Tafuta

Vatican News
Watawa katika huduma ya Kanisa na ulimwengu Watawa katika huduma ya Kanisa na ulimwengu 

Idhini ya Vatican inahitajika katika kuanzisha taasisi mpya za kidini katika Makanisa ya Mashariki

Katika Barua ya Kitume iliyotolewa kwa njia ya 'motu proprio',Baba Mtakatifu Francisko anarekebisha sheria ya kanuni ya Makanisa ya Mashariki kuhitaji idhini yaVatican ili kuwa na utambuzi halali wa taasisi mpya na jamuyia za kitume katika majimbo.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican.

Imetangazwa tarehe 7 Desemba 2020  Barua yake binafsi  ya kitume ya Motu proprio ya  Baba Mtakatifu Francisko kuhusu marekebisho ya Kanuni ya Sheria ya Makanisa ya Nchi za Mashariki, kifunga  435 §1 na  506 §1 (Codicis Canonum Ecclesiarum Orientalium) ambapo kwa sasa inahitajika idhini ya kitume kutoka Vatican katika kuwa na utambuzi halali wa taasisi yoyote mpya na jumuiya za kitume katika upatriaki. Katika barua hiyo inasema kulingana na mahitaji yaliyoidhinishwa na Makao makuu Vatican kuhusu uchaguzi wa Taasisi mpya za kidini ni kwamba tangu mwanzo wa Kanisa baadhi ya waamini walihisi kujiweka wafu kwa namna ya pekee katika maisha yao kwa ajili ya  huduma ya Mungu na ndugu, kwa  kushuhudia  mbele ya jumuiya kujiweka wakafu katika  ulimwengu kwa njia ya kuweka nadhiri za kiinjili, usafi, useja na utii.

Katika uzoefu wa kila mtu waiishi kwanza katika  nchi za Mashariki na baadaye za magharibi na zile za maisha ya ndugu kijumiya, zinazojikita katika Kanisa na katika utii wa wakuu. “Kwa maana hiyo ikatokea kama isemavyo mtaguso II wa Vatican kuwa Mamlaka ya Kanisa, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, yalifanya bidii kuyafafanua mashauri hayo, kuratibisha utekelezaji wake na kuasisi, kutokana nao, miundo thabiti ya maisha. Basi ikawa kama ilivyo katika mti uliopandwa na mbegu ya Mungu na kutoa matawi katika shamba la Bwana kwa namna za ajabu nyingi, ziliongezeka njia mbalimbali za maisha ya upweke na pamoja na familia mbalimbali, zinazositawi kwa ajili ya manufaa ya washiriki wake na kwa ajili ya wema wa Mwili wote wa Kristo(Katiba  ya kidogma juu ya Fumbo, Lumen Gentium 43).

Kanisa linawapokea kwa mitindo tofauti ya maisha ya wakfu kama inavyojionesha katika utajiri wa zawadi za Roho Mtakatifu, mamlaka ya kikanisa hasa Wachungaji wa Makanisa mahalia, watafsiri wa mashuri na kanuni za matendo na kuanza na hizo zinaunda mitindo yenye msimamo wa maisha, na kuzuia uwezekano wa kuundwa kwa taasisi zisiso na maana na wala ambazo  hazina ruhusa (Decreto Perfectae caritatis, 19). Makao makuu Vatican, kazi yake ni kuwasindikiza wachungaji katika mchakato wa kufanya mang’amuzi ambayo yanapelekea utambuzi wa kikanisa wa Tasisi mpya au chama chochote cha kitume chenye haki kijimbo na kuwa na neno la mwisho katika kufikia maamuzi kamili. Kwa maana hiyo katika Baru ya Kitume ya Papa Francisko ya Motu proprio, ameagiza kuwa ina nguvu thabiti, licha ya kitu chochote kinyume hata ikiwa inastahili kutajwa maalum na kwamba itangazwe kupitia chapisho la Osservatore Romano, na kuanza kutumika mnamo  tarehe 8 Desemba 2020 na baadaye ichapishwe katika ufafanuzi rasmi wa Acta Apostolicae Sedis. Barua iliandikwa Lateran, tarehe 21 Novemba 2020, katika Kumbukumbu ya kutolewa kwa  Bikira Maria Hekaluni, katika mwaka wa nane wa upapa wake.

07 December 2020, 16:03