Tafuta

Vatican News

Kwa kufunga mwaka wa Maria nchini Argentina Papa ashauri kumuiga Maria

Ni mama wa Yesu na ambaye alimleta Yesu ulimwenguni.Ni mwanafunzi.Ni wa kwanza kumfuata Yesu afanye kila ambacho Yesu anasema na kutii.Ni ujumbe kwa njia ya video wa Papa Francisko kwa waamini nchini Argentina katika kufunga"Mwaka wa Maria” kitaifa akionesha ukaribu wake na kuwaalika wamfuate mwanafunzi wa kwanza wa Yesu ambaye ni Maria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe wa Papa Francisko aliotuma kwa njia ya video katika fursa ya kufungwa kwa "mwaka wa Maria" kitaifa nchini Argentina, Papa Francisko anasema: “Mwaka wa Maria kitaifa unafungwa leo. Mwaka ambao kutokana na vizuizi vya kipindi cha janga, imebidi tufuatilia shughuli nyingi katika kumbu kumbu na heshima ya Bikira Maria. Ninaungana na waamini wote leo hii ambao wanasheherekea hitimisho la Mwaaka huu wa Maria Kitaifa. Ninasali kwa ajili yenu na ninawaomba msali kwa ajili yangu. Msisahau kuwa Maria ni Mama na mfuasi. Ni mama wa Yesu na ambaye alimleta Yesu ulimwenguni. Ni mwanafunzi. Ni wa kwanza kumfuata Yesu afanye kila ambacho Yesu anasema na kutii. Sura hii ya Maria, Mama na mwanafunzi, itusindikize katika maisha yetu ya kila siku! Ninawaomba msali kwa ajili yangu. Na mimi ninafanya hivyo kwa ajili yenu. Na Mungu anawabariki. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu amina" amehitimisha Papa Francisko ujumbe wake.

Kufungwa kwa Mwaka wa Maria wa Lujan

Ujumbe huo umetangazwa wakati wa Misa katika Kanisa Kuu la La Plata wakiwa wameweka picha ya Bikira Maria wa Luján wakiwa wanafunga Mwaka huo maalum. Ulitangazwa na Baraza la Maaskofu nchini Argentina  kwa ajili ya kufanya kumbu kumbu ya miaka 400 tangu kufika kwa picha iitwayo “Virgen del Valle” yaani “Bikira wa Bondeni” katika Wilaya ya Catamarca. Mwaka wa Maria ulitangazwa rasmi katika Siku kuu ya Mama yetu wa Medali ya Miujiza , mnamo tarehe  27 Novemba 2019, na kuzinduliwa rasmi baadaye tarehe 8 Desemba, katika Siku kuu ya Bikira Maria Mkingia dhambi ya asili, kwa maana hiyo ilikuwa ni siku chachache kabla ya kuanza kuenea kwa  janga la  Covid-19. Mwaka  guo ulikuwa umezindukiwa kwa misa Takatifu wakiwa wanaomba umoja na amani. Ni maadhimisho yaliyoongozwa katika Kanisa kuu la Madhabahu ya Mama yetu wa Luján, na Askofu  Oscar Ojea, wa Jimbo la Mtakatifi San Isidro na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Argentina. Kati ya washiriki alikuwapo Rais mstaafu Mauricio Macri, na rais Mteule Alberto Fernández.

Maskofu katika mwaka wa Maria

Katika kuanza kwa Maka huo, maaskofu nchini Argentina walikuwa wameandika ujumbe wao wakiwaalika waamni wote nchini humo  kuishi kwa kina mwaka huo kama zawadi ya Mungu na ambayo ilikuwa inakumbusha hata kushehere kufika kwa Piacha ya Bikira maeia wa Bonde  Wilayani Catamarca, inayofanyiwa ibada ya kina katika nchi hiyo na kukumbuka  haya Misa ya kwanza iliyoadhimishwa kwa mara ya kwanza miaka 500 iliyopita nchini Argentina. Kwa mujibu wa maaskofu, walisema ni matukio ambayo katika muktadha wa kijamii na kiutamaduni, bado unaendelea kuwaomba jitihada kuwa wa kweli kwa kujiuliza wano ni nani na kama kama wakatoliki katika nchi pendwa ya Argentina, ambayo inateseka lakini yenye kujazwa na matumaini wamesisitiza.

09 December 2020, 17:00