Tafuta

Nia za Papa kwa mwezi Desemba:Uhusiano wetu na Yesu umwilishwe kwa sala

Katika ujumbe kwa njia ya Vedeo wa Niaza maombí kwa mwezi Desemba 2020,Papa anashauri kutafakari kwa kina kuhusu uhusiano wetu binafsi na Yesu Kristo na ili upatekwe kumwilishwa kwa Neno la Mungu na maisha ya sala.

Sala inaweza kubadilisha hali halisi na mioyo, kubadili maisha yetu na pia ni mchakato wa njia kwa ajili ya kumkaribia Baba. Sala ndiyo kiini cha Nia za Papa Francisko kwa mwezi Desemba 2020 ambayo utangazwa na mtandao wa kimataifa wa maombi. Papa Francisko katika nia hizo amethibitisha kwamba sala ni moyo wa utume wa Kanisa, ufunguo kwa ajili ya kuingia katika mazungumzo na Baba. Kila mara tunaposoma sehemu ndogo ya Injili tunasikiliza Yesu ambaye anaongea nasi.

Tunazungumza na Yesu. Tunamsikiliza na kumjibu. Hiyo ndiyo sala. Kwa kusali, Papa amesisitiza tunabadilisha hali halisi. Tunabadili hata mioyo Yetu. Ndiyo Mioyo yetu inabadilika tunaposali. Tunaweza kufanya mambo mengi, lakini bila sala haiwezekani kufanya lolote. Tusali ili maisha yetu ya husiano binafsi na Yesu Kristo yaweze kumwilishwa na Neno la Mungu na kuwa na maisha ya sala. Video ya Papa Francisko kwa mwezi huu  Desemba inahitimishwa na mwaliko maalum ambao alikuwa ameutoa tarehe 28 Juni 2019 wakati wa Mkutano na Mtandao wa sala ulimwenguni. Kwa maana hiyo Papa alikuwa amewaalika kuwa: “Kwa ukimya, wote, kila mmoja asali kwa moyo”.

01 December 2020, 18:14