Tafuta

2020.10.14 uharibufu wa makazi huko  Nagorno Karabakh -Stepanakert kwa sababu ya vita 2020.10.14 uharibufu wa makazi huko Nagorno Karabakh -Stepanakert kwa sababu ya vita 

Papa:Inatosha umwagaji damu kwa wasio na hatia katika vita ya Nagorno-Karabakh!

Inatosha uwagaji wa damu kwa wasio na hatia ndiyo ombi la Papa mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana.Amepyaisha wito wake ili migogoro iweze kumalizika.Amewakumbuka wathirika wa tetemeko la bahari ya Egeo pia kukumbusha juu ya Misa yake kwa ajili ya marehemu katika makaburi ya Vatican,tarehe 2 Novemba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko amekumbusha kutangazwa mwenye heri Michael Mc Givney wa Hartford nchini Marekani tarehe 31 Oktoba 2020 ambaye alikuwa ni Padre na Mwanzilishi wa Shirika la Kijeshi la Colombus aliyeridhiwa na wengine  na Papa Francisko kunako tarehe  26 Mei iliyopita alipokutana na Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu. Yeye alikuwa anajikita katika uinjilishaji na aliendelea kuwasaidiawenye kuhitaji, huku akihamasisha msaada bila kusita. Papa Francisko amesema mfano wake utoe chachu kwa wote ili kushuhudia daima Injili ya upendo. Kwa njia hii ameomba wamepigie makofi….

Vita na uharibifu huko Nagoro Karabakh pia tetemeko la nguvu bahari ya Ageo

Papa Francisko aidha amekumbusha kile kinachoendelea huko Nagoro Karabakha mahali ambamo amesema machafuko na mapigano ya kisilaha yanaendelea kudhoofisha wadhaifu na kuleta majanga na waathirika, uharibifu wa makazii, miundombinu na mahali pa kufanyia ibada, na ushiriki unaozidi kuongezeka wa idadi ya raia. Inasikitisha sana amesema Papa. Akiendelea na suala hili ameongeza “Ningependa kupyaisha wito wangu  kutoka moyoni kwa viongozi wa pande zote kwenye mzozo ili kuchukua hatua ya haraka iwezekanavyo kumaliza umwagaji wa damu kwa wasio na hatia. Wasifikirie kutatua ubishani ambao unapingwa na vurugu bali kwa kutafuta kushiriki mazungumzo ya dhati na msaada wa jamuiya ya kimataifa. Kwa upande wangu, niko karibu na wote wanaoteseka na ninawaalika tuombe kupitia maombezi ya watakatifu kwa ajili ya amani thabiti katika kanda hiyo” , Papa Francisko amesema. Vile vile ameomba kusali kwa ajili ya watu wa eneo la Bahari ya Egeo, ambao siku zilizopita wamekumbwa na tetemeko la nguvu la ardhi.

Mbio za kila siku kuu ya watakatifu wote

Papa Francisko ametoa salamu kwa waroma, mahujaji kutoka sehemu mbali mbali, kwa namna ya pekee sala kwa wanambio wa Siku ya watakatifu inayoandaliwa kila mwaka na Mfuko wa Don Bosco ulimenguni  ambao mwaka huu wanafanya mashindano kwa njia za umbali na binafsi. Papa amesema “Licha ya kufanyika katika vikundi vidogo kwa kufuata utengamano uliowekwa na janga, tukio hili la michezo linatoa mwelekeo wa sherehe maarufu katika maadhimisho ya  kidini ya watakatifu wote. Asante kwa hatua yenu na kwa uwepo wenu”.

Maadhimisho ya siku ya watakatifu

Papa Francisko amebainisha juu ya siku ya kuwaombea marehemu wote kwamba, mchana ataiadhimisha katika Makaburi teutonico mahali ambapo kuna makaburi katika mji wa Vatican.  Amethibitisha juu ya kushiriki kiroho na wote ambao kwa siku hizi wanafuata hatua za kiafya  na ambazo ni muhimu watakwenda kusali katika makaburi ya wapendwa wao kila kona ya Dunia. Na kwa wote wamewatakia siku kuu njema na usindikizwaji wa kirohoo wa kila mtatifu, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

01 November 2020, 17:08