Tafuta

2020.11.11 Katekesi ya Papa 2020.11.11 Katekesi ya Papa 

Papa:sala inatuliza wasiwasi na kujifungua moyo kwa Mungu

Sala inajua jinsi ya kutuliza wasiwasi lakini pamoja na hayo sisi hatujatulia,tunataka daima vitu kabla ya kuomba na tunataka mara moja.Ni jinsi gani ilivyo nzuri ikiwa sisi tunaweza kufanana kidogo na Mama yetu! Kwa moyo ulio wazi,kwa Neno la Mungu,kwa moyo wa kimya na moyo mtiifu,moyo unaojua jinsi ya kupokea Neno la Mungu na kuliruhusu likue na mbegu ya mema ya Kanisa.Ni maneo ya Papa wakati wa tafakari ya katekesi, Novemba 182020,

Na  Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Papa wakati wa tafakari ya  katekesi, tarehe 18 Novemba 2020, akiwa katika maktaba ya jumba la kitume, emeongozwa na sura ya Maria, mama wa Kanisa na mama yetu anayesali kwa ajili yetu na kusindikiza Kanisa. Papa akianza tafakari hii amesema katika safari yetu ya katekesi juu y sala, leo hii tunakutana na Bikira Maria, kama mwanamke anayeomba. Mama aliyekuwa anasali. Wakati ulimwengu ulikuwa unamdhrau, yeye mwenyewe akiwa msichana rahisi na aliyekuwa ameposwa na mwanaume wa nyumba ya Daudi, Maria alikuwa anasali. Tunaweza kifikiria kijana wa Nazareth aliyejiunda ndani ya ukimya akiendelea kuzungumza na Mungu, ambaye baadaye angeweza kukabidhiwa utume wake. Yeye tayari amejaa neema na asiye na dhambi, lakini bado hajuhi lolote la mshangao na wito maalum na baharí ya mawimbi makuu ambayo yangemsibu. Lakini jambo moja ni hakika. Maria ni wa kundi kubwa la wale wanyenyekevu wa moyo ambao wanahistoria rasmi hawajumuishwi katika vitabu vyao, lakini ambao Mungu ameandaa ujio wa Mwanawe. Maria haelekezi maisha kwa uhuru wake: anasubiri Mungu achukue hatamu za njia zake na amwongoze apendako. Yeye ni mpole, na na uwezekano wake,wa kuandaa tukio  kubwa ambalo linahusisha Mungu katika ulimwengu. Katekisimu ya Kanisa Katoliki inatukumbusha uwepo wake wa kila wakati, wa kujali katika mpango mwema wa Baba na katika kipindi chote cha maisha ya Yesu (taz. KKK, 2617-2618).

Papa Francisko akiendelea na tafakari kuhusu mama amesema : Maria alikuwa katika maombi wakati malaika mkuu Gabrieli alipokuja  kumpasha habari  huko Nazareti. Tazama mimi hapa, ndogo na kubwa sana, ambayo wakati huo ilifanya uumbaji wote uruke na furaha, na alikuwa ametanguliwa katika historia ya wokovu na wengine wengi  wa “mimi hapa”, na utii mwingi wa kuamini, na uwezekano wa mapenzi ya Mungu. Hakuna njia bora ya kuomba kuliko ilie ya kujiweka kama Maria katika hali ya uwazi, na moyo ilio wazi kwa Mungu: Bwana, unalotaka, kile ambacho unataka na jinsi gani unavyotaka”. Papa Francisko amesisitiza zaidi na kwamba  hii ina maana ya kuwa na moyo uliofunguliwa kwa mapenzi ya Mungu!.  Na Mungu hujibu kila wakati. Waamini wangapi wanaishi kwa maombi yao kwa njia hii! Wale walio wanyenyekevu zaidi wa moyo huomba hivi: “Bwana, unachotaka, na lini unataka na jinsi gani Unavyotaka”. Na hawa husali hivyo, bila kukasirika kwa sababu siku zimejaa matatizo, lakini wanakwenda  huku wakikutana na hali halisi kwa utambuzi kuwa katika upendo mnyenyekevu, katika upendo unaotolewa katika kila hali, tunakuwa vyombo vya neema ya Mungu. “Bwana, kile Unachotaka, wakati Unataka na jinsi Unavyotaka”. Sala hii ni rahisi, lakini ni kuweka maisha yetu mikononi mwa Bwana: na atuongoze. Sote tunaweza kuomba hivyo, karibu bila maneno”, Papa amezidi kuhimiza.

Sala inajua jinsi ya kutuliza wasiwasi Papa amebainisha na kwamba  pamoja na hayo  sisi hatujatulia, tunataka daima vitu kabla ya kuomba na tunataka mara moja. Ukosefu wa utulivu huo unatuumiza, na sala inajua jinsi ya kutuliza kutokuwa na utulivu, inajua jinsi ya kuibadilisha katika uwezekano. “Wakati sijatulia, ninasali na sala hufungua moyo wangu na kunifanya niwe na uewezakano kwa mapenzi ya Mungu. Bikira Maria, katika nyakati hizo chache mara baada ya kupashwa habari, alijua jinsi ya kukataa woga, pamoja na kutamka “ndiyo” yake  ambayo ingemletea majaribu magumu sana. Ikiwa katika maombi tunaelewa kuwa kila siku imetolewa na Mungu  basi ni wito, tunafungua mioyo yetu na tunamkabidhi kila kitu. Tunajifunza kusema: “Unachotaka, Bwana. Niahidi tu kwamba utakuwapo kila hatua nitakayopitia”.  Hili ni jambo muhimu: kumwomba Bwana kwa uwepo wake katika kila hatua ya safari yetu: kwamba asituache peke yetu, kwamba asituache katika majaribu, na kwamba asituache wakati mbaya. Hitimisho la sala ya Baba yetu ni kama hii: neema ambayo Yesu mwenyewe alitufundisha kumwomba Bwana. Maria alisindikiza kwa sala maisha yake yake yote Yesu hadi kifo na ufufuko wake; na hatimaye aliendelea kusindikiza hatua za kwanza za Kanisa linalozaliwa (taz Mdo At 1,14).

Maria anasali na wafuasi wa Yesu ambao wanapitia kashfa ya msalaba.Anasali na Petro aliyekumbwa na woga na kulia kwa sababu ya majuto. Maria yuko pale na wanafunzi, kati kati ya wanaume na wanawake ambao waliitwa na mwanae na kuunda jumuiya. Maaria siyo kuhani kati yao! Ni mama wa Yesu anayesali nao katika jumuiya na akiwa na jumuiya. Anasali na wao na kwa ajili yao.Na kwa upya sala yake inatangulia ya wakati ujao unaotaka kutimilika. Kwa njia ya Roho Mtakatifu amekuwa mama wa Mungu na kwa njia ya Roho Mtakatifu amekuwa mama wa Kanisa. Akisali na Kanisa changa, akawa Mama wa Kanisa, akasindiza  wanafunzi katika hatua za kwanza ya Kanisa kwa maombi, wakingojea Roho Mtakatifu. Katika ukimya, yeye daima alikuwa kimya. Maombi ya Maria ni ya ukimya. Injili inatuambia sala moja tu kutoka kwa Mama Maria alipokuwa huko Kana, wakati anamwomba Mwanawe, kwa ajili ya watu maskini, ambao walikuwa  karibu kufanya sikukuu ya aibu. Papa Francisko ametoa mfano wa fikiria  kuwa na sherehe ya harusi na kuimaliza na maziwa kwa sababu hapakuwapo na divai! Aibu  gani! Yeye alisali na kumwomba  Mwanae atatue shida hiyo. Uwepo wa Maria mwenyewe ni maombi, na uwepo wake kati ya wanafunzi katika Chumba cha Juu, wakingojea Roho Mtakatifu, yupo kwenye maombi. Kwa maana hiyo Maria anazaa Kanisa, yeye ndiye Mama wa Kanisa. Katekisimu  ya kanisa katoliki inaelezea: “Kwa imani ya mtumishi wake mnyenyekevu, Zawadi ya Mungu, ambayo ni, Roho Mtakatifu  hukaribishwa kama vile alivyotarajia tangu mwanzo wa nyakati” (KKK, 2617).

Katika Bikira Maria, ana uelewa wa asili ya  kike na kuimarishwa na umoja wake wa kipekee na Mungu katika sala. Kwa sababu hiyo, tukisoma Injili, tunaona kwamba wakati mwingine anaonekana kutoweka, ili aweze kuonekana katika wakati muhimu. Maria yuko wazi kwa sauti ya Mungu ambaye huongoza moyo wake, huongoza hatua zake pale uwepo wake unapohitajika. Anaonekana uwepo wake kimya wa umama na mwanafunzi. Maria yuko kwa sababu yeye ni Mama, lakini pia yuko kwa sababu ndiye mwanafunzi wa kwanza, yule aliyejifunza mambo ya Yesu vizuri zaidi.  Yeye alisema Fanya kile anachowambia”, kila wakati akimwonyesha Yesu. Mtazamo huo ni mfano wa mwanafunzi, na yeye ndiye mwanafunzi wa kwanza: anaomba kama Mama na anaomba kama mwanafunzi. Mama Maria alikuwa anaweka mambo yote hayo akiyatafakari katika moyo wake  (Lk 2,19). Ndivyo  Mwinjili Luka anamwonyesha Mama wa Bwana katika Injili ya utoto. Kila kitu kilichotokea karibu naye kiliishia kuwa na tafakari ya  kina cha moyo wake. Ni katika siku zilizojaa furaha, kama vile nyakati za giza zaidi, wakati yeye pia alipokuwa na ugumu wa kuelewa ni njia zipi  za Ukombozi lazima zitimizwe. Kila kitu kinaishia moyoni mwake, ili aweze kugeuzwa sura yake. Yote hayo kama vile  zawadi za Mamajusi, au kukimbilia Misri, hadi Ijumaa  kuu hiyo mbaya ya mapenzi ya Mungu. Mama alihifadhi kila kitu na kuwa na   mazungumzo yake na Mungu. Mtu fulani alilinganisha moyo wa Maria na lulu ya uzuri usioweza kulinganishwa, ulioundwa na kulainishwa na kukaribisha kwa subira mapenzi ya Mungu kupitia mafumbo ya Yesu yaliyotafakariwa katika maombi.  Ni jinsi gani ilivyo nzuri sana ikiwa sisi pia tunaweza kufanana kidogo kama Mama yetu! Kwa moyo ulio wazi, kwa Neno la Mungu, kwa moyo wa kimya na moyo mtiifu, na moyo ambao unajua jinsi ya kupokea Neno la Mungu na kuliruhusu likue na mbegu ya mema ya Kanisa, amehitimisha Papa Francisko.

18 November 2020, 16:25