Tafuta

Vatican News
2020.12.08 Mtakatifu Yosefu 2020.12.08 Mtakatifu Yosefu 

Papa Francisko:tujifunze kutoka kwa Mtakatifu Yosefu

Katika salam mbalimbali za Papa Francisko mara baada ya tafakari ya katekesi yake Jumatano,Papa amekumbuka kutangazwa kwa Barua ya Kitume ya P'atris corde' ambayo inaelezea maisha ya Mtakatifu Yosefu.Amewashauri waamini kumwomba Mtakatifu Yosefu Msimamizi wa Kanisa katika kipindi hiki kilichotolewa kwa Mwaka wa Mtakatifu Yosefu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya katekesi ya Papa Francisko akiwa katika Maktaba ya Kitume, Jumatano tarehe 9 Desemba 2020, katika salam kwa waamini kwa lugha mbali mbali, Papa amejikita  kuelekeza kiini cha maisha ya Kanisa. Na zaidi amejikita kuzama mwaka wa Mtakatifu Yosefu. Papa amesema  “ Patris Corde" yaaani  "moyo wa Baba” ndiyo kichwa cha Barua ya Kitume ambayo inajikita kufafanua  Mtakatifu Yosefu ambayo inaangazia miaka 150 tangu kutangazwa kuwa Msimamizi wa Kanisa la Ulimwengu. Barua hiyo inatoa ufupisho wa maisha yake na utume wake.  Mungu alimkabidhi tunu zenye thamani kuu Yes una Marian a yeye alijibu kwa imani kuu, ujasiri, upendo na moyo wa ubaba. Tumwombwa ulizi wake juu ya Kanisa katika wakati huu, na tujifunze kutoka kwake kufanya dima kama yeye kwa unyenyekevu na mapenzi ya Mungu.

Malekezo ya kupokea Msamaha wa dhambi katika mwaka wa Mtakatifu Yosefu

Ikumbukwe kwamba Papa Francisko amechapisha Barua yake ya kitume inayomhusu kwa Baba mlinzi wa Yesu, na kwa maana hiyo kusindikiza Mwaka Maalum wa Mtakatifu huyo ambao umeanza tangu tarehe 8 Desemba utafungwa manmo tarehe 8 Desemba 2021. Kutokana na hilo, Hati ya kutoka Idara ya Kitume kuhsu Msamaha wa dhambi iliyoridhiwa na Papa, inatoa maelekezo muhimu ya uwezekano wa kupokea katika kipindi hicho msamaha maalum  kufuatia na Mwaka Maalum wa sura ya Mtakatifu Yosefu, lakini kwa kufuata hali zake zinazotakiwa kama vile kufanya sakramenti ya kitubio, kupokea ekaristi na kusali kwa ajili ya nia za Baba Matakatifu.

Mtakatifu Yosefu amependwa na watu wengi katika historia

Kwa nafasi yake ya historia ya  Kanisa, Papa anakumbusha katika Barua ya Patris corde, kwamba Mtakatifu Yosefu ni baba ambaye daima amependwa na wakristo, kama inavyo jionesha ulimwenguni kote ambapo amewekwa kuwa msimamizi wa makanisa mengi, taasisi mbali mbali za kidini, jumuiya mbali mbali za kidini, vyama vya kitume,  makundi ya kikristo ambayo yanaongozwa na tasaufi  yake na watakatifu wengi ambao wamefanya ibada kuu ya Mtakatifu huyo.

Kwa bahati mbaya wapo watoto wengi ambao ni kama yatima

Mtakatifu Yosefu  kwa  maana hiyo ni mfano wa baba. Kwa bahati mbaya, Papa anasema katika Waraka wa Kitume Patris corde, watoto mara nyingi wanaonekana kuwa yatima wa baba, wa baba wenye uwezo wa kumfundisha mtoto uzoefu wa maisha, bila kumshikilia au kummiliki, badala yake kumfanya awe na uwezo wa kuchagua, wa kuwa uhuru, na ili kuondoka.

Mtakatifu Yosefu alikweka katikati Yesu na Maria katika maisha yake

Alitambua kwa kina kutoweka katikati maisha yake binafsi bali  kwa ajili ya Yesu na Maria. Papa Francisko kwa kusisitiza zaidi  sura ya Mtakatifu huyo amefafanua kwamba "Ulimwengu leo hii unahitaji baba, wa kukataa mabwana na  kwamba, kukataa wale ambao wanataka kutumia miliki ya mwenzake kwa kujaza utupu wao wenyewe; kukataa wale ambao wanachanganya mamlaka na ubabe, huduma na utumishi, mapambano na dhuluma, upendo na ustawi, nguvu na uharibifu. Kiukweli kila wito wa kweli umezaliwa kutoka na zawadi binafsi na hivyo hatuwezi kukubali kuacha ziendelea mantiki za kuwatesa kwa kwa sadaka.

09 December 2020, 16:48