Tafuta

2020.11.15 Sala ya Malaika wa Bwana 2020.11.15 Sala ya Malaika wa Bwana 

Papa Francisko aonya kuwa uvivu siyo wa kikristo.Umepewa mengi unaacha maskini afe na njaa?

Katika tafakari ya Papa Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini waliokusanyika uwanja wa Mtakatifu Petro amefafanua juu ya mfano wa talanta kama mafundisho kwa wote kwa namna ya pekee wakristo. Huo ni urithi ambao Mungu aliukabidhi kwa kila mtu tangu mwanzo wa maisha.Lazima kuifanyia kazi na sio kuificha kama alivyo fanya mtumwa wa tatu.Tabia ya namna hiyo inaonekana kwa walio wengi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ametoa mwaliko wa kuwatunza maskini, amejibu shutuma za wale wanaosema kwamba makuhani lazima wazungumze juu ya uzima wa milele na badala ya maskini lakini Papa amesema kuwa maskini wako katikati ya Injili, na amewaomba kila mtu akumbuke kwamba Yesu anatuambia kuwa yeye mwenyewe ni maskini anayehitaji. Amesema hayo wakati wa tafakari kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 15 Novemba 2020, kwa waamini wakati mama Kanisa anaadhimisha Siku ya Maskini duniani katika Dominika ya tatu ya mwaka. Injili ya siku ilikuwa inawakilishwa na mfano wa talanta, na jinsi ambavyo bwana mmoja alikuwa asafiri na kuwakabidhi talanta watumwa wake kadiri ya uwezo wa kila mmoja. Mmoja alipewa talanta tano, mwingine mbili na mwingine moja. Bwana ambaye anatujua vizuri, anajua kuwa hatufanani na hataki kumpa mtu yeyote upendeleo kwa wengine.

Wakati wa kukosekana kwa bwana, watumishi wawili wa kwanza waliifanyia kazi kwa bidii na kuongeza mara dufu ya dhamana waliyopewa, lakini wa tatu, yule ambaye alipokea talanta, moja  kwa kujiepusha hatari, akaichimbia talanta hiyo ndani ya shimo na kuiacha bila kuifanya izae  matunda. Na kwa maana hiyo, wakati bwana alikuwa akiwatuza watumwa ambao walifanya talanta zizalishe matunda, ndipo wakati huo mtumwa wa tatu alikuwa akijaribu kujitetea kutokana na uvivu wake kwa kumshutumu bwana kuwa mgumu na akawa amenyang'anywa talanta na kutupwa nje ya nyumba yake.

Papa Francisko amesema kuwa ni mfano ambao unatumika kwa kila mtu, lakini hasa kwa Wakristo, amesema Papa na kuongeza ni kwa sababu sisi sote tumepokea urithi kutoka kwa Mungu kama wanadamu, tangu kuanzia maisha yenyewe hadi uwezo wetu, lakini zawadi hizi lazima zitimizwe kama huduma kwa Mungu na kwa ndugu, kwa sababu hii ndiyo itakayohesabiwa katika hukumu ya mtu binafsi. “Leo ni Siku ya Maskini, mahali ambapo Kanisa linawaambia Wakristo kutoa kwa ukarimu kwa maskini. Wewe siyo peke yako maishani, kuna watu wanakuhitaji. Usiwe mbinafsi. Lazima sote tutumie zawadi zetu kwa wema.

Baba Mtakatifu Francisko ameendelea: “Leo Kanisa linakuambia kwa tumia kile ambacho Mungu amekupatia na uangalie maskini. Kuna wengi wao, hata katika miji yetu, katikati ya miji yetu! Tendeni wema! Kutotenda mabaya ni vizuri. Lakini kutenda wema si vizuri. Kuna njaa nyingi katika miji yetu, na mara nyingi tunaingia katika mantiki ya kutokujali. Mpe ukarimu  maskini, ni Kristo! Baadhi ya wengine wanasema kwamba maaskofu wanazungumzia juu ya maskini ... lakini sisi tunataka wazungumze  nasi juu ya uzima wa milele! Lakini tazama ndugu kaka au dada, maskini wako katikati ya Injili! Ni Yesu anazungumza nasi kwa njia  ya maskini! Wewe umepokea mambo mengi lakini unamruhusu kaka au dada yako afe na njaa?, Papa ameuliza.

15 November 2020, 14:44