Tafuta

Vatican News
2020.10.14 Mkataba wa Elimu kimataifa 2020.10.14 Mkataba wa Elimu kimataifa 

Papa Francisko:Amani kama vita huzaliwa katika akili ya mwanadamu!

Mkataba wa Elimu Kimataifa na utekelezaji wa lengo la 4.7 utafanya kazi pamoja kwa ustaarabu wa upendo,uzuri na umoja.Papa amesema hayo akihutubia washiriki wa Kongamano na kuonesha maono yake kuwa:"Natumai nyinyi muwe washairi wa uzuri mpya wa kibinadamu,uzuri mpya wa kindugu na wa kirafiki na pia wa kulinda dunia tunayoikanyaga”.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Kongamano la elimu ni tendo la matumaini ambalo limefanyika kuanzia tarehe 16 na 17 Desemba 2020, kwa kushirki viongozi wa harakati za vijana ulimwenguni na wataalam wa sekta hiyo. Mkutano huo unafanyika katika sehemu mbili wengine kupitia mtandaoni  na wengine huko Casina Pio IV, jijini  Vatican ulioandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Sayansi jamii na Umoja wa Mataifa. Siku ya kwanza imejikita katika kuzinduliwa kwa Utume 4.7, yaani utekelezaji wa lengo la 4 la Ajenda ya Umoja wa Mataifa la 2030 la maendeleo endelevu ambalo linataka kuhakikisha elimu bora na inayojumuisha na kukuza fursa za kuendelea kujifunza kwa wote, na hoja yake ya 7 ambayo inakusudia kufanikisha elimu inayolenga maendeleo endelevu na mtindo wa maisha, haki za binadamu, usawa wa kijinsia, kukuza utamaduni wa amani na usio na vurugu, uraia wa ulimwengu na kuthamanisha utofauti za kiutamaduni. Yote haya kwa kushirikiana na Mkataba wa Duniani juu ya Elimu na Mkataba wa Mfumo Mpya wa Elimu Kimataifa uliozinduliwa na Papa Francisko Oktoba iliyopita.

Mkataba wa elimu ulimwenguni umegawanyika

Papa anaonesha uwepo wake kwa njia ya kutuma ujumbe kwa njia ya video ambapo anawapongeza kwa jitihada za serikali nyingi na taasisi katika kambi ya elimu na kuthibitisha kuwa “ni ukweli wa tendo la tumaini katika wakati ujao na mshikamano mbele ya vizazi vipya. Jitihada ambayo ni muhimu zaidi leo hii mahali ambamo mkataba wa elimu ulimwenguni, umegawanyika hata kwa sababu ya janga na kuonesha uwazi zadi wa ulazma wa kuendelea mtindo mpya wa elimu ambao inaruhusu kushinda sintofahamu za utandawazi wa sana na utamaduni wa kubagua. Papa Francisko anaofafanua mwaka 2020 kwa maneno kama haya ya mateso kutokana na janga la Covid-19 na athari zake: “Mwaka wa karantini ya kulazimishwa na kutengwa, kwa uchungu na migogoro ya kiroho na sio vifo vichache na shida ya kielimu isiyokuwa ya kawaida.

 Fursa ya maendeleo kijamii na utambuzi

Zaidi ya watoto bilioni wamekabiliwa na usumbufu katika masomo yao. Mamia ya mamilioni ya watoto wamerudi nyuma katika fursa za maendeleo ya kijami na utambuzi. Na, katika maeneo mengi, migogoro ya kibaolojia, kisaikolojia na kiuchumi imechochewa na mizozo inayohusiana ya kisiasa na kijamii”. Mbele ya makabiliano haya ya hali halisi Papa Francisko amesisitiza, inahitajika kitendo cha matumaini ili msukumo wa chuki, mafarakano na ujinga viweze kushindwa kupitia fursa mpya za elimu kulingana na haki kijamii na kupendana na ndiyo Mkataba mpya wa Elimu”. Na ameendelea kusema: “Ninawashukuru kwa kuungana pamoja leo ili kufanya matumaini na mipango yetu ikue katika elimu mpya ambayo inakuza kupitia kwa mwanadamu, maendeleo fungamani ya binadamu, mazungumzo ya kiutamaduni na kidini, kulinda sayari, mikutano ya amani na ufunguzi ulio wazi kwa Mungu”.

Amani, kama vita, huzaliwa katika akili za wanadamu

Kimsingi, Papa Francisko anasema ni hatua ya Umoja wa Mataifa (UN) kuhusisha serikali na jamii kutoka ulimwenguni kote  katika juhudi za kupata elimu mpya. Na ananukuu maneno ambayo Mtakatifu Paulo VI alikuwa amewambia Umoja wa Mataifa wakati wa ziara yake ya kihistoria mnamo tarehe 4 Oktoba 1965: “Waheshimiwa, mmefanya na mnafanya kazi kubwa: elimu ya ubinadamu kwa ajili ya amani”. Vile vile amekumbusha kuwa Katiba ya Unesco, iliyopitishwa mnamo 1945, mwishoni mwa Vita ya Pili ya Kidunia ilitambua kuwa “kwa maana katika vita huzaliwa katika akili za watu, ni kwa roho ya watu kwamba ulinzi wa amani lazima uwekwe. Hii ilikuwa ni miaka miaka 75 iliyopita, na leo? Papa amethibitisha: Katika wakati wetu, wakati mkataba wa kielimu kimataifa umevunjwa, ninaona kwa kuridhika kwamba serikali zimejitoa tena kutekeleza maoni haya kupitia kupitisha Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, kwa ushirikiano na mkataba wa kimataifa juu ya elimu. Kiini cha Malengo ya Maendeleo Endelevu ni kutambua ukweli kwamba elimu bora kwa wote ni msingi wa lazima wa kulinda nyumba yetu ya pamoja na kukuza udugu wa kibinadamu.

Jitihada ya pamoja kwa ajili ya ustaarabu wa upendo

Mkataba wa Elimu Ulimwenguni wa utekelezaji wa lengo la 4,7 la Ajenda ya Umoja wa Mataifa utafanya kazi pamoja kwa ajili ya ustaarabu wa upendo, uzuri na umoja, hivyo Papa amewageukia washiriki wa Kongamano hilo na kuhitimisha kwa maono ya shauku yake: “Ninatumani nyinyi ni washairi wa uzuri mpya wa kibinadamu, uzuri mpya wa kindugu na wa kirafiki pia wa kulinda dunia tunayo ikanyaga”.

16 December 2020, 16:43