Tafuta

Sala ya Malaika wa Bwana Sala ya Malaika wa Bwana  

Papa Franciskoko:Tusikilize Mungu anapobisha mlango wa moyo wetu

Jumapili tarehe 29 Novemba umeanza mwaka mpya wa kiliturujia,kwa kufunguliwa na ki;inidi cha Majilio.Kipindi hiki ni mwaliko wa matumaini bila kuchoka.Kinatukumbusha kuwa Mungu yupo daima katika historia ili kutufikisha hadi mwisho katika utumilifu wake kwa njia ya mwanaye,Bwana Yesu Kristo.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Leo ni Dominika ya kwanza ya majilio ambapo umeanza mwaka mpya wa kiliturujia. Katika kipindi hiki Kanisa linajikita ndani ya mchakato wa maadhimisho msingi wa matukio ya maisha ya Yesu na historia ya wokovu. Kwa kufanya hivyo kama mama, anaangazia safari ya maisha yetu, na kutusaidia katika shughuli zetu za kila siku huku zikielekezwa katika mwisho kukutana na Kristo.  Liturujia ya siku inatualika kuishi kipindi cha nguvu ambacho ni Majilio, mwanzo wa mwaka wa kilituruja ambao unatuandaa kuelekea katika siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa maana hiyo ni kujiandaa kwa subira na  kupindi cha matumaini. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Papa Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 29 Novemba 2020, kwa mahujaji na waamini waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Papa Francisko akiangazwa na somo la Mtakatifu Paulo (1Kor 1,3-9) anaelekeza suala la subira katika maonesho ya Bwana. Mtume anaalika wakristo wa Korinto hata sisi kuwa na umakini juu ya kukutana na mtu Yesu ambaye atakuja mwisho wa ulimwengu na ambaye anakuja kila siku kwa sababu kwa njia ya  neema yake, sisi tunaweza kutumiza mema katika maisha yetu na yale ya wengine. Mungu wetu ni Mungu ambaye anakuja. Yeye hakatishi tamaa ya subirá! Alikuja katika wakati uliotabiriwa na wa kihistoria na kujifanya mtu kuchukua mwenyewe dhambi zetu: atakuja mwisho kama hakimu wa ulimwengu; anakuja kila siku kutembelea watu wake , kutembelea kila mwanaume na mwanamke ambao wanampokea katika Neno lake, katika Sakramenti na kwa  kaka na dada.

Kwa mkristo jambo muhimu ni mkutano na Bwana unaoendelea na kukaa naye. Na kwa kuzoea kukaa na Bwana katika maisha tunajiandaa vema kukutana naye na kukaa na Bwana katika milele. Bwana hakatishi tamaa. Papa Francisko amesisitiza.  Anaweza kufanya tusubiri labda wakati wa kipindi cha giza ili kutufanya tukomae matumaini yetu, lakini kamwe  hakatishi tamaa. Bwana daima anakuja na daima yuko karibu nasi. Ndiyo wakati mwingine hajioneshi lakini yupo anakuja. Wakati wa sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana ni kumbukumbu ya kuja kwake kwa mara ya kwanza Yesu katika kipindi cha kihisotria. Anakuja kwa mara ya pili ana ya tatu kwa njia tofauti. Katika biblia Yesu anatuambia kuwa yuko mlangoni anabisha. Kila siku.Yeye yupo katika mlango wa moyo wetu na kubisha. Wewe unatakiwa kusikiliza Bwana anayebisha, ambaye amekuja leo hii kwa ajili ya kukutembelea, ambaye anabidha katika moyo unaongaika, ule wenye mawazo. Alikuja huko Bethlehemu na atakuja mwisho wa ulimwengu lakini kila siku anakuja. Inabidi kuwa makini kutazama na kuhisi ndani ya moyo wakati Bwana anabisha.

Papa Francisko ameabainisha jinsiambavyo tunajua kuwa maisha kwa kawaidia yana matatizo, yaani  yenye mwanga na vivuli. Kila mmoja anafanya uzoefu wa kipindi cha kukatisha tamaa, kushindwa na kuhangaika. Zaidi ya hayo kipindi ambazo tunaisha cha janga, kinasababisha wasiwasi mkubwa, hofu na kukosa amani. Kuna hatari ya kuangukia kwenye ugumu, kujifungia na kutokuwa na upendo. Je tufanyeje mbele ya hayo? Mzaburi anatoa ushauri “roho yangu inamsubiri Bwana, yeye ni msaada na ngao yetu. Katika yeye moyo wangu unafurahi( Zab 32, 20-21). Papa Francisko ameongeza kusema roho ambayo inasuburi ujio kwa imani katika Bwana inapata nguvu na ujasiri wakati wa giza la maisha yetu. Na Je ujasiri huo unazaliwa wapi,  na ahadi ya imani?  Inazaliwa kutoka katika matumaini. Na matumaini hayakatishi tamaa , ile fadhila ambayo tunapeleka mbele kwa kutazamia mkutano na Bwana.

Majilio ni mwaliko usioisha wa matumaini. Anatukumbusha Mungu kuwa yupo katika historia kwa ajili ya kutufikisha mwisho wake na utimilifu ambao ni Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu yupo katika historia ya ubinadamu na Mungu yupo pamoja nasi anatembea karibu nasi ili kutusaidia. Mungu hayupo mbali daima nasi na  mara nyingi anabisha mlangoni pa moyo wetu. Bwana hatuachi kamwe; anatusaidia na katika mambo yetu ya maisha na kutusaidia tugunde maana ya safari, maana yake kila siku na kutupatia ujasiri wa majiribu na uchungu. Mbele ya migoro ya maisha, Mungu anatusaidia daima kwa mikono yake anatukomboa na hatari.  Sisi tumsubiri na kuwa na imani lakini pia naye ni matumaini yake kuwa hata sisi tutajionesha kwake. Maria Matakatifu atujalie kusubiri, atusindikize katika hatua zetu katika mwaka mpya wa kiliturujia tunao uanza, na atusaidie kutimiza shughuli yetu ya ufuasi wa Yesuna iliyoelekezwa na Mtume Petro. Je kazi ni ipi ni kutufanya kuwa sababu ya matumaini ambayo yamo ndani mwetu (1 Pt 3,15).

30 November 2020, 09:20