Tafuta

Papa Francisko:haki ya kijamii ni kuwapa maskini,mali binafsi

Papa Francisko ametuma video mbili za salam na hotuba,katika fursa ya mkutano wa kwanza kwa njia ya mtandano wa mahakimu ambao ni wajumbe wa Kamati kwa ajili ya haki kijamii barani Afrika na Marekani wakiongozwa na mada “Ujenzi wa haki kijamii.Kuelekea utekelezwaji kamili wa haki msingi za watu katika mazingira magumu.Anawakumbusha mahakimu kuwa sentensi zao zinaweza kutengeneza mashairi,kuponya majeraha ya maskini,kuunganisha sayari na kulinda dunia.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Papa Francisko ametuma  video mbili za  salam na hotuba, katika fursa ya mkutano wa kwanza kwa njia ya mtandano wa mahakimu ambao ni wajumbe wa Kamati kwa ajili ya haki kijamii barani Afrika na Marekani ambao wanaoongozwa na mada “Ujenzi wa haki  kijamii. Kuelekea utekelezwaji kamili wa haki msingi za watu katika mazingira magumu”. Katika ujumbe huo  Papa Francisko anafurahi kuwatumia maneno hayo kabla ya kuanza kazi yao na hata baadaye fursa ya kutafakari nao na  ambayo wamependekeza. Anawapongeza kwa kuanzisha na kufikiria, kutafakari na kujenga haki kijamii. Ni jinsi gani ilivyo vizuri wao kuweza  kufanya mapumziko katika kazi yao ya kwaida ili kufikiria na kujifikiria. Ni uhakika wa Papa kuwa mazoezi haya yatawasaida kupata ukuu zaidi wa kutimiza utume wao na uwajibikaji wao kijamii.

Mbele ya kukabiliwa na jamii ambayo leo inaonekana na kutokuaminiana na kutowaamini wale ambao wana uwezo wa kuamua ni nini, tukio hilo linaweza kuwa mafuta ya  heri ya kukarabati. Hata hivyo Papa amewakumbusha alivyowaambia wakati uliopita walipokuwa wanafanya mkutano wao Casina Pio IV Roma , kama harakati za kijamii, wao  pia walikuwa washairi. Na hivyo amependa kurudia wazo hilo. Mshairi anahitaji kutafakari, kufikiria, kuelewa muziki wa hali halisi na kuutengeneza kwa maneno. Ninyi, katika kila uamuzi, katika kila sentensi, mnakabiliwa na uwezekano mzuri wa kutengeneza mashairi: shairi ambalo huponya vidonda vya maskini, ambalo linaunganisha sayari, ambayo yanalinda dunia mama  na uzao wake wote. Shairi linalokarabati, likomboa, na kulisha.

Papa amewaomba mahakimu wasiache uwezekano huo. Wachukue neema hiyo ambayo ndiyo waliyo nayo na maamuzi na ujasiri. Wawe na utambuzi kuwa kila kitu ambacho wanaweza kuchukua katika unyoofu wa kazi yao na jitihada zao ni muhimu sana. Papa Francisko amewaomba wakumbuke daima kwamba ikiwa haki ni halisi ya dhati, haki hiyo hufanya nchi zifurahi na wenyeji wao wanastahili. Hakuna hukumu inayoweza kuwa ya haki, hakuna sheria halali ikiwa kile wanachotoa hakuna usawa zaidi, ikiwa kile wanachotoa ni kupoteza haki zaidi, kutostahili au vurugu. "Kaka na dada fanyeni mazoezi ya ushairi wenu na mtakuwa washairi bora na mahakimu bora. Na msisahau kamwe kwamba shairi ambalo halibadilishi ni maneno machache tu yaliyokufa. Mkutano wao huwe  na mafanikio.

Aidha katika tafakari yake ya mkutano huo, Papa Francisko sisitiza juu ya misingi mitano ya haki kijamii. Kwa wanawake na wanaume wanaofanya kazi katika mabara mawili kwa ajili ya kutoa haki na kufikiria jinsi ya kujenga haki mpya ya kijamii Papa Francisko anaorodhesha misingi mitano ya haki hii ya kijamii katika hotuba yake iliyofungua mkutano wao. Mawazo yenu kwanza kabisa, hayapaswi kupoteza ukweli ... picha inayofadhaisha ambayo sehemu ndogo ya ubinadamu inaishia kwa utajiri, wakati hadhi zaidi na zaidi hazijulikani na haki zao za binadamu ni kupuuzwa na kukiukwa. Hatuwezi kufikiria kutengwa na ukweli”

Msifanye nadharia bali mazoezi mapya ya kimahakama

Msingi wa pili wa haki mpya ya kijamii ni kutambua kuwa hii ni kazi ya pamoja, ambayo watu wote na wote wenye nia njema ushughulikia changamoto na kukubali kuwa, kama wema na upendo, haki pia ni jukumu ambalo lazima lishinde kila siku, kwa sababu usawa ni jaribu la kila wakati. Kwa hili, na ni msingi wa tatu, katika mtazamo wa kujitoa na ambao ni muhimu, kufuata njia ya Msamaria Mwema, kwa sababu jaribu la kutopendezwa na wengine, hasa wadhaifu zaidi, unaonekana mara kwa mara. Lazima tukubali kwamba tumeshazoea kupita kando, tukipuuza hali hadi zitakapotugusa moja kwa moja. Kujitoa bila masharti ni kuchukua maumivu ya mwingine, na sio kuingilia kwenye utamaduni wa kutokujali.

Kiu ya utu: Tafakari ya nne na ya lazima kwa wale ambao wanataka kufikia haki mpya kijamii kwa sayari yetu, wana kiu ya utu, ndiyo inakuwa mada kuu. Papa Francisko ameelezea kuwa  Huko  ​​kuna mapambano, ushindi na kushindwa.Hapo kuna damu ya wale ambao walitoa maisha yao kwa ajili ya ubinadamu fungamani.  Hizi ndiyo mizizi ya uzoefu, hata ile ya haki kijamii ambayo leo hii tunataka kufikiria tena, kuikuza na kuimarisha, Papa amesisitiza.

Sisi ni watu na watu, sio wasomi wa Mungu: Msingi wa tano, Papa anaendelea, ni watu. Hatuwezi kujidai kuwa wasomi walio na nuru, lakini watu, ili kuonyesha kwamba sisi ni wa kudumu na wasiochoka katika kazi ya kujumuisha, kufungamanisha na kuwainua  wale ambao wameanguka. Kwa sababu wale ambao hufuata njia ya wasomi wa Mungu, wanaishia katika uandishi maarufu wa wasomi ambao hufanya kazi kwa watu, lakini hawafanyi chochote na watu, na hawahisi kuwa wao ni watu.

Mshikamano: kupambana dhidi ya utamaduni wa kutumia wengine: Papa Francisko amewaomba wale ambao wanataka kufikiria tena wazo la haki ya kijamii, kuonyesha mshikamano na usawa. Mshikamano, kupambana dhidi ya sababu za kimuundo za umaskini, ukosefu wa usawa, ukosefu wa kazi, ardhi na makazi. Kwa kurudia kusema T tatu katika lugha ya kispanyola ‘techo, tierra y trabajo’ tatu za T, maana yake Ardhi, paa la nyumba na kazi. Kwa kupambana, kwa kifupi, dhidi ya wale wanaonyima haki za kijamii na za kazi. Kwa kupambana na utamaduni huo unaosababisha kuwatumia wengine, kuwatumikisha wengine na kuishia kuchukua heshima ya wengine.

Haki: kuwalipa maskini kilicho chao: Na wenye haki, tukijua kwamba wakati, kwa kutumia sheria, tunawapa maskini vitu ambavyo ni muhimu, hatuwapi vitu vyetu, wala vya watu wengine, lakini tunawarudishia kilicho chao. Wazo ambalo tumepoteza mara nyingi Papa amesisitiza. Tunaunda haki mpya kijamii kwa kukubali kwamba tamaduni ya Kikristo haijawahi kutambua haki ya mali binafsi kama isiyoweza kuguswa na haki imekuwa ikisisitiza kazi ya kijamii na mtindo wake. Haki ya mali ni haki ya asili ya pili inayotokana na haki ambayo kila mtu anayo, alizaliwa kutokana na hatima ya uliwengu wa mali zilizoundwa.

Msifanye nadharia, bali mazoezi mapya ya kimahakama: Hakuna haki ya kijamii inayoweza kutegemea uovu, inayowakilishwa na mkusanyiko wa utajiri. Matumaini ya mwisho  ya Papa FRancisko ni kwamba kila kitu ambacho kitajengwa katika siku hizi mbili juu ya haki mpya kijamii ni zaidi ya nadharia tu, na kwa maana hiyo ni mazoezi mapya na ya haraka ya kimahakama, ambayo inachangia kuhakikisha kuwa ubinadamu unaweza, katika siku zijazo za karibu sana, kufungamanisha  katika utimilifu na  katika amani.

01 December 2020, 17:38