Tafuta

2020.11.25 Katekesi ya Papa Francisko 2020.11.25 Katekesi ya Papa Francisko  

Papa Francisko:Kanisa sio soko wala chama imetengenezwa na Roho Mtakatifu

Katika Katekesi ya Papa Francisko amezungumzia juu ya Jumuiya ya kwanza ya Kikristo kama inavyoeleza na kitabu cha Matendo ya Mitume ambao waliishi na kudumu katika maombi.Hakuna Kanisa ikiwa panakosekana usikivu wa Neno,muungano wa kidugu,Ekaristi na sala.Ni Mungu anayetengeneza Kanisa kwa njia ya Roho Mtakatifu na sio kelele za kazi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Papa Francisko akianza tafakari yake katika katekesi ya Jumatano tarehe 25 Novemba 2020, katika mwendelezo wa mada ya sala, akiwa katika Maktaba ya Jumba la kitume mjini Vatican, ameongozwa na mtazamo wa Jumuiya ya kwanza ya mitume kama inavyofafanuliwa  Jumuiya hiyo ya kikristo huko  Yerusalem kwa mujibu wa somo kutoka  Matendo ya Mitume (At 4,23-24.29.31). Papa Francisko amesema mchakato wa hatua za kwanza za Kanisa zilikuwa zimejikita katika sala. Waandishi wa kitume na wasimulizi wa Matendo ya Mitume wanaonesha picha ya Kanisa katika safari inayojishughulisha na ambayo lakini inakutana kwenye mikuntano ya sala, msingi na shauku ya matendo ya kimisionari. Picha ya Jumuiya ya kwanza ya Yerusalemu ni kiini cha hatua ya kumbukumbu kwa kila uzoefu mwingine wa Kikristo. Luka anandika katika kitabu cha Matendo ya Mitume kwamba “hawa wote waliendelea katika mafundisho ya mitume na katika mikutano huku wakiumega mkate na kusali (Mdo 2,42).

Papa Francisko amesema katika sehemu hizi kuna tabia nne muhimu za maisha ya Kikanisa: kusikiliza mafundisho ya mitume, kulinda umoja katika kuelewana, kuumega mkate na kusali. Hawa wanakumbusha uwepo wa Kanisa likiwa na maana ya kubaki kidete na muungano na Kristo. Kuhubiri, na katekesi zinashuhudia maneno na ishara za Mwalimu. Kutafuta bila kuchoka umoja wa kidugu na kuepuka ubinafsi na umaarufu; kuumega  mkate unatimiza sakrameti ya uwepo wa Yesu katikati yetu. Yeye hatakosekana kamwe, Yeye anaishi na kutembea na sisi. Na mwisho ni maombi ambayo ni nafasi ya mazungumzo na Baba kwa njia ya Kristo katika Roho Mtakatifu. Papa Francisko amesema. Kanisa sio soko; Kanisa sio kikundi cha wajasirimali ambao wanakwenda na kazi yao  mpya. Kanisa ni kazi ya roho Mtakatifu ambayo Yesu alitutumia ili kutukusanya. Kanisa ni kazi ya dhati ya Roho Myakatifu katika Jumuiya ya Kiristo, katika maisha ya jumuiya, katika Ekaristi katika sala… na daima. Yote ambayo yanakua nje ya uratibu huo yanakosa msingi, ni kama nyumba iliyojengwa juu ya mchanga (Mt 7,24-27). Ni Mungu anayetengeza Kanisa na sio Kilele za Kazi. Ni neno la Yesu linalojaza maana ya jitihada zetu. Linaangaza na kujenga wakati ujao wa ulimwengu, amesisitiza Papa Francisko.

Papa Francisko aidha amebainisha ni kwa jinis gani anakuwa huzuni anapoona baadhi ya jumuiya katika mapenzi mema, lakini wanakosea njia kwa sababu ya kufikiria kutengeneza Kanisa katika kukusanyika, utafikiri ni chama cha kisiasa. Lakini walio wengi au wachache wanafikiria hili na lile, ni kama Sinodi, yaani njia ya sinodi ambayo anasema ni lazima kuifanya. Lakini anauliza maswali, je Roho Mtakatifu yuko wapi? Je sala iko wapi; Je upendo wa kijumuiya uko wapi?; Je Ekaristi iko wapi? Bila uratibu wa mambo hayo manne, Kanisa linageuka kuwa jamii ya binadamu, chama cha kisiasa, kikuu au kidogo, mabadiliko yanafanywa kama vile kampuni, iliyo ndogo au kubwa… Lakini hakuna Roho Mtakatifu. Na uwepo wa Roho Mtakatifu ni udhihirisho wa uratibu wa mambo manne. Ili kutathimini hali kama ni ya kikanisa au siyo, tujiulize juu ya utarabu wa mambo hayo manne, amesisitiza Papa Francisko. Maisha ya jumuiya, maombi, Ekaristi na muungano kidugu. Je ni jinsi gani ya kuendeleza maisha hayo katika mambo hayo manne? Ikiwa hayapo basi roho inakosekana hivyo kitakuwa ni chama kizuri cha kibinadamu, cha ufadhili, hata cha kisiasa tunaweza kusema hivyo.   Lakini siyo Kanisa! Ndiyo maana Kanisa haliwezi kukua bila kuwa na misingi hiyo, kwa sababu linakuwa si kwa njia ya upropaganda, au kama aina yoyote ya kampuni badala yake kwa ajili ya mvutio. Je ni nani mwanzilishi wa mvutio huo? Ni Roho Mtakatifu. Papa Francisko amehimiza kutosahau maneno ya Papa Mstaafu Benedikto XVI ambaye alisema “Kanisa halikui kwa propaganda, hukua kwa mvuto”. Ikiwa Roho Mtakatifu anakosekana, ambaye ndiye inaayemvutia Yesu, hapo hakuna Kanisa. Kuna Club nzuri ya marafiki, kwa nia njema, lakini hakuna Kanisa, hakuna muungano, amesisitiza Papa.

Tunaposoma  kitabu cha Matendo ya Mitume, tunagundua kwa maana hiyo jinsi injini ya uinjilisha inavyotokana na muungano wa sala, mahali ambamo anayeshiriki uzoefu hai wa uwepo wa Yesu naguswa na Roho. Wajumbe wa Jumuiya ya kwanza, lakini hata hivyo ni ile inayotakiwa iwe hata ya sasa leo  na daima kwetu sisi, Papa amesema walitambua kuwa historia ya kukutana na Yesu, haikusimama wakati wa Kupaa kwake. Lakini inaendelea katika maisha yao. Kwa kusimulia kile alichosema na alichofanya Bwana, kwa kusali ili kuingia katika muungano na Yeye na yote yanageuka kuwa hai. Sala intoa mwanga na joto. Zawadi ya Roho Mtakatifu inafanya kuzaliwa ndani mwao shauku kubwa.   Katika muktadha huo Katekisimu ina kielelezo cha kina sana. “Roho Mtakatifu anayeshikili kumbukumbu hai ya Kristo katika Kanisa lake linalosali anaongoza pia kwenye kweli yote na anavuvia miundo mipya inayoelekeza fumbo lisiloelezeka la Kristo anayetenda kazi katika maisha ya sakramenti na katika utume wa Kanisa lake (n. 2625). Tazama ndiyo kazi ya Roho Mtakatifu katika Kanisa, ni kukumbuka Yesu. Lakini sio kama zoezi na mantiki ya kielimu na kiufundi. 

Wakristo, kwa kutembea katika nyayo za utume, wanakumbuka Yesu huku  wakimfanya awe hai, katika maisha yao yote na  kutoka kwake na Roho yake, wanapokea msukumo wa kwenda kutangaza na kuhudumia. Katika sala mkristo anaingia ndani ya fumbo la Mungu ambaye anapenda kila mtu na anatamani kuwa Injili iweze kutangazwa kwa wote. Mungu ni Mungu wa wote na kwa Yesu kila ukuta wa mahangaiko unanguka kabisa. Anasema hivyo Mtakatifu Paulo “Yeye ni amani yetu ambaye amefanya jamii kuwa moja kwa maana katika mwili wake yeye mwenyewe aliubomoa ule ukuta uliowatenganisha na kuwafanya maadui.(Ef 2,14). Ndiyo hivyo maisha ya Kanisa la kwanza, lilibaki na kuendelea kuadhimisha, kukutana, katika nyakati za sala ya jumuiya na binafsi. Ni Roho ambaye anatoa nguvu kwa wahubiri ambao wanajiweka katika safari na kwa sababu ya upendo wa Yesu wanavuka bahari, wanakabiliana hatari, na kujinyenyekeza. Mungu anatoa upendo na kuomba upendo. Huo ndiyo mzizi wa tafakari kuu ya maisha yote ya mwamini. Wakristo wa kwanza wakati wa kusali lakini hata sisi ambao tumefika baada ya karne nyingi zilizopita, tunaweza kuishi na kufanana na uzoefu huo, Papa Francisko ameshauri. Roho Mtakatifu anaongoza kila kitu. Kila mkristo ambaye hana hofu ya kujikita katika muda wa sala anaweza kweli kuyafanya maneno  yake ya Mtakatifu Paulo kuwa yake: “Maisha haya ninayoishi sasa naishi kwa amani, imani katika Mwana wa Mungu aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu”, (Gal 2,20). Ni katika ukimya wa kuabudu inawezekana kupata ukweli wote wa maneno haya. Na lazima turudie tena hali ya kuabudu. Mwabudu, muabudu Mungu, muabudu Yesu, muabudu Roho. Baba, Mwana na Roho: kuabudu kwa ukimya. Sala ya kuabudu ni sala inayotufanya kumtambua Mungu kama mwanzo na mwisho wa historia yote. Na sala hii ni moto hai wa Roho ambao hutoa nguvu ya kushuhudia na utume.

KATEKESI PAPA 25

 

25 November 2020, 15:56