Tafuta

 Papa Francosko Papa Francosko 

Papa kwa Caritas ya Slovenia:Kanisa limeungana,siyo mfananisho!

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa tamasha la hisani “Klic dobrote” kwa ajili ya shughuli za Caritas nchini Slovenia,amehimiza iwe na kielelezo cha maelewano ya umoja kati yao.Hawapaswi kuwa madhehebu yasiyoeleweka,au vyama,lakini kuwa na umoja. Kwa karama yao wenyewe,lakini kila wakati katika umoja.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa wandaaji wa tamasha la hisani kwa ajili ya Caritas nchini Slovovenia, lijulikanalo kwa jina la  “Klic dobrote” maana yake ‘wito wa ukarimu’ katika maadhimisho ya miaka 30  tangu kuanza suala hili la utamaduni na ufadhili ambao unajihusisha hasa katika utamaduni wa kipindi cha mwezi  mmoja kabla ya Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Papa Francisko, anawashukuru kwa kile ambacho wanafanya kwa ajili ya Caritas  na pia kusali ili ‘Klic dobrote’ mwaka huu iweze  kupiga hatua mbele na hatau zaidi kwa ajili ya muugano wa Kanisa na watu wao wote.

Mahali pasipo na umoja hakuna Roho ya Mungu

Miaka 30 inahitaji uvumilivu wa kwenda mbele anaadika Papa katika ujumbe huo, na kwamba anasali kwa ajili yao na kuwatakia matashi mema ya tamasha hili.  “Mahali pasipo na umoja, hakuna Roho wa Bwana, Bwana daima hutafuta umoja, ambao haumaanishi kufanana. Kila mmoja ana sifa zake, karama  yake mwenyewe, nafsi yake mwenyewe, lakini kila wakati katika umoja, na Roho wa umoja. Hatupaswi kuwa madhehebu yasiyo  julikana,ambayo ni kutenda mmoja dhidi ya mwingine; hatupaswi kuwa watu wa vyama ”. Hapana”, Papa Francisko ametoa onyo! Na amehitimisha kwa kuomba kwamba tamasha hilo liwe la maelewano na umoja kati yao na kuwabariki.

26 November 2020, 16:18