Tafuta

Vatican News
Papa Francisko: Sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko: Sala ya Malaika wa Bwana  (Vatican Media)

Papa Francisko:Kila binadamu ameumbwa na Mungu kwa ukamilifu wa utakatifu na uzuri!

Mtakatifu Paulo anatufanya tutambue kuwa kila binadamu ameumbwa na Mungu kwa ukamilifu wa utakatifu,katika uzuri ule ule ambao Mama alikuwa amevikwa tangu mwanzo.Uzuri usio haribiwa wa Mama yetu ni wa kuigwa na wakati huo huo unatuvutia.Tumkabidhi yeye na kusema kwa mara nyingi na daima hakuna kutenda dhambi na ndiyo neema ya kuomba.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko katika tafakari yake, kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 8 Desemba 2020, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili amesema kuwa “Injili katika liturujia ya siku  inaadhimisha kwa mshangao wa historia ya wokovu. Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili. Hata yeye alikombolewa na Kristo, lakini kwa maana ya ajabu, kwa sababu Mungu alipenda tangu kutungwa kwa mimba ya mama wa mtoto wake asiguswa kabisa na uharibifu wa dhambi. Kwa maana hiyo katika mchakato wake wa maisha, hapa duniani alikuwa hana madoa ya dhambi na alijazwa neema kama alivyomwita Malaika (Lk 1,28), na kupokea kwa namna ya pekee matendo ya Roho Mtakatifu ili kuweza kujitunza daima  husiano mkamilifu na mwanae Yesu. Na zaidi alikuwa mfuasi wa Yesu, mama na mwanafunzi, japokuwa yeye hakuwa na dhambi.

Tumeumbwa na uzuri ule ule wa mama

Papa Franciskoakiendelea na tafakari hiyo amesema, katika wimbo wa kumtukuza Bwana, katika Barua kwa waefeso1,3-6.11-12, Mtakatifu Paulo anatufanya tutambue kuwa kila binadamu ameumbwa na Mungu kwa ukamilifu wa utakatifu, katika uzuri ule ule ambao Mama alikuwa amevikwa tangu mwanzo. Na ndiyo hatima tunayo alikwa hata sisi katika zawadi ya Mungu ambayo Mtume anasema, “tulichaguliwa kabla ya uumbaji wa ulimwengu ili tuwe watakatifu na wasio na dhambi; alifufanya katika Kristo  kuwa siku moja tuwe huru dhidi ya dhambi”. Hii ni neema ya bure na zawadi ya Mungu, Papa amesisitiza. Na ndiyo ambayo Maria alikuwa nayo tangu mwanzo na ambayo  tutaipata  hata sisi siku ya mwisho  mara baada ya  kutakazwa  dhambi  kwa neema ya Mungu. Na ile inayotufungulia mlango wa mbingu ni neema ya Mungu inayopokelewa kwa imani.  Hata wale wasio kuwa na hatia zaidi na ambao walikuwa na dhambi ya asili, walipambana kwa nguvu zote dhidi ya madhara yake. Papa Franciskoa amesema, hao wamepitia kwa njia ya mlango mwembamba ambao unafikisha katika uzima (Lk 13,24).

Neema ya Mungu inatolewa kwa wote katika Dunia hii

Kwa kuongezea Papa Francisko ameuliza swali kama wanajua aliye kuwa wa kwanza kuingia katika mlango wa mbingu na Yesu, yaani kati ya wale majambazi wawili waliovsulibishwa na Yesu. Wa kwanza alisema “nikumbuke mimi katika ufalme wako. Na Yesu akamjibu leo hii utakuwa nami mbinguni” (Lk 23,42-43).  Kwaa maana hiyo Papa amesema, neema ya Mungu inatolewa kwa wote na wengi katika dunia hii, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza. (Mk 10,31). Lakini lazima kuwa makini, Papa ameonya kwani sio wengine kufanya ujanja wa kukawia ukisubiri, badala yake ni lazima kuchukua uwajibikaji katika maisha na kutumia wakati wa uvumilivu wa Bwana. “Yeye ni mvumilivu, anatusubiri kwa ajili ya kutupatia neema yake daima. Sisi tunaweza kudanganya watu  na siyo Mungu, kwani yeye anajuia vema mioyo yetu binafsi. Tutumie fursa hii kwa maana ya kikristo katika siku hii. Sio kufurahia maisha ya wakati unapumbazwa na mambo ya kidunia, badala yake ni kukaribisha ya leo hii na kukataa mabaya, huku ukiitikia ndiyo kwa Mungu, na kujifungulia neema yake; kuachana kabisa na kujifungia binafsi kwa  kuvutwa na ubinafsi. Lazima kutazama hali halisi inayozunguka  na jinsi ulivyo na kutambua kuwa tumependwa na Mungu, lakini hatukumpenda jirani kama tunavyopaswa.

Kuanza safari ya uongofu na kuomba msamaha

Kuungama kwa namna hiyo ni kuanza upya safari ya uongofu na kuomba awali ya yote msamaha wa Mungu katika Sakramenti ya kitubio na baadaye kufanya malipizi ya mabaya yaliyotendeka dhidi ya wengine. Yote hayo Lakini  daima ni katika kujufunulia neema. Bwana anabisha katika milango yetu, anabisha katika mioyo yetu ili aingie ndani mwetu kwa urafiki na muungano na ili tupate wokovu. Hiyo ndiyo njia, kwa ajili yetu ya kugeuka kuwa watakatifu wasio na dhambi. Uzuri usio haribiwa wa Mama yetu ni wa kuigwa na wakati huo huo unatuvutia. Tumkabidhi yeye na kusema kwa mara nyingi na daima hakuna kutenda dhambi na ndiyo neema, Papa Francisko amehitimisha.

PAPA NA SIKU KUU YA MKINGIWA
08 December 2020, 13:56