Tafuta

Papa Francisko na Mkuu wa shirika la Mateso ya Yesu Kristo. Papa Francisko na Mkuu wa shirika la Mateso ya Yesu Kristo. 

Papa Francisko:pelekeni moto wa upendo wa Yesu ulimwenguni!

Papa Francisko amemtumia barua Mkuu wa shirika la Mateso ya Yesu Kristo kufuatia na maadhimisho ya Jubilei ya miaka 300 tangu kunzishwa kwa shirika lao akionesha shukrani ya fursa ya kuungana nao kiroho katika furaha kwa ajili ya zawadi ya miito ili kuishi na kuangaza kumbu kumbu ya Mateso ya Kristo.Ni kwa yule aliyesulibiwa na upendo kama Yesu msalabani ana uwezo wa kukumbilia wasulibiwa wa historia kwa maneno na matendo ya dhati.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amemtumia barua Mkuu wa shirika la Mateso ya Yesu Kristo (Passionists), Padre Joachim REGO C.P.; kufuatia na maadhimisho ya Jubilei ya miaka 300 tangu kunzishwa kwa shirika lao akionesha shukrani ya  fursa ya kuungana nao kiroho katika furaha kwa ajili ya zawadi ya miito waliyopokea ili kuishi na kuangaza kumbu kumbu ya Mateso ya Kristo, huku wakifanya fumbo la Pasaka kuwa kiini cha maisha yao.  Papa anaonesha wazi karama yao kama ilivyo ya kila mwenye wakfu kwamba  ni mwangaza wa upendo wa wokovu ambao unatokana na fumbo la utatu, na unaoonesha upendo wa Msulibiwa (taz Wosia: Maisha ya wakfu 17-19. 23), na ambao msingi wake ni mtu aliyechaguliwa kwa upendo katika tarehe  ya jumuiya, kupandwa katika Kanisa ili kutoa jibu kwa namna ya pekee hitaji la historia. Na ili karama iweze kudumu kwa muda mrefu inahitaji upyaisho, kwa kuzingatia chachu ya  nguvu mpya ya ubunifu.

Papa Francisko amesema kuwa katika fursa ya miaka 300 hiyo inawakilisha fursa ya kutembea katika kuelekea maono ya kitume bila kuangukia katika vishawishi vya kuacha mambo kama jinsi yalivyo(Evangelii gaudium, 25). Hii ni katika kuwasiliana na Neno la Mungu kwa njia ya sala, kusoma ishara za nyakati, na matukio ya kila siku ambayo yanawawezesha kuelezea upeo wa ubunifu wa Roho Mtakatifu ambaye anavuvia kwenye wakati akitarajia  majibu kutoka katika jumuiya. Ubinadamu katika kutafuta mabadiliko, umejiweka katika mjadala si katika thamani ya utamadini ambao umetajirishwa hadi leo hii, lakini hadi kufikia uundaji wake wenyewe.  Shukrani ni kwa ajili ya uzoefu ya yule aliyeishi wakati uliopita kwa tabia ya kusifu na kutembea ili kueleza wakati ujao kwa mtindo wa Ekaristi. Shukrani ni tunda la kumbu kumbu ya mateso. Kutafakari kwa kina na jitihada ya kutangaza upendo ambao ulitoka juu ya msalaba, kwa muda mrefu unaendelea katika historia ambapo umetimizwa na furaha. Tumaini ni furaha kwa kile ambacho kipo badala ya kulalamika kwa kile ambacho hakuna, anasisitiza Papa Francisko. Kwa maana nyingine anawashauri wasiache waibiwe furaha ya kuinjilisha  (Evangelii gaudium,83).

Papa Fracisko anawatakia wanashirika wote ili waweze kuhisi soko la moto, wa utume unaojikita mizizi yake katika kumbukumbu ya mateso. Mwanzilishi wao Mtakatifu Paulo wa msalaba kwa kujiita "Mateso ya Yesu”, ilikuwa ni kazi iliyo kubwa sana na ya upendo wa Mungu wa ajabu (Barua II, 499).  Kwa upendo huo alikuwa anahisi kuungua na angeweza kuchoma ulimwengu mzima kwa shughuli za kimisionari binafsi na wenzake. Ni jinsi gani ilivyo muhimu anasema Papa kwamba utume wa kimisionari ni mateso kwa ajili ya Yesu lakini wakati huo huo ni mateso ya watu wake. “Tunapokuwa mbele ya Yesu Msulibiwa, tunatambua upendo wake wote, lakini wakati huo huo tusipokuwa vipofu, tutaanza kutambua mtazamo ule wa Yesu ambaye anapanua na kutukumbatia kwa upendo na zaidi shauku kubwa kwa watu wake", amesisitiza Papa

Papa Francisko amewaomba wasiache jitihada zao kusadia mahitaji ya ubinadamu. Umisionari kwa mara nyingine  tena hasa kuelekeza waliosulibiwa katika nyakati hizi ni maskini, wadhaifu, walisongwa, walibaguliwa na aina mbali mbali za ukosefu wa haki. Hali halisi katika hao inahitaji ushiriki wao wa kweli na jitihada za upyaisho wa kina ambao unatokana na uhusianao binafsi na Msulibiwa na mfufuka. Ni kwa njia ya  yule tu aliyesulibiwa na upendo kama alivyo fanya Yesu Msalabani ana uwezo wa kusadia waliosulibiwa katika historia kwa maneno na matendo ya dhati. Hii ni kutokana na kwamba haiwezekani  kuthibitisha upendo wa Mungu kwa wegine kwa njia ya maneno na  nadharia tu. Inahitaji ishara za dhati ambazo zifanyiwe uzoefu wa upendo kwa kujitoa na kuwashirikisha wasulibiwa, kujitoa hadi maisha, huku wakitangaza na kukaribisha kwa imani matendo ya Roho Mtakatifu.  Papa Franciso amehitimisha kwa kuwakabidhi kwa Mama wa msulibiwa na mfufuka, sura ya Kanisa, Bikira ambaye anasali na kutoa maisha, pia kwa mwanzilishi wa Shirika Mtakatifu Paulo wa Msalaba, watakatifu na wenyeheri wa shirika hilo.

19 November 2020, 15:21