Tafuta

Siku ya Kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake Siku ya Kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake 

Siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake

Katika siku hii Papa amesema mara nyingi wanawake hukerwa, kutendewa vibaya,kubakwa,kushawishiwa kwa ukahaba.Ikiwa tunataka ulimwengu uwe bora na kwamba iwe ni nyumba ya amani na sio uwanja wa vita, lazima sote tufanye mengi zaidi kwa ajili ya hadhi ya kila mwanamke.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 25 Novemba ni maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Ni fursa ya kitafakari hata kwa njia ya maneno ya Papa Francisko kuhusiana na jeraha kubwa lililoenea ulimwenguni na ambalo katika kipindi cha janga la corona limekuwa la kutisha zaidi. Papa katika siku hii, kwenye mitanadao ya Kijamii amesema“mara nyingi wanawake hukerwa, kutendewavibaya, kubakwa,kushawishiwa kwa ukahaba. Ikiwa tunataka ulimwengu uwe bora na kwamba iwe ni nyumba ya amani na sio uwanja wa vita, lazima sote tufanye mengi zaidi kwa ajili ya hadhi ya kila mwanamke”.

Aidha Papa alisema “Ili kufahamu kiwango cha ustaarabu wa watu, jamii au mtu, inatosha kuangalia kati ya kuta za nyumba, kando ya barabara, kati ya picha za filamu au tangazo ya biashara. Kutokana na  jinsi tunavyouchukulia mwili wa mwanamke, tunaelewa kiwango chetu cha ubinadamu”. Alisema Papa Francisko wakati wa mahubiri yake Siku ya tarehe 1 Januari 2020. Papa Francisko akifafanua maana ya kuzaliwa na mwanamke alisema kuzaliwa kwa ubinadamu unaanzia na mwanamke. Wanawake ni kisima cha maisha. Walakini kila wakati huwa wanachukizwa, wanapigwa, wanabakwa, wanalazimishwa kufanya ukahaba na kukandamiza maisha wanayobeba tumboni mwao. Kila ukatili wowote, na  kudhulumiwa kwa wanawake ni kukufuru mbele Mungu aliyezaliwa na mwanamke.

wanamke lazima awe huru dhidi ya ununuzi wa kibiashara na kutumiwa, lazima aheshimiwe na kutukuzwa; ni mwili mzuri kabisa ulimwenguni, Yeye alichukua mimba na akazaa Upendo ulio tuokoa! Leo hii umama pia umedhalilishwa, kwa sababu ya ukuaji pekee unaotuvutia ni ukuaji wa uchumi. Kuna akina mama ambao wanajihatarisha katika safari zisizo na kizuizi ili kujaribu kutafuta maisha kwa maangaiko makubwa katika kupata tunda la  maisha bora ya baadaye na wakati huo huo wanahukumiwa kuwa ni namba kubwa na watu ambao matumbo yao yamejaa lakini kuwa na vitu na moyo mtupu usio na upendo. Kutoka kwa mwanamke alizaliwa Mfalme wa amani. Mwanamke ni mtoaji na mpatanishi wa amani na lazima ahusishwe kikamilifu na michakatoya kufanya maamuzi. Kwa sababau wanawake wakiwezesha  kuonesha zawadi zao, dunia hii itajikuta inaungana zaidi na kuwa na amani zaidi. Kwa maana hiyo mafanikio ya wanawake ni mafanikio ya ubinadamu wote.

Katika mahojiano ya Mwandishi Valentina Alazraki na yaliyotangazwa na Televisheni ya Mexico 2019, Papa alisisitiza kuwa ulimwengu bila mwanamke haufanyi kazi. Lakini katika kanda nyingi  za sayari, pamoja na Ulaya, wanawake wamegeuzwa  kuwa watumwa. “Nilipotembelea kituo cha kusadidia mhemko kwa wasichana katika katika Mwaka wa Huruma, mmoja alikuwa amekatwa sikio kwa sababu hakuwa ameleta pesa za kutosha. Wana udhibiti maalum juu ya wateja, kwa hivyo ikiwa msichana hafanyi wajibu wake wanampiga au kumuadhibu kama vile yule walivyofanya”.  Mwanamke hutoa mchango wa lazima kwa jamii, hasa na unyeti wake na akili kwa wengine, wadhaifu na wasio na ulinzi. Alisema haya Papa Francisko katika Mkutano  mnamo tarehe 25 Januari 2014, kwa washiriki wa Mkutano wa Kitaifa ulioandaliwa na Kituo cha Wanawake cha Italia. Nafsi ya mwanamke ni nguvu ya kweli kwa maisha ya familia, kwa mazingira ya utulivu na bila yeye wito wa kibinadamu hauwezi kutekelezwa. Sifa za zao kuu, unyeti wa kipekee na upole, ambayo roho ya kike ni tajiri, haiwakilishi nguvu ya kweli kwa maisha ya familia, kwa kuangaza hali ya utulivu na maelewano tu, lakini pia ni ukweli ambao bila wito wa kibinadamu haungewezekana. Na hii ni muhimu. Bila mitazamo hii, bila sifa hizi za wanawake, wito wa kibinadamu hauwezi kutekelezwa” alibainisha Papa.

25 November 2020, 16:53