Tafuta

Papa Francisko katika maadhimisho ya kesha la Noeli na Ujumbe wake wa "Urbi et Orbi" utatangazwa pia kwa kutumia lugha ya alama kwa ajili ya walemavu. Papa Francisko katika maadhimisho ya kesha la Noeli na Ujumbe wake wa "Urbi et Orbi" utatangazwa pia kwa kutumia lugha ya alama kwa ajili ya walemavu. 

Papa Francisko: Kesha la Noeli na "Urbi et Orbi": Lugha ya Alama

Kutokana na msisitizo uliotolewa na Baba Mtakatifu Francisko, vyombo vya mawasiliano ya jamii vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Vatican, kwa kushirikiana na Kituo cha Televisheni cha Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, TV2000 pamoja na Sr. Veronica Donatello kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI, watarusha matangazo maalum ya alama kwa walemavu wakati wa Noeli 2020.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Kesha la Noeli kwa Mwaka 2020 hapo tarehe 24 Desemba pamoja na maadhimisho ya Sherehe ya Noeli tarehe 25 Desemba 2020, kuanzia saa 6:00 za Mchana kwa Saa za Ulaya, atatoa salam kwa ajili ya mji wa Roma na Ulimwengu katika ujumla wake, maarufu kama “Urbi et Orbi”. Hili ni tukio ambalo linawawezesha watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia kuunganika na Baba Mtakatifu kwa njia ya vyombo mbali mbali vya mawasiliano pamoja na mitandao ya kijamii ili kusikia kwa muhtasari ujumbe wa amani, upendo na matumaini kwa kugusa baadhi ya matukio makubwa yaliyoitikisa dunia katika maeneo haya na mwelekeo mpya unosheheni mwanga wa matumaini.

Kutokana na msisitizo uliotolewa na Baba Mtakatifu mwenyewe kuhusu maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ya mawasiliano ya jamii, kuhakikisha kwamba, matangazo ya imani na mafundisho ya Kanisa yanawafikia watu wengi zaidi na hasa wale wenye ulemavu, katika kipindi hiki cha janga kubwa la homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19. Ni katika muktadha huu, vyombo vya mawasiliano ya jamii vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Vatican, kwa kushirikiana na Kituo cha Televisheni cha Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, TV2000 pamoja na Sr. Veronica Donatello kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI, watarusha matangazo maalum ya alama kwa walemavu. Watu hawa wanaweza kujiunga na anuani ifuatayo ili kuweza kupata matangazo haya mubashara https://e.va/lis

Walemavu

 

23 December 2020, 15:01