Tafuta

2020.11.19 Economy of Francesco. Mkutano wa kwa njia ya mtandao. 2020.11.19 Economy of Francesco. Mkutano wa kwa njia ya mtandao. 

The Economy of Francesco-Kard.Turkson,vijana wameanzisha mtandao wa ulimwengu!

Katika hotuba ya Kardinali Peter Turkson,Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu katika ufunguzi amesema"Mmeamua kuanzisha mtandao wa ulimwengu wa vijana ambao uweze kufanya mabadiliko.Mmeamua kumsaidia Papa,Kanisa na ulimwengu ili kutimiza uchumi jumuishi na uliosawa,katika huduma ya wote,uchumi kijamii ambao unawekeza katika watu na kuhakikisha mafunzo na kazi yenye hadhi.

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican.

Papa Francisko alikuwa amezungumza kwa nguvu sana katika mzunguko wake wa katekesi baada ya wimbi la kwanza la janga, kwa kujikita juu ya ulazima wa “kuponesha ulimwengu dhidi ya ukosefu wa usawa, uliooneshwa na mgogoro wa kiafya. Virusi ni mtoto wa uchumi uliougua. Ugonjwa mmoja ambao ni tunda linalokua kwa sasa katika muktadha wa mabadiliko ya sasa ya uchumi na kutoa roho ya kesho. Kwa maana hiyo Papa Francisko mwezi Mei 2019 alikuwa amezindua wazo la “The Economy of Francesco”, akiwaalika wote kushiriki mwezi Machi 2020 mjini Assisi kwa maelfu ya vijana wanauchumi na wajasiriamali.

Kutokanana kuharishwa kwa sababu ya wimbi la kwanza la janga la corona tukio hili sasa limefunguliwa kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 19 kwa ushiriki wa vijana elfu mbili waliojiandikisha kutoka nchi 120, ili kushikamana, kwa siku tatu, ulimwenguni kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la francescoeconomy.org na ushiriki wa dhati kwa njia ya mtandao na Papa Francisko. Huko Assisi, ambayo inaongoza tukio, Profesa Luigino Bruni, wa Uchumi wa Siasa katika Chuo Kikuu cha Lumsa cha Roma na mkurugenzi wa kisayansi wa “Economy of Francesco”, yaani ‘Uchumi wa Francisiko’, amezungumza na studio za Radio Vatican Italia juu ya hali ya furaha na matumaini na anaelezea jinsi ambavyo Papa alivyoomba kuhuuisha uchumi kwa dhati.

Kurudisha roho na kuponesha uchumi uliougua

Kuhuisha inamaanisha kurudisha roho kwa sababu kurudisha roho katika uchumi ni mojawapo ya mada kuu ya mafundisho ya Papa Fransisko. Lakini pia inamaanisha kumhuisha mtu aliye mgonjwa na tena katika mawazo ya Papa, uchumi leo hii umeugua na hivyo unapaswa kuponywa. Kwa jinsi hiyo kuhuisha tena uchumi ni kucheza na maneno ambayo kwa hakika yana maana ya  mambo mawili, amebainisha Profesa Bruni. Kwanza ni kurudisha roho na kuponyesha uchumi uliougua. Na ndivyo hivyo hasa vijana ambao wamefanyia kazi kwenye tukio hili na wapo wanafanya kwa shauku yao yote na kujitoa. Profesa akiendelea amesema kuwa “Hatupaswi kufikiria kuwa vijana kuwa na shauku” tu, lakini kuna mengi, kujitoa sana kwa upande wao. Mchanganyiko huu wa shauku na kujitoa kwa labda ni jambo bora juu ya kazi ndefu ya maandalizi”.

Siyo ukuaji wote ni mzuri

Ukuaji ni moja ya maneno makuu na ufunguo wa mkutano huo amesema, lakini pia ni neno linalowezekana, kwa sababu sio ukuaji wote ni mzuri, kama tunavyojua. Hata wasiwasi zinaweza kukua: lakini kiukweli siyo tukio chanya hali nzuri. Kwa maana hiyo kunaweza kuwa na ukuaji mzuri, ukuaji wa ustawi, wa mali za uhusiano, wa mali za pamoja. Lakini ikumbukwe kuwa siyo ukuaji wote ni mzuri kabisa. Kwa kuendelea amesea “Sisi, kwa mfano, tumekua katika miaka arobaini iliyopita, tukiharibu sayari, kwa sababu hatukuzingatia athari za ukuaji. Sisi sote tulifurahi na Pato la Taifa ambalo lilikuwa likikua kwa 3 au 4% kwa mwaka. Mbaya sana kwamba wakati unakua tulikuwa tunaharibu mazingira ya asili yanayotuzunguka”.  “Kwa maana hii tunahitaji kukua, lakini pia tunahitaji kufikiria juu ya maendeleo, juu ya maeneo mengine mengi ambayo sio ya upimaji tu. Kwa sababu wakati tunazungumza juu ya ukuaji daima kuna shida kubwa sana kwamba hupimwa kwa idadi tu, kwa wingi, wakati vipimo vingi vya maisha ya mwanadamu hupimwa kwa ubora wake. Dhana ambayo siyo sehemu ya hesabu za kitaifa lakini ambayo ni muhimu” amesisitiza Profesa Luigino Bruni, mchumi na mhusika wa maandalizi ya “Economy of Francesco”.

Kuna haja ya mtaji wa kiroho. Wafanya biashara wanajua vizuri

Hatimaye akieleza juu ya suala la kiroho amesema kuna haja kubwa ya mtaji wa kiroho. Wafanyabiashara wanajua hii vizuri, lakini shida ni kwamba hali ya kiroho inahitaji upendeleo. Hali ya kiroho haiwezi kuzingatia suala la kuwa na faida. Hali ya kiroho inazingatia usafi wa watu ambao ndiyo hasa kama kampuni kubwa zinakosa. Hali kama hii amesema siyo rahisi kuitambua vema labda kufanyia kazi ya siku nne katika nyumba nzuri ya watawa huko Umbria... hata hivyo amesema ipangwe ili mapema au baadaye itoe kitu, kwa sababu kampuni inafuata mantiki ya kwanza ya hesabu kuwa mapema ua baadaye lazima irudi. Wakati hali ya kiroho inahitaji hewa iliyo huru, paa za juu kuliko zile za ofisi, inahitaji madirisha mkubwa kuliko yale ya viwanda vyetu. Kwa hivyo ni tumaini kwamba tukio hili pia ni wito wa uwekezaji katika hali ya kiroho ambayo uchumi unahitaji sana.

20 November 2020, 16:27