Tafuta

2020.11.15 Siku ya Maskini duniani 2020.11.15 Siku ya Maskini duniani 

Papa Francisko:Ufalme wa mbinguni unaanzia hapa&kuna hitaji la mshikamano!

Janga la covid,limepanua na kuonesha wazi zaidi matatizo na ukosefu wa usawa kijamii na kiuchumi ambapo tayari ulikuwa unasumbua sana bara la Amerika Kusini ambapo sehemu kubwa ya watu wana matatizo na maskini.Amesema hayo Papa kwa washiriki wa Semina kwa njia ya mtandao huko Amerika ya Kusini.Papa anaorodhesha matatizo na namna ya kukabiliana na majanga kwa njia ya mshikamano wa dhati kwa wanaoteseka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Semina kwa njia ya mtandao unaoongozwa na mada “Amerika ya Kusini: Kanisa, Papa Francisko na matukio ya majanga”, tarehe 19 Novemba 2020. Papa Francisko akianza ujumbe wake kwa njia ya video amewasalimia wote na kuangazia mada yao ambayo anasema inalengo la kuangazia na kutathimini hali ya janga la  Covid-19 barani Amerika ya Kusini na msaada wa mshikamano ambao unatakiwa uongozwe na wote ambao ni sehemu ya bara, na ambao kwa dhati wanasuka uzuri na matumaini ya bara lao. Anawashukuru waandaaji, akitumaini kuwa anzisho hilo linaweza kuigwa na kuamsha michakato ya kuunga mkono  muungano na kutoa mwamko kwa mikakati yote ya lazima ili kuhakisha maisha yenye hadhi katika watu wao hasa waliobaguliwa zaidi. Ni kwa njia ya uzoefu wa kidugu na ujenzi wa urafiki kijamii kwamba inawezeka.  “Ninaposema waliobaguliwa aina maana ya kutoa vijisenti kwa  omba omba , au kama ishara ya ufadhili, hapana ni kama ufunguo wa kweli wa mshikamano” Papa amesisitiza. Kuanzia hapo lazima kila eneo la pembezoni mwa wanadamu, kuwaajibisha kila mmoja kwani ikiwa hatuanzii hapo, tunakusea. Labda hii ndiyo usafishaji wa mawazo ya kwanza ambayo lazima yatendeke”, amesisitiza Papa.

Janga la covid, limepanua na kuoneshwa wazi zaidi matatizo na ukosefu wa usawa kijamii na kiuchumi ambapo tayari  ulikuwa unasumbu sana bara la Amerika Kusini ambapo sehemu kubwa ya watu wana matatizo na maskini amesema Papa. Ukosefu wa usawa na ubaguzi ambao unazidi kuongezeka kijamii, unaongezwa na hali halisi ambazo tunaishi kama vile magonjwa, na familia nyingi ambazo zinapitia ugumu wa ukosefu wa usalama na kutopata haki sawa kijamii. Hii inajionesha hata katika ugawaji wa vifaa vya kinga ya Covid-19; au wengine mahali pa kulala palipo na usalama wa kuwa na umbali kijamii, mazingira, kazi ya uhakika, ambayo iweze kumwakikishia maisha. Mambo hayo yote ni lazima kuyazingatia na kuwa na wawasi. Kwa kujiuliza je wote wanayo nyumba ya usalama? Je wote wanafikiwa maji? Je wote wanapata vifaa vya kujikinga katika mazingira. Je wana kazi ya usalama? Janga limeonesha wazi wazi hatari iliyopo katika mantiki hiyo.

Papa Francisko aidha amekumbusha,  kuwa  licha ya madhara ya janga la covid, lakini ndugu wengi wanaona kwa huzuni mkubwa wa mazingira yanayo wazunguka na hatari ya  vichaka na misitu yao kuharibiwa na moto kama vile Pantanal na Amazonia maeneo ambayo ameelezea kuwa ni mapafu ya Amerika ya Kusini na ulimwengu mzima. “Tunao utambuzi ya kuwa, matokeo ya janga tutaendelea kuyaishi kwa muda mrefu hasa kwa upande wa uchumi ambapo katika hali hii tunatakiwa kuwa na tumaini la mshikamano kama pendekezo la ubunifu katika uzito huo wa mgogoro”, anashauri Papa. Katika Ufalme wa Mungu ambao unaanza katika ulimwengu huu, mkate unaotufikia  ni kwa ajili ya wote na kubaki, ushirikiano kijamii, msingi wake ni kuchangia, kushirikisha na kugawanya, na siyo kumiliki binafsi, siyo kubagua na kujirundikia. Mambo hayo makuu Papa Francisko anasema ni lazima yapite ndani ya mawazo yetu. Kwa maana hiyo sisi sote tunaitwa kila mmoja binafsi na kwa ujumla kujikita katika kazi zetu au utume kwa uwajibikaji, uwazi na uaminifu. Janga limefanya kutazama vizuri au vibaya watu wetu na vema na vibaya kila mtu binafsi. Leo zaidi ya awali, kuna ulazima wa kuwa na dhamiri ya uwepo wa upamoja.

Virusi vinatukumbusha kwa namna ya kuweza kuanza kwa upya kutunzana na  kujifunza kumtumaini na kuwalinda wale ambao wako karibu nasi. Ni kuanzia na dhamiri ya mitaa, dhamiri ya watu, dhamiri ya mkoa na dhamiri ya nyumba yetu ya pamoja. Tunajua kuwa karibu  na janga la Covid-19, kuna magonjwa mengine ya kijamii kama vile ukosefu wa nyumba, ukosefu wa ardhi ukosefu wa kazi, mambo hayo matatu, ambayo  Papa amewakumbusha katika lugha yao ya kispanyola yanaitwa “T” tatu maarufu kama (techo, tierra, trabajo) ambayo yanasaidia kuwa kama kiongozi na kuomba jibu la ukarimu na umakini wa haraka, amesisitiza Papa. Mbele ya hali halisi kama hiyo, watu wa Amerika Kusini amesema wanatufundisha kuwa ni watu wa roho iliyotambua kukabiliana kwa ujasiri na migogoro na walitambua kutoa sauti ambayo kwa kupaza katika jangwa, waliweza kusikilizwa na Bwana. (Mik 1, 3). Pap Francisko ameshauri “ Tafadhali msiache kuibiwa matumaini! Safari ya mshikamano kama ile ya haki ni kielelezo bora na  chachu ya  pendo na ukaribu. Kuanzia  hapo ndipo tunaweza kuondokana na mgogoro huo  tukiwa bora, kama vile walivyoshuhudua kaka na dada zetu katika zawadi ya kila siku ya maisha yao na katika mambo ambayo watu wa Mungu walianzisha.

Papa Francisko aidha mtazamo wake, umekuwa ni kwa wale ambao wanamajukumu ya kisiasa, na kuomba ruhusa kwa mara nyingine taena wawe  na msimamo wa kisiasa ambao “wito mkubwa,  ni moja ya mtind owenye thamani ya hisani kwa sababu unatafuta ustawi wa pamoja”. Na kama alivyosema katika waraka wa hivi karibuni wa Fratelli tutti: “Kutambua kila mwanadamu kama kaka au dada na kutafuta urafiki kijamii ambao ni pamoja na kila mtu sio utopia tu. Kunahitaji uamuzi na uwezo wa kupata njia nzuri ya mchakato wao halisi una hakikisha uwezekano wao. Kila jitihada  yoyote katika mwelekeo huu inakuwa mazoezi ya hali ya juu ya hisani. Kwa sababu mtu binafsi anaweza kumsaidia mtu aliye na shida, lakini anapojiunga na wengine kutoa maisha kwa michakato ya kijamii ya udugu. Ni suala la kuendelea kuelekea mpangilio wa kijamii na kisiasa ambao roho yake ni hisani ya kijamii (Fratelli tutt n. 180).

Papa Francisko anawashauri ili kwamba kwa kusukumwa na mwanga wa Injili waendelea kutoka nje pamoja  na watu wenye mapenzi mema kutafuta wale ambao wanahitaji msaada, wafanane kama Msamaria mwema , kuwakumbusha zaidi walio wadhaifu (taz.Fratelli tutti n. 11). Mbele ya changamoto kubwa hizo, Papa anasema “tumwombe Bikira Maria wa Guadalupe ambaye ni mama wa ardhi ya Amerika ya Kusini asiache kuwa mama na wala kupoteza kumbu kumbu ya umama wake,  katika mgogoro atutengenisha na mgogoro hho na kutusaida tuthamishe utambuzi kuwa sisi sote ni ndugu wa Baba Mmoja atutazame kama alivyowazama mabazo zetu  (Lk, 1, 54-55) amehitimisha.

19 November 2020, 16:32