Tafuta

Papa Francisko akumbuka wafidini wa El Salvador baada ya miaka 40 iliyopita

Baada ya miaka 40 ya kifodini,Papa amekumbuka wanawake wamisionari waliouawa kinyama huko El Salvador wakiwa katika huduma ya utume wa kuwasaidia watu waliokuwa wanateseka na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Papa Francisko mara baada ya katekesi yake tarehe 2 Desemba 2020 amekumbuka miaka 40 tangu kifo cha wamisionari wanne huko Kaskazini mwa Amerika, waliouawa kinyama huko El Salvador. Hawa walikuwa ni watawa wa shirika Maryknoll, Sr. Ita Ford na Maura Clarke,  vile vile na wa Shirika la  Mtakatifu Ursula, Sr. Dorothy Kazel na mmmoja wa kujitolea Jean Donovan.

"Hii ilikuwa ni mnamo tarehe 2 Desemba 1980 wakati walitekwa nyara, walibakwa na kuuawa na kundi la wanamgambo. Walikuwa wakitoa huduma huko  El Salvador katika muktadha wa vita vya wenyewe kwa wenyewe", Papa amebainisha.

Akiendelea Papa Francisko amesema "Kwa kujitoa kwa  ajili ya Injili huku wakikabiliwa na hatari kubwa walikuwa wakikimbia kupeleka chakula na dawa kwa watu waliokuwa wanakimbia vita hivyo na hivyo walikuwa wakisaida familia maskini zaidi. Wanawake hawa waliishi imani yao kwa ukarimu mkubwa. Hawa ni mfano kwa wote kuwa wanafunzi waaminifu wa kimisionari", Papa Francisko amefafanua.

02 December 2020, 16:20