulizi hii inaweza kusema kuwa  inagawa ulimwengu sehemu mbili: kwanza kwa yule hasiye na shukrani na anayeshukuru; anayejidai kana kwamba kila kitu anapaswa  kuwa nacho na yule ambaye anapokea kila kitu kama zawadi na kama neema! Katika Katekisimu imeandikwa kuwa kila tukio na kila hitaji linaweza kugeuka kuwa shukrani (n.2638.).

Sala ya kushukuru inaanzia daima hapo, kwa kujitambua kuwa tulibarikiwa. Sisi tulifikiriwa kabla ya kuanza kujifunza kufikiri; sisi tulipendwa kabla ya kujifunza kupenda; tumetamaniwa kabla ya ndani ya moyo wetu kuchomoza tamanio. Ikiwa tunazama maisha namna hii, basi  neema inageuka kuwa sababu ya kutuongoza kila siku yetu nzima. Ni kusema asante kwa maana mara nyingi sisi tunasahau kusema asante, amesisitiza Papa. Kwetu sisi wakristo kutoa shurani kumetoa jina la Sakramenti  msingi ambayo ni Ekaristi. Katika neno la kigiriki, kiukweli, maana yake hasa ni hii: shukrani, yaani Ekaristi ni kushukuru. Wakristo wote kama ilivyo kwa waamini wote wanashukuru Mungu kwa zawadi ya maisha. Kuishi awali ya yote ni kupokea. Kuishi awali ya yote ni kwamba tulipokea maisha! Sisi sote tunazaliwa kwa sababu kuna aliyetamani maisha kwa ajili yetu. Na hii ni mojawapo ya safu ndefu za madeni tulizo nazo wakati tunaishi. Madeni ya kuwa na utambuzi wa kutoa shukrani. Katika maisha yetu, zaidi ya mtu aliye tutazama kwa macho safi, na kwa  kutoa bure. Mara nyingi ni walimu, makatekista na watu ambao walijikita kwa kina katika nafasi yao ya kupima maombi ya uwajibu. Na walifanya kuchanua ndani mwetu ile shukrani. Hata urafiki ni zawadi ambayo inastahili kushukuru.

Hii neema ambaye tunapaswa kusema mara nyingi na ndiyo neema ya mkristo ambayo anaishikirikisha kwa wote, inapanuka katika kukutana na Yesu. Injili zinathibitisha kuwa nyayo za Yesu zilikuwa mara nyingi zinaibua furaha na sifa kwa Mungu kwa wale ambao walikuwa wakikutana nao. Simulizi ya Siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana, zimejaa sala za moyo uliopanuka kutokana na kuja kwa Mwokozi. Hata sisi tunaitwa kushiriki furaha hii mara tatu zaidi.  Tukio la kupona kwa wakoma kumi linatoa ushauri na kuonesha wazi. Ni wazi kwamba wote walikuwa na furaha kubwa ya kurudia afya yao na kuweza kutoka nje ya karantini isiyoisha ya kulazimishwa, ambayo ilikuwa inawatenga na jumuiya. Lakini kati yao yupo mmoja ambaye furaha yake iliongezeka furaha, mara dufu kwani zaidi ya ponywaji, alifurahi kukutana na Yesu kweli.

Na si tu aliweza kumwondolea ubaya lakini sasa anao uhakika wa kuwa anapendwa. Hiyo ni sehemu ndogo hasa unaposhukuru na kutoa shukrani, unajielezea uhakika wa kupendwa. Na ndiyo hatua kubwa ya kuwa na uhakika ya kwamba ulipendwa, amesisitiza Papa. Ni kugundua upendo kama nguvu ambayo inashikilia ulimwengu, Mtunzi mmoja wa kiitaliano Dante angesema Upendo “ambao unasukuma jua na hata nyota nyingine” (Paradiso, XXXIII, 145). Sisi siyo tena wasafiri wanaotangatanga kwenda huku na huko, hapana: tuna nyumba, tunakaa ndani ya Kristo, na kutoka katika “makao” haya tunatafakari ulimwengu wote na inaonekana kuwa mzuri zaidi. Sisi ni watoto wa upendo, sisi ni ndugu wa upendo. Sisi ni wanaume na wanawake wa neema.

Papa Fracisko aidha ameomba kutafuta kukaa daima katika furaha ya kukutana na Yesu na kukuza furaha hiyo. Kwa upande mwingine, shetani, baada ya kutudanganya na jaribu lolote  huwa anatuacha tukiwa na huzuni na peke yetu. Ikiwa tuko ndani ya Kristo, hakuna dhambi na hakuna tishio linaloweza kutuzuia kuendelea na safari na furaha, pamoja na wasafiri wenzetu wengi. Zaidi ya yote, tusisahau kushukuru: ikiwa sisi ni wabebaji wa shukrani, ulimwengu pia unakuwa bora, hata ikiwa ni kidogo tu, lakini inatosha kupitisha tumaini kidogo.

Ulimwengu unahitaji tumaini na shukrani, na katika tabia hii ya kutoa shukrani, hatuwezi kusambaza tumaini kidogo.  Kila kitu kimeunganishwa, kila mmoja anaweza kufanya sehemu yake mahali alipo. Njia ya furaha ni ile ambayo Mtakatifu Paulo alielezea mwishoni mwa moja ya barua zake: "Ombeni bila kuchoka, shukrani kwa kila jambo: kiukweli haya ni mapenzi ya Mungu katika Kristo Yesu katika kuelekea ninyi. Msizime  Roho(1 Ts 5,17-19). Papa ameongeza kusema “kutozima Roho ndiyo mpango wa maisha. Tusizime Roho ambayo imo ndani mwetu na kutupelekea kuwa na shukrani”.

30 December 2020, 11:56