Tafuta

Papa:roboti inaboresha ulimwengu ikiwa inajifafanua katika wema wa wote!

Katika nia za mwezi wa Novemba,itoletolewayo kila mwezi na Mtandao wa kimataifa wa Maombi kwa mwezi Novemba Papa Francisko anaangazia maendeleo ya akili bandia huku akikumbusha hitaji la kuelekeza kila wakati kuheshimu hadhi ya mtu na uumbaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni maendeleo ya haraka ambayo hayana hatari na athari mbaya ikiwa hayatawaliwi na yakizingatia umasikini wa mwanadamu. Hii ndio tabia ya akili bandia, mantiki ya kiteknolojia katika jamii ya leo ambayo Papa  Francisko anatoa maombi kwa waamini ulimwenguni kote. Kwa njia ya   video akiwa na nia ya maombi anayokabidhi kwa Kanisa lote kwa mwezi wa Novemba, Papa Francisko anabainisha, akiongea kwa lugha ya Kihispania, kwamba “akili ya bandia ni msingi wa mabadiliko ya  wakat tunaoupitia”. Na anaendelea: “Roboti inaweza kufanya ulimwengu  uwe bora iwezekanavyo ikiwa inajumuishwa  wema wa wote. Kwa sababu ikiwa maendeleo ya kiteknolojia yanaongeza ukosefu wa usawa kwa maana hiyo  sio maendeleo ya kweli”.

Tuombe ili maelendelo ya roboti yawe kwa huduma ya wanadamu

Kwa maana hiyo Papa anaonyesha njia ya kwenda kwa kukumbusha kwamba “maendeleo ya baadaye lazima yaelekezwe kuheshimu hadhi ya mtu na uumbaji”. Ombi lililopendekezwa ni lile ambalo halipotezi mtazamo wa ubinadamu. Papa Francisko anasema: "Tuombe ili kwamba  maendeleo ya roboti na akili za bandia ziweze kuwa katika huduma ya mwanadamu siku zote, au tuseme kuwa za kiutu”.

Hatua za maendeleo katika akili ya bandia

Katika taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Maombi wa kimataifa  wa Papa, ambao uhamasishwa na  mpango huu kila mwezi, maneno ya  Papa Fransisko yanawekwa katika muktadha kwamba  “Sio jambo jipya kwamba katika miaka ya hivi karibuni Akili  bandia (AI) umeendelea kwa kiwango kikubwa . Leo, asilimia 37% ya mashirika ya ulimwengu yametekeleza mpango huko (AI) kwa njia fulani, na ongezeko la asilimia 270% kwa miaka minne iliyopita.

Akili bandia na uwezo wa kutatua masuala mengi

Akili bandia ina uwezo wa kutatua masuala mengi. Taarifa hiyo kwa waandishi wa habari inaorodhesha badhi ya mambo ambayo yanawezekana, kama vile kutathmini uwezo wa wanafunzi wa kusoma, kusaidia watu wenye ulemavu, kukuza zana bora za mawasiliano, na kuwezesha ukusanyaji na usambazaji wa habari za kiafya ili kuboresha utambuzi na matibabu. Matumizi yake pia ni muhimu katika uwanja wa ekolojia: kwa mfano inaezekana kutathimini data juu ya mabadiliko ya hali ya hewa  na inaweza kuchambuliwa kutabiri majanga ya asili. Inaweza pia kutumika kuunda miji endelevu, na kupunguzwa kwa gharama za miji na kuongezeka kwa ufanisi wa nishati.

Inahitajika kuhakikisha fursa na ustawi kwa wote

Uwezekano wa kutumia maendeleo kwa faida ya wote ni kubwa sana na video ya Papa, iliyotengenezwa kwa  picha za Enel na Taasisi ya Teknolojia ya Italia, inaonyesha baadhi. “Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba, kama Papa Francisko Francisko anavyosisitiza, faida zinazotokana nayo zinasambazwa sawa swa  na kutoa fursa na ustawi, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Enel Francesco Starace. “Ili kuelekeza vyema hatua zetu na uchaguzi zinazohusu sasa na siku zijazo, heshima kwa watu na mazingira lazima viwekwe katikati, kupitisha maono kulingana na uendelevu wake . Ni kwa njia hiyo tu ndipo mageuzi ya kiteknolojia yanaweza kuwa mshirika wa wanadamu na kutoa fursa ambazo hata miaka michache iliyopita hatungeweza kufikiria “ amesisitiza mkurugenzi huyo. “ Ni jinis gani ingekuwa vizuri kama ukuaji wa ubunifu wa kisayansi na kiteknolojia ukwa unalingana na usawa zaidi na ujumuishaji wa kijamii! (Baba Mtakatifu Francisko, katika waraka wa Fratelli Tutti yaani Ndugu wote) "

Maendeleo na uwajibikaji lazima viende pamoja

“Mabadiliko ya jumuiya zetu pia hubadilisha kazi yetu. Haya ni mabadiliko ya haraka ambayo yanapaswa kusindikiza  ili iwe kwa faida ya wote , anasema Padre Frédéric Fornos SJ, mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Maombi ya Papa  Ulimwenguni. Kwa mujibu wa Padre amesema faida ambayo ubinadamu imepata, na ambayo itaendelea kupata kuanzia maendeleo ya kiteknolojia, lazima iwe pamoja na, sambamba, maendeleo ya kutosha ya uwajibikaji na maadili . Akili bandia, roboti na matumizi mengine ya kiteknolojia, yanafungua changamoto kubwa kwa maadili na haki ya kijamii. Kwa hili, ni muhimbi maombi ya Papa kusali kwa ajili ya maendeleo ili yanaweza kuwa ya kibinadamu siku zote, amehitimisha Padre Fornos.

05 November 2020, 17:25