Tafuta

Vatican News

Papa Francisko:Lazima kuwa na mkakati wa kupunguza hewa chafuzi hadi “net zero”

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video,Jumamosi tarehe 12 Desemba kwa washiriki wa Mkutano wa ngazi ya juu katika fursa ya miaka 5 tangu kuwekwa mkataba wa Paris na sherehe za“Mkutano wa ngazi za Juu” kuhusu mabadiliko ya tabianchi ambapo ni sambamba na miaka mitano ya kutangazwa kwa Waraka wa Laudato si’,kuhusu utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko Jumamosi tarehe 12 Desemba 2020, ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa “Mkutano wa ngazi ya Juu ya mabadiliko ya tabianchi” uliofanyika kwa njia ya mtandao. Katika ujumbe wake amesema, janga la sasa na mabadiliko ya tabianchi vinaleta madhara, si tu katika mazingira lakini hata kimaadili, kijamii, kiuchumi na kisiasa na kuwakumba hasa maisha ya walio maskini zaidi na wadhaifu. Kwa maana hiyo kuna ulazima wa wote kuwajibika katika  kuhamasisha jitihada ya pamoja na mshikamano, katika utumaduni wa kutunza na ambao unaweka kiini cha hadhi ya binadamu na wema wa pamoja.

Ni lazima kuwa na mkakati wa kupunguz hewa chafuzi

Licha ya kuchukua hatua ambazo haziwezi kuwachwa kwa kiasi fulani, ni lazima kuwa na mkakati wa kupunguza kiwango cha hewa chafuzi, ili kufikia kile kiitwacho “net zero”.  Papa Francisko amethibitisha kuwa Vatican inaunga mkono lengo hilo kwa kufuata hatua mbili: kwa upande mmoja  Mji wa Vatican unajitahidi kupunguza hewa chafuzi kwa kiwango cha kufikia Zero ifikapo 2050. Kwa kuongeza juhudi za uendeshaji wa mazingira, ambayo tayari wamekwishaanza miaka kadhaa  nambapo wanafanya kila uwezekano wa matumizi ya busara ya rasilimali kama vile maji na nishati, ufanisi wa nishati, uhamaji endelevu, upandaji miti mpya na mzunguko wa uchumi  pia katika usimamizi wa taka.

Vatican inahamasisha elimu ya Ikolojia fungamani

Kwa upande wa pili , Papa Francisko amebainisha kuwa, Vatican inajitahidi kuhamasisha katika elimu kwa ajili ya ikolojia fungamani. Hatua za sera kisiasa na kifundi lazima ziunganishwa katika mchakato wa elimu ambayo inasaidia mtindo ya kiutamaduni kwa maendeleo na endelevu ambayo msingi wake ni udugu na mapatano kati ya binadamu na mazingira. Katika maono hayo, Papa Francisko amekumbusha alivyozindua Mpango  Mkakati wa Elimu Kimataifa , kwa ajili ya kusindikiza shule na vyuo vikuu katoliki, vinavyoudhuliwa na wanafunzi zaidi milioni 70 katika mabara yote; na amesaidia hata ‘Economy of Francesco’ au Uchumi wa Francisko ambao kwa njia ya vijana wanauchumi, wajasiriamalia, wataalam wa fedha na watu wa ulimwengu wa kazi , katika kukuza na kuhamasisha njia mpya zinazoshinda umaskini wa nishati, ambazo zinaweka utunzaji wa shughuli zote za pamoja katikati ya sera za kitaifa na kimataifa, na ambayo inakuza uzalishaji endelevu hata katika nchi zenye kipato cha chini, ikishiriki katika teknolojia sahihi za hali ya juu.  Papa Francisko kwa kuhitimisha amesema “Umefika wakati sasa wa mabadilisha. Tusiibie kizazi kipya matumaini katika wakati ujao ulio bora”, na amewashukuru.

12 December 2020, 18:29