Tafuta

Vatican News

Papa anatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa ili wakimbizi wa Iraq na Siria warudi kwa usalama

Kila jitihada iwe ndogo au kubwa inayofanywa kwa ajili ya mchakato wa amani ni kama kuongeza tofari juu ya mengine katika ujenzi wa mshikamano wa haki na ambao unafungua ukarimu,na mahali ambamo wote wanaweza kupata mahali pa kuishi kwa amani.Ni katika ujumbe wa Papa kwa njia ya video aliotuma kwa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu katika Mkutao kuhusu mgogoro wa kibinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya binadamu katika fursa ya Mkutano kuhusu mgogoro wa kibinadamu wa Siria na Iraq ambao umefanyika kwa njia ya mtandao, Alhamisi tarehe 10 Desmba 2020. Katika ujumbe wake Papa nayo furaha ya kuwatumia salam za dhati wakati wa mkutano huo ulioandaliwa na Baraza hilo kwa ushirikiana na mabaraza mengine ya Vatican, ili kujadili juu ya matatizo makubwa ambayo bado leo hii yanasumbua watu wapendwa wa Siria, Iraqna Nchi zinazopakana nazo.  Kila jitihada iwe ndogo au kubwa inayofanywa kwa ajili ya mchakato wa amani ni kama kuongeza tofari juu ya  mengine  katika ujenzi wa mshikamano wa haki na ambao unafungua ukarimu, na mahali ambamo wote wanaweza kupata mahali pa kuishi kwa amani. Wazo la Papa limewaendea hasa watu ambao wamelazimika kuacha nyumba zao na kukimbia mabaya ya vita, katika kutafuta hali ya maisha  bora kwa ajili yao na kwa ajili ya wapendwa wao.

Wakristo waliolazima kukacha nyumba na makazi walipozaliwa

Kwa namna ya pekee Papa anawakumbuka wakristo waliolazimika kuacha maeneo yao ambayo walizaliwa na kukulia, mahali ambamo walikuza na kutajirishwa na imani yao. Lazima kufanya lolotae kwa namna ya kwamba uwepo wa Wakikristo katika ardhi hizo unaendelea kuwapo kama ilivyokuwa daima tangu mwanzo yaani kuwa ishara ya amani, ya maendeleo na mapatano kati ya mtu na watu.  Wazo la pili, la Papa  Francisko limewaendel wakimbizi ambao wanataka kurudi katika nyumbani kwao. Papa Francisko amerudia kutoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, ili iweze kufanya kila jitihada kwa ajili ya kuwezesha watu hawa kurudi, kwa kuwahakikisha hali ya usalama na hali ya uchumi wa lazima ili jambo hili liweze kweli kutokea. Kila ishara, kila jitihada katika mwelekeo huo ni lenye thamani kubwa, Papa amehimiza.

Shughuli za Mashirikia katoliki katika kutoa msaada wa kibinadamu

Tafakari ya mwisho ambayo Papa Francisko ameitoa kuhusu kazi ya mashirika katoliki ambayo yamejitikita katika kutoa msaada wa kibinadamu. Papa anawatia moyo wa kuendelea na kuwajibika kwa ajili ya kukarimu kwa mfano wa Msamaria Mwema, kwa maana hao anasema wamekita bila kubakiza a katika kukaribisha, kutunza, kusindikiza wahamiaji na waliorundikina ndani katika nchi hizo, bila ubaguzi wa imani yao waliyo nayo. Kama alivyopata fursa nyingi kusema na amerudai  kwamba Kanisa siyo Shirika la ONGs. “Matendo yetu ya upendo lazima yawe mfano  na kufuata Injili. Misaada hiyo lazima iwe ishara muhimu ya upendo wa Kanisa mahalia ambao wanasaidia Kanisa jingine ambalo linateseka, kwa njia ya vyombo hivyo vya kushangaza ambavyo ni mashirika Katoliki ya msaada wa kibinadamu na maendeleo. Ni Kanisa moja ambalo linasaidia Kanisa jingine! Papa amesisitiza. Kwa kuhitimisha, Papa Francisko amependa kuwajulisha kuwa wanapokuwa wanatoa huduma katika maeneo hayo, wao  siyo peke yao. Kwa sababu Kanisa zima ni moja kwa ajili ya kwenda kukutana na mtu aliyejeruhiwa na majambazi, kando kando ya njia kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Katika kazi yao, Baraka yake inawasindikiza na ambayo kwa siku hii amewabariki ili katika mkutano huo uweze kuzaa matunda mengi na matarajio, maendeleo na amani kwa maisha mapya katika nchi hizo.

10 December 2020, 16:00