Tafuta

2020.11.02  Papa Francisko ameathimisha misa kwa ajili ya waamini marehemu na katika sala kwenye makaubiri ya Teutonico na katika  Groto za Vatican. 2020.11.02 Papa Francisko ameathimisha misa kwa ajili ya waamini marehemu na katika sala kwenye makaubiri ya Teutonico na katika Groto za Vatican. 

Papa Francisko:Matumaini baada ya kifo yanatoa maana ya maisha

Katika mahubiri ya Papa Francisko ya kuombea waamini marehemu katika Kanisa lililoko kwenye makaburi ya teutonico,Vatican,ametumia maneno ya Ayubu kuwa ya kwake na kukumbusha kuwa uhakika wa kikristo wa maisha ya baadaye ni zawadi ya bure ya Mungu ambayo lazima kumuomba.Badaye amekwenda kwenye groto zilizoko kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili kuombea kuombea Mapapa marehemu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika wakati wa furaha na wakati mbaya sana, katika majaribu, hata kifo kinapokaribia, tunaweza kusema kama Ayubu: ninajua kuwa Mwokozi wangu yu hai, na kwa macho yangu nitamwona. Haya ndiyo matumaini ya kikristo, zawadi ambayo ni Bwana peke yake anaweza kutujalia ikiwa tunamwomba. Leo hii, katika mawazo ya ndugu kaka na dada ambao waliondoka, itakuwa vizuri kuwatazama vema na kuangalia juu kwa kurudia maneno ya Ayubu. Ndiyo umekuwa moyo wa mahubiri ya Papa Francisko aliyotamka bila kusoma wakati wa misa kwa ajili ya kuwaombea waamini marehemu katika misa aliyoadhimisha majira ya mchana tarehe 2 Novemba 2020, katika Kanisa la Mtakatifu Maria la Teutonic kabla ya kusali mbele ya makaburi ya Vatican na baadaye katika Mapango ya Vatican, mbele ya makaburi ya mapapa marehemu.

Papa ametafakari  juu ya kifungu kutoka somo la Kwanza la liturujia ya siku  iliyochukuliwa kutoka Kitabu cha Nabii Ayubu, ambaye alishinda, na kuwa mvulimivu katika ugonjwa, na ngozi yake iliharibiwa  karibu, hadi kufa, lakini bado alikuwa na  uhakika na kusema: “Najua kwamba Mkombozi wangu yu hai na kwamba, mwishowe, atainuka juu ya mavumbi. Papa Francisko amesisitiza “Ayubu yuko chini zaidi, chini, chini”, lakini katika wakati huo “ni hali halisi ya  kukumbatia nuru na joto ambayo ilimtuliza na kusema “Nitamwona Mkombozi na macho haya, macho yangu yatamtafakari, na sio mwingine”.

Papa  amesisitiza, kuwa “ukweli huu,wakati wa ukaribu wa mwisho wa maisha, ni tumaini la Kikristo. Tumaini ambalo ni zawadi. Hatuwezi kuwa nayo, lakini lazima tuiombe: Bwana, nipe tumaini. Kuna mambo mengi mabaya sana, Papa  Francisko ameendelea, ambayo hutupelekea kukata tamaa, kuamini kwamba kila kitu kitakuwa ushindi wa mwisho, na  kwamba baada ya kifo hakuna kitu. Lakini sauti ya Ayubu inarudi tena. Matumaini hayatukatishi tamaa, Paulo alitueleza. Tumaini linatuvutia na kutupatia maana ya maisha na kuacha tabia za kusema kuwa mimi sioni maisha ya baadaye. Lakini matumaini ni zawadi ya Mungu ambayo inatuvuta kuelekea maisha, kuelekea furaha ya milele. Tumaini ni nanga ambayo tunayo kwa upande mwingine, sisi, tukishikilie kamba, tunasaidiana. Ninajua kwamba Mwokozi wangu yu hai na nitamwona. Na hii, ni kuirudia na kusema wakati wa furaha na wakati mbaya na wakati wa kifo” Papa Francisko ameshauri..

Tumaini, Papa Francis ameongeza kusema  ni zawadi ya bure ambayo hatustahili kamwe, kwa maana  inatolewa na kupewa. Ni neema. Na katika kifungu cha Injili ya Yohana, Yesu anathibitisha tumaini hili ambalo halitukatishi tamaa. Wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu. Hili ndilo lengo la tumaini la kwenda kwa Yesu”, Papa amesisitiza. Na yule anayekuja kwangu, sitamtupa nje. Bwana, anahitimisha na hivyo ni yeye ambaye hutupokea huko, ambapo nanga ipo. Maisha ya tumaini ni kuishi hivi, Papa amesisitiza  na kwa kwa maana hiyo kushikilia na kamba mkononi, kwa nguvu, huku kwa kutambua kwamba nanga iko pale. Na haikatishi tamaa. Leo, hii kwa mawazo ya kaka na dada wengi ambao wamekwisha ondoka yatatusaidia kutazama makaburi na kuangalia juu na kurudia, kusema kama Ayubu: “Najua kwamba Mkombozi wangu yu hai na nitamwona, mimi mwenyewe; macho yangu yatamtazama, na sio mwingine”. Na hii ndiyo nguvu inayotupatia tumaini, zawadi hii ya bure ambayo ni sifa ya tumaini. Bwana atupatie sisi sote” Papa amehitimisha.

02 November 2020, 17:00