Tafuta

Papa:Siku ya Vijana kijimbo itafanyika Siku ya Kristo Mfalme mwaka ujao!

Papa Francisko amesema kuwa baada ya kusikiliza maoni mbali mbali kutoka Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha,wanaohusika na huduma ya vijana,ameamua kuhamisha, kuanzia mwaka ujao,sherehe ya majimbo ya Siku ya Vijana duniani(WYD) kutoka Jumapili ya Matawi hadi Siku ya Jumapili ya Kristo Mfalme.Katika kitovu hicho bado kuna Fumbo la Yesu Kristo Mkombozi wa mwanadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya  maadhimisho ya  Ekaristi Takatifu katika Kanisa Kuu la Makatifu Petro, Jumapili ya Siku Kuu ya Kristo Mfalme tarehe 22 Novemba 2020, Papa Francisko ameanza mahubiri yake na kusema “ninawapa salam ninyi nyote mliopo  hapa na wale wote wanafuatilia kwa njia ya vyombo vya habari. Salam kwa namna ya pekee inawaendea vijana wa Panama na Ureno, wanaowakilisha sehemu zote mbili ambazo muda mchache watafanya ishara muhimu ya kukabidhiana Msalaba na Picha ya Maria Salus Populi Romani; ishara za Siku ya Vijana duniani. Ni hatua muhimu ya hija ambayo itatupeleka huko Lisbon kunako 2023”. 

Papa Francisko akiendelea amesema “katika kujiandalia toleo hili ya Kimataifa la vijana ninapenda kuzindua hata maadhimisho katika Makanisa mahalia.  Miaka thelathini na tano imepita tangu kuanzishwa kwa siku ya vijana duniani ( WYD), na  baada ya kusikiliza maoni mbali mbali kutoka kwa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, wanaohusika na huduma ya vijana, nimeamua kuhamisha, kuanzia mwaka ujao, sherehe ya majimbo  ya siku ya vijana duniani( WYD) kutoka Jumapili ya Matawi  hadi  siku ya Jumapili ya Kristo Mfalme”.

Hata hivyo Papa  akifafanua kueleza maana yake amesema “Katika kitovu hicho bado kuna Fumbo la Yesu Kristo Mkombozi wa mwanadamu, kama vile Mtakatifu Yohane Paulo II, mwanzilishi na na msimamizi wa Siku ya Vijana  WYD, alivyokuwa akisisitiza kila wakati.” Papa Francisko ameongeza kusema kuwa “wapendwa Vijana, pigeni kelele na maisha yenu kwamba Kristo anaishi, na kwamba Kristo anatawala, na kwamba  Kristo ndiye Bwana! Ikiwa mtakaa kimya, nawahakikishia kwamba mawe yatalia” (Lk 19,40), amehitimisha.

22 November 2020, 16:18