Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko: Tafakari juu ya Mtoto Yesu aliyelazwa horini iwasaidie waamini kumhudumia Yesu kwa kuwapenda jirani zao wanaokutana nao kila siku! Baba Mtakatifu Francisko: Tafakari juu ya Mtoto Yesu aliyelazwa horini iwasaidie waamini kumhudumia Yesu kwa kuwapenda jirani zao wanaokutana nao kila siku! 

Papa Francisko: Mtoto Yesu Awe Kiini Cha Upendo na Huduma!

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kusema kwamba, katika kipindi hiki cha Sherehe za Noeli, bado anapenda kuwaalika waamini kuendelea kumtafakari Mtoto Yesu aliyelazwa kwenye Pango la Noeli, ili hatimaye, waweze kujizatiti kumhudumia na kuwapenda jirani zao wanaokutana nao katika hija ya maisha yao ya kila siku. Anawashukuru waamini kwa sala na salam zao za Noeli.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana katika maadhimisho ya Sikukuu ya Mtakatifu Stefano Shemasi na Shuhuda wa huruma na upendo wa Mungu unaoganga na kuponya, unaookoa na kuleta mageuzi makubwa katika historia ya mwanadamu, amewashukuru na kuwapongeza wale wote walioshiriki pamoja naye katika tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana kutoka katika Maktaba ya Kitume mjini Vatican, tarehe 26 Desemba 2020. Hii ni sehemu ya utekelezaji wa protokali ya mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19. Itifaki hii inalenga kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Corona, COVID-19.

Baba Mtakatifu anaendelea kusema kwamba, katika kipindi hiki cha Sherehe za Noeli, bado anapenda kuwaalika waamini kuendelea kumtafakari Mtoto Yesu aliyelazwa kwenye Pango la Noeli, ili hatimaye, waweze kujizatiti kumhudumia na kuwapenda jirani zao wanaokutana nao katika hija ya maisha yao ya kila siku. Anakiri kwamba, katika kipindi hiki cha Noeli amepokea salam na matashi mema ya Noeli na Mwaka Mpya wa 2021 kutoka ndani na nje ya Italia. Si rahisi sana kuweza kumjibu kila mmoja, lakini Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuwashukuru wale wote waliomtumia salam na matashi mema ya Noeli na Mwaka Mpya 2021. Kikubwa zaidi anasema Baba Mtakatifu ni sala, ambazo zimetolewa na waamini kwa ajili ya maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Papa: Shukrani Angelus

 

26 December 2020, 16:07