Tafuta

Papa Francisko:Imani mbele ya mauti inabadilisha kila kitu

Papa Francisko wakati wa mahubiri yake kwenye Misa ya kuwaombea marehemu Kardinali na maaskofu waliofariki kwa mwaka huu,amesema kuwa imani inabadilisha mategemeo na kumwalika anayeamini aweze kuongoka.Kifo siyo mwisho wa kila kitu,maana Yesu ni uzima wa maisha ya milele.Bwana hatuachi,bali anabaki daima nasi.Ni mwaminifu katika ahadi yake.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vtican.

Papa Francisko wakati wa kuanza mahubiri yake, Siku ya Alhamisi tarehe 5 Novemba  2020 wa misa kwa ajili ya Marehemu Makardinali na Maaskofu ambao walikufa kwa kipindi cha mwaka huu,  amesisitizia juu ya imani kubwa ya ufuko wa katika Bwana. Misa Takatifu imeadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa ushiriki wa waamini wachache tu kufuatia na sheria zinazoendelea za kuzuia maambukizi ya covid. Katika Injili iliyosomwa Yh 11,17-27,  Yesu anatangaza uonesho  wake kuwa “Mimi ndimi ufufuko, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi milele” (Yh 11, 25-26). Mwanga mkubwa wa maneno hayo unajionesha  wazi katika giza la msiba mkubwa wa kifo cha Lazaro. Marta anampokea kwa imani thabiti ambayo anathibitisha wazi kuwa “Ndiyo Bwana mimi ninaamini kuwa wewe ni Kristo Mwana wa Mungu ambaye alikuja ulimwengunini”. Maneno ya Yesu, yanampatia Marta matumani kwa  wakati uliopo kwenda wakati ujao, yaani ufufuko ambao tayari upo karibu kwa maana ya uwepo wake wake Kristo.

Papa Francisko akiendelea na takafakari yake amesema “Kujifunua  kwa Yesu leo hii, ni mwaliko kwa wote, kwamba tunaalikwa kuamini katika ufufuko na sio kama aina ya mwangaza wa juu ya upeo wa macho tu, lakini kama tukio ambalo  tayari lipo  linalotuhusisha kwa kushangaza sasa.  Pamoja na hayo yote imani katika ufufuko haidharau wala kuweka barakoa ya kujificha  lakini ni  kufanya uzoefu wa kibinadamu mbele ya kifo. Bwana Yesu mwenyewe kwa kuona dada zake Lazaro wanalia na wale ambao waliokuwa wamewazunguka, bila hata kuficha hisia hizo mwinjili anaonesha kuwa aliangukia katika kilio (Yh11,35). Pamoja na kwamba yeye hana dhambi lakini anashiriki mshikamano na binadamu, alifanya uzoefu wa maombolezo, uchungu wa machozi yaliyo ndondoka kwa sababu ya mtu mpendwa. Jambo hilo halikupunguza ukweli wa mwanga wa uwezo wake na ambao anasema ni ufufuko ukawa ishara kwa kumfua Lazaro. Papa Francisko aidha amesema hata sisi Bwana anatuleza kuwa “mimi ni ufufuko na maisha. Anatualika kupyaisha imani kuu, kuingia tangu sasa katika mtindo wa kufikiria mwanga wa Ufufuko. “Naye aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? (Yh 26). Jambo hilo linapotokea, kwa namna yetu ya kufikiria na kutazama mambo inabadilika.

Macho ya imani, kwa kutazama yasioonekana yanaona kwa yale ambayo yanaonekana (Eb 11,27). Kadhalika Papa amesisitiza kuwa hicho ndicho kinachoonesha katika sehemu ya kitabu cha Hekima. Kifo cha mapema cha mwenye haki kinafikiriwa na maoni tofauti kulingana na mantiki ya kawaida. “Aliyempendeza mungu naye Mungu akampenda, wakati alipokuwa anaishi na wenye dhambi, Mungu alimchukua, akamhamisha ili uovu usibadili busara yake, udanganyifu usiweze kuipotosha roho yake (Hk 4,10-11). Kwa maoni ya imani, kifo hicho hakionekani kama bahati mbaya, lakini kama kitendo cha Bwana, ambaye mawazo yake hayapatani na mawazo yetu. Kwa mfano, mwandishi huyo anasema kwamba, kulingana na mtazamo wa Mungu,” uzee unaheshimika, sio tu kwa urefu wa maisha wala haupimwi kwa wingi wa miaka. Hekima na maisha mema ni ishara ya kukomaa; hivyo huja pamoja na uzee”( Hk 4,8-9).

Wapendwa wa ishara ya  Mungu, kwa wateule wake, wanatoroka kila kitu kwa wale ambao  wanamtazamo mmoja wa hali halisi ya ulimwengu. Kwa maana hiyo mtazamo wao, kama inavyoonesha kuwa “watu waovu watamwona mwenye busara anakufa lakini hawataelewa matakwa ya Bwana juu yake, wala kwa sababu gani alimweka salama( Hk 4,17), Papa Francisko amefafanua. Katika kusali kwa ajili ya Makardinali na Maaskofu marehemu ambao wametangulia kwa mwaka huu wa mwisho, Papa Francisko ameomba kusali kwa Bwana ili atusaidie kufikiria kwa namna  sahihi mafundisho msingi. Tumwombe ili kusululisha mitazamo hasi inayochanganya na ambayo mara nyongi inajichanganya ndani mwetu kama vile kifo ndiyo mwisho wa kila kitu. Hii ni hisia ya  mbali sana na imani na ambayo inamfikisha mwanadamu kuwa na hofu ya kufa ambayo hakuna mtu anayeweza kusema ana kinga. Kwa sababu hii, akikabiliwa na fumbo la kifo, hata mwamini lazima abadilike kila wakati. Kila siku tunaitwa kupitia zaidi ya picha tuliyo nayo ya asili ya kifo kama maangamizi kamili ya mtu; na lazima kuvuka dhahiri kile kinachoonekana kwa mawazo yaliyowekwa wazi na dhahiri, ili kujiaminisha kabisa kwa Bwana anayetangaza: Mimi ni ufufuko na uzima, aniamini mimi hata akifa, ataishi; kwa maana hiyo anayeishi anaamini mimi na wala hatakufa milele (Yh 11-225-26).

Kwa kutumia maneno ya  yake Mtakatifu Paulo, Papa Francisko amewaalika kwa wote wahisi kuwa na imani(…) Iwe kwa kukaa ndani ya mwili au kwenda uhamishoni, tunajitahidi kumpendeza (2Kor 5,8-9). Maisha ya mtumishi wa Injili yanazungukia shauku ya kuweza kupendezwa yote na Bwana. Mantiki hiyo ndiyo kila uchaguzi na kila hatua ya kutimiza. Kwa kukumbuka kwa shukrani, ushuhuda wa Makardinali na Maaskofu marehemu walioishi kwa imani, kwa mujibu wa Mungu, Papa Francisko ameomba kusali kwa ajili yao na zaidi kutafuta kufuata mifano yao. Bwana anajikita daima juu ya hekima  ya roho zao , kwa namna ya pekee katika kipindi hiki cha majaribu. Na zaidi katika masaa ambayo safari inakuwa ngumu sana. Bwana hatuachi, bali anabaki daima nasi, ni mwaminifu katika ahadi yake. Tazama mimi niko nanyi siku zote hadi miisho ya Dunia ( Mt 28,20).

05 November 2020, 16:33