Tafuta

Vatican News
2020.12.08 Mama Yesu wa Guadalupe 2020.12.08 Mama Yesu wa Guadalupe 

Papa aongeza muda wa msamaha katika maadhimisho ya Mama Yetu wa Guadalupe!

Hati ya kuongeza msamaha wa dhambi na kwa ajili ya wote katika fursa ya miaka 125 tangu kuwekwa kwa taji la Mama yetu wa Guadalupe.Tarehe 12 Desemba katika Kumbu kumbu ya Mama Yesu Papa anatarajia kuadhimisha misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Idara ya Kitume kwa ajili ya toba, baada ya kupokea maombi tarehe 3 Desemba kutoka kwa Kardinali Carlos Aguiar Retes, Askofu Mkuu wa Mji wa Mexico na mkuu wa Kanisa Kuu la Mexico, na kwa kuidhinishwa na  Papa, wameongezewa muda wa msamaha na faida zote za kiroho ambazo tayari zilitolewa katika Hati ya tarehe 14 Mei 2019 na agizo la tarehe 14 Agosti 2019  kwa waamini wote ulimwenguni.

Katika fursa ya kuadhimisha miaka 125 tangu kuwekwa taji la Mama Yetu wa Guadalupe, na kwa sababu ya janga la sasa la COVID-19, waamini hawatalazimika kwenda katika hija kwenye Kanisa la Madhabahu ya kitaifa la Mama Yetu wa Guadalupe. Na kwa njia hiyo wataweza kuchukua fursa ya kitendo hiki cha uchaji, kwa  kubaki katika makazi yao, huku  wakiheshimu  Picha Takatifu ya Mama Yetu wa Guadalupe na juu ya yote, kufuatilia hata sherehe  ya maadhimisho ya Misa Takatifu kupitia  vyombo vya habari (redio, runinga, utiririshaji wa moja kwa moja kama vile YouTube  na utangazaji).

Hata hivyo Idara ya kitume ilikuwa tayari imeshaongeza muda hadi tarhe 12 Oktoba 2021 katika mwaka wa  Jubilei ya Guadalupe ambayo ilitangazwa katika fursa ya kuadhimisha miaka 125 tangu kivikwa kwa taji Bikira Mama Yetu wa Guadalupe tukio lililofanyika mnamo tarehe 12 Desemba 1895.

Kwa dhati  ilianza tarehe 8 Desemba 2020 na ambayo ilikuwa ifungwe tarehe 12 Oktoba mwaka huu, lakini kwa sababu ya miezi hii yote ya janga na ambalo limesababisha upungufu mkubwa wa waamini kwenda hija katika ya Mama Maria ambayo inatembelewa na wanahija kutoka ulimwengu mzima.

Jumamosi tarehe 12 Desemba 2020  katika Kumbu kumbu ya Mama wa Guadalupe, Papa Francisko anatarajia kuadhimisha misa saa  5:00 asubuhi majira ya Ulaya katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

09 December 2020, 18:50