Tafuta

Papa ameombea nchi ya Nigeria kwa Mungu ili ageuze mioyo ya magaidi!

Maombi ya Papa na wito kwa ajili ya kuongoka wale wanaofanya mambo mabaya kama vile mauaji yaliyotendeka Jumamosi iliyopita nchini Nigeria.Papa ametoa wito mpya na ushauri kwa nchi hiyo ambayo umegubikwa na vurugu kutoka na makundi ya msimamo mkali wa kiislam.

Papa Francisko mara baada ya katekesi yake, Jumatano tarehe 2 Desemba 2020 akiwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume mjini Vatican, mawazo yake  ya sala zake ni kwa ajili ya  Nigeria, mahali ambapo kwa bahati  amesema mbaya bado umwagaji damu unaendelea kutokana na gaidi.

“Jumamosi iliyopita huko Kaskazini Mashariki mwa nchi wameuawa kwa ukatili mkubwa zaidi wakazi miaka moja wakiwa wanafanya kazi. Mungu awapokee katika amani yake na kuwapa nguvu familia zao; na wakati huo huo atoe uongofu kwa wale ambao wanatekeleza makosa ya namna hiyo na kulikosea heshima jina lake. 

02 December 2020, 16:55