Tafuta

Papa na Rais wa Iraq Papa na Rais wa Iraq 

Papa Francisko ataanza ziara zake kwenda Iraq kuanzia tarehe 5-8 Machi 2021

Ni tangazo kwa mara nyingine tena ya hija ya kitume.La kwanza lilikuwa limetolewa mwishoni 2019.Ni kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican kwamba Papa atatembelea jiji la Baghdad,na uwanda wa Ur,Erbil,Mosul na Qaraqosh.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Ni siku nne ya ziara ya Papa Francisko atakayo tembelea nchini Iraq. Mara baada ya miezi kumi na mmoja tangu kuahirishwa kwa ziara za kimataifa kwa sababu ya janga, sasa Papa anaanza kwa upya ziara. Kwa kupokea mwaliko wa Jamhuri ya nchi ya Iraq na Kanisa Katoliki mahalia, Papa Francisko atatimiza Ziara yake ya kitume katika nchi hiyo kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi 2021, kwa kutembelea mji wa Bagdad, uwanda wa Ur, ambao unahusiana na kumbu kumbu ya Ibrahim, mji wa Erbil, kama ilivyo mji wa Mosul na Qaraqosh katika uwanda wa Ninawi.

Hata hivyo baadaye itatangazwa, ratiba kamili ya ziara hiyo ambayo itazingatia dharura ya kiafya ulimwenguni. Kwa hakika safari hii ni ishara ya dhati ya ukaribu wa watu wote, ambao wameteseka kwa vita nchini humo. Papa Francisko alikuwa amelezea nia ya kutembea nchini Iraq kunako tarehe 10 Juni  2019, wakati wa Mkutano wake na Washiriki wa Mkutano wa Shughuli za Msaada wa Makanisa hitaji  katika Makanisa ya Mashariki (Roaco). Katika maneno yake alikuwa amesema “wazo langu mara nyingi linalonijia ni kufikiria Iraq kuitembelea kunako 2020, kwa sababu waweze kuwa na matarajio ya amani na ushirikishano wa kushiriki kujenga wema wa pamoja kwa watu wote wakiwemo hata dini  katika  jamii nzima na ili  wasiangukie katika mivutano inayotokana na migogoro ya nguvu za kikanda”.

Nchini Iraq kabla ya mwaka 2003 mwaka ambao unakumbusha migogoro iliyofikia kuanguka kwa rais Saddam Hussein, wakristo walikuwa karibu milioni moja na laki nne. Hofu ya vita na kukaliwa uwanda wa Ninawi na serikali iliyojiita la Kiislamu, kati ya 2014 na 2017, iliwapunguza hadi kufikia karibu wakaristo laki tatu na nne hivi. Rais Salih amesisitiza mara kadhaa thamani ya Wakristo na jukumu lao katika ujenzi, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu, Mustafa Al-Kazemi, ambaye aliwaalika Wakristo, waliokimbia Iraq kwa sababu ya vurugu, kurudi kuchangia ujenzi wa nchi hiyo. Pamoja na hayo hayo bado inabaki uwanja wazi kwa ajili ya amani, usalama na utulivu

Mgogoro wa kiuchumi, ukosefu wa ajira, ufisadi na mchezo usioisha kama wa kuigiza wa wakimbizi wa ndani takriban milioni 1.7, unaweka majaribu magumu ya mipango ya maendeleo. Unicef ​​inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 4 wanahitaji msaada wa kibinadamu, nusu yao ni watoto. Katika muktadha huu ambapo hospitali na dawa zinakosekana, janga la Covid-19 limeua maelfu ya watu.

Walio mstari wa mbele katika hayo ni Kanisa mahalia ambalo sasa linamsubiri mfuasi wa Mtakatifu Petro ambaye ataweza kutimiza mpango uliokuwa ufanyike kunako mwaka 2000 na Mtakatifu Yohane Paulo II.  “Papa Francisko ni mwanaume aliye wazi, mtafutaji wa amani na udugu. Iraq nzima, wakristo wote na waislam,  tupo karibu naye kwa ajili ya tabia yake rahisi na ukaribu wake”. Alikuwa amesema hayo Kardinali Louis Raphael Sako, Patriaki wa  Babilonia ya Wakaldayo katika Gazeti la Kanisa Katoliki Ia Italia SIR. Akiendelea  alisema “ Maneno yake kwa hakika yanagusa moyo wote kwa sababu ni maneno ya mchungaji. Ni mwanaume ambaye anaweza kuleta amani. Milioni ya waislam walifuatilia ziara ya Papa Francisko akiwa huko Abu Dhabi. Na hao hao watafutilia hata akiwa Iraq”. Alisema Patriaki huyo.

Uwanda wa Ur wa Wakaldayo nchini Iraq ulikuwa uwe ndiyo hatua ya kwanza ya hija ya Kitume  ya Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 2000. Ziara yake ilikuwa imepangwa kuanzia tarehe Mosi hadi 3 Desemba 1999. Lakini haikiwezekana kutokana na kwamba Saddam Hussein, baada ya mazungumzo kudumu miezi michache, alikuwa ameamua kuiahirisha. Miaka ishirini baadaye ndoto hiyo ya Mtakatifu Yohane Paulo II inatimia kwa mrithi wake wa pili.

07 December 2020, 12:00