Tafuta

2020.11.15 Misa ya Papa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika siku ya Maskini duniani 2020.11.15 Misa ya Papa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika siku ya Maskini duniani 

Papa Francisko:Ikiwa hatutaki kuishi maskini tuombe neema ya kuona Yesu kwa Maskini!

Katika Misa takatifu iliyoongozwa na Papa Francisko kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican,tarehe 15 Novemba 2020,katika fursa ya maadhimisho ya Siku IV ya Maskini duniani,Papa amesisitiza kutosahau maskini kwani wako katikati ya Injili.Injili haiwezi kueleweka bila maskini.Maskini wako katika nafsi sawa na Yesu,aliyekuwa tajiri,akajifanya maskini na mdhambi.Ikiwa hatutaki kuishi maskini tuombe neema ya kuona Yesu katika Maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameadhimisha Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patro Vatican, Jumapili tarehe 15 Novemba 2020, ikiwa ni Siku ya IV ya Maskini duniani iliyoanzishwa na Yeye kunako mwaka 2017 akibainisha ifanyike kila Jumapili ya 33 ya  mwaka. Ni katika muktadha wa kuweka umakini wa maskini ambaye amekuwapo katika mchakato wa historia na ambaye Bwana Yesu anajifafanisha na maskini. Kauli mbiu inayoongoza maadhimisho haya ni “Wape maskini kwa ukarimu ( rej Sir 7,32). Washiriki wa Misa walikuwa ni mia moja tu kutokana na muktadha wa janga la virusi vya sasa,na kwa maana hiyo kwa mwaka huu maadhimisho ya siku hii yamekuwa tofauti. Papa Francisko akianza tafakari ya siku kuongozwa na Injili ya Mtakatifu Matayo (Mt 25,14-30) amesema, Somo ambalo limesomwa lina mwanzo, katikati na mwisho na likiangazia mwanzo, katikati na mwisho wa maisha yetu. Mwanzo. Yote yalianza na wema mkubwa. Bwana akuweza kutunza utajiri wake binafsi, bali kuwapatia watumwa. Kuna aliyepewa talanta tano, mwingine akapewa mbili na mmmoja akapewa talanta moja, kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake Mt 25,15). Hata hivyo Papa amesema inahesabiwa kuwa talanta moja ililingana na mshahara wa karibu miaka ishirini ya kazi: ilikuwa faida nzuri sana, ambayo ilikuwa ya kutosha kwa ajili ya maisha yote.

Tazama mwanzo, Papa ameendelea na tafakari kuwa, hata kwetu sisi yote yalianzia na neema ya Mungu ambaye ni Baba na aliweka mikononi mwetu mema mengi, kwa kukabidhi kila mmoja talanta tofauti. Sisi ni wabebaji wa utajiri mkubwa ambao hautokani na sisi wenyewe, yani  kwa yote ambayo tumefanya bali na yanatokana na kile ambacho sisi ni,..  yaani kutokana na kile ambacho tumepokea, wema ambao umo ndani mwetu, kutokana na uzuri usio na kifani ambao Mungu alitupatia, na kwa sababu sisi ni sura na mfano wake, kila mmoja wetu ni mwenye thamani machoni mwake, wa kipekee na asiyelinganishwa  katika historia. Papa Francisko amesema ni kwa jinsi gani ilivyo muhimu kukumbuka hilo. Mara nyingi kwa kutazama maisha yetu, tunaona kile ambacho tunakosa. Na kwa maana hiyo tunajiachia katika kishawishi cha “labda”. Labda kama ningekuwa na kazi ile, labda kama ningekuwa na nyumba ile, labda kama ningekuwa na fedha, mafanikio, labda kama nisingekuwa na matatizo hayo, labda kama ubora ungekuwa unanizunguka!...  yote hayo ni udanganyifu wa “labda” ambao unatuzuia kuona wema na kutufanya kusahau talanta tulizo nazo, amesisitiza Papa. Ka kuongeza amesema “Lakini Mungu alimkabidhi kila mmoja wetu na anajua ni uwezo gani tulio nao; anamwamini kila mmoja wetu licha ya udhaifu wetu”.  Papa kwa kusisitiza “anamwamini hata yule mtumwa aliyekwenda kuficha talanta, akiwa na tarajio kuwa angeweza kushinda hofu yake na ili aweze kutumia wema ambao aliupokea”. Kwa hakika Bwana anatuomba tufanye jitihada za wakati uliopo bila kumbukizi la wakati uliopita, bali  kusubiri matarajio ya kazi yake kwa ajili ya kurudi kwake, Papa amesisitiza.

Katikati ya mfano wake ni  katika kazi ya watumwa, yaani huduma. Huduma ni hatima kazi yetu, kile ambacho kinafanya kuzaa talanta na kutoa maana ya maisha. Haitajiki yule anayeishi kwa ajili ya kuhudumia tu. Je ni mtindo upi wa kuhudumia? Ppa ameuliza na kujibu kwamba “Katika Injili watu wenye akili ni wale wanaothubutu. Wao siyo walinzi na wala kuhifadhi kile walichopokea, badala yake  wanakifanyia kazi. Hii ni kwa sababu wema usipo wekwezwa, unapotea, na kwa sababu thamani yetu ya maisha, haitegemei na kile ambacho tumeweka pembeni, lakini ni matunda mangapi ambayo sisi tunayotoa. Akitoa mfano Papa Francisko amesema “Ni watu wangapi wanaishi maisha kwa ajili ya kukusanya tu, wakifikiri kuishi vizuri, zaidi badala ya kutenda wema. Lakini ni kwa jinsi gani maisha hayo yalivyo matupu yanayofuata mahitaji, bila kutazama aliye na shida! Ikiwa tunazo zawadi ni kwa sababu sisi ni zawadi!” Lazima kusisitiza kuwa watumwa wanaowekweza na wanaothubutu, kwani ni mara nne wanaitwa wema na waaminifu ( Mt, 21.23). Katika Injili hakuna imani bila hatari.Kuwa mwaminifu wa Mungu ni kujitoa maisha na kujiachia katika mipango ya huduma. Ni huzuni ikiwa mkristo anachezea juu ya kujilinda, kushambulia na kuhifadhi sheria na heshima ya amri. Hiyo haitoshi,Papa amesisitiza, kwani uaminifu wa Yesu siyo tu kutofanya makosa.  Na ndivyo alikuwa anafikiria mtumwa mvivu katika mfano wa Injili, hakuwa na mpango wowote na ubunifu na akaenda kuificha nyuma ya hofu na kuzika talanta aliyopewa. Papa Francisko ameuliza swali “Kwanini kuwa Mkristo lazima kuthubutu? Ndiyo mpendwa, lazima kuthubutu. Ikiwa hutathubutu utaishia kuwa kama mtumwa wa tatu anayonekana katika somo, kwa kuzika uwezo wako wote, utajiri wako wa kiroho, na mali na kila kitu, na kwa maana hiyo ni kuthubutu. Kwa maana hakuna uaminifu  bila kuthubutu”, Papa amefafanua.

Na hatimaye Bwana akamwita yule mtumwa mbaya na ulegevu (26). Pamoja na kwamba hakufanya baya! Lakini pia tayari hakufanya mema. Alipendelea dhambi ya kutotimiza wajibu badala ya kuthubutu kukosea. Hakuwa mwaminifu wa Mungu ambaye anapenda kujitoa, na yeye alimfanyia kosa baya zaidi la kurudisha zawadi aliyopewa. Bwana anatualika kujikita katika mchezo wa ukarimu, kushinda hofu kwa ujasiri wa upendo, kushinda ulegevu ambao unageuka kuwa mgumu. Leo hii katika nyakati zisizo na uhakika, za udhaifu tusiharibu maisha kwa kujifikiria sisi wenyewe tu. Tusidanganywe kwa kusema “kuna amani na usalama ( 1Watesa, 5,3). Mtakatifu Paulo anatualika kutazama usoni hali halisi na bila kuacha kuambukizwa na kutojali. Ni kwa njia gani ya kuweza kuhudumia kwa mujibu wa Mungu? Papa Francisko ameuliza swali na  kufafanua kuwa bwana anaelezea yule mtumwa hasiye mwaminifu kwamba “basi ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoa riba, nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake” (27). Papa ameongeza , “lakini msiwasahau. Maskini wako katikati ya Injili. Injili haiwezi kueleweka bila maskini. Maskini wako katika nafsi  sawa na Yesu, aliyekuwa tajiri, akajinyenyekeza mwenyewe, akajifanya maskini na  mdhambi, umaskini mbaya zaidi”. Papa amesisitiza.

Je hao ni wakina nani watoa riba wenye uwezo wa kupata hata faida ya kudumu? Ni maskini. Wao wanatuhakikishia faida kubwa ya milele na ambayo tayari sasa inaturuhusu kujitajirisha kwa upendo. Umaskini mkubwa wa kupambana nao ni umaskini wa upendo. Papa amefafanua. Kitabu cha Mithari mwandishi anasifu mwanamke mwema ni mwenye kujishughulisha katika upendo ambao thamani yake ni kubwa zaidi ya lulu, ni wa kuigwa mwanamke ambaye anatajwa kuwa huwakunjulia maskini mikono yake (Mit 31,20). Uwanyoshea wahitaji mikono yake badala ya kijidai kwa kile anacho kosa. Na kwa maana hii kitaongezeka kile ambacho umepokea. Papa ameongezea kusema “ Tunakaribis kipindi cha Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, kipindi cha sikukuu. Ni maswali mangapi yanaulizwa na watu wengi: “ Ni kitu gani ninaweza kununua? Ni kitu gani ninaweza kuwa nacho cha zaidi? Lazima niende madukani (…) Tuseme neo jingne: “ ninaeza kunua nini kwa ajili ya wengine ili niweze kuwa kama Yesu aliyetoa maisha yake mwenyewe na akazaliwa katika pango la kweli?”. Papa Francisko akifafanua hatua ya mwisho ya mfano  Injili anasema kwa maana kila mwenye kitu atapewa na kuongezewa tele, lakini atakayeharibu atabaki maskini. Mwisho wa maisha, kwa kifupi, ukweli utafunuliwa: hadithi ya ulimwengu itafifia, kulingana na mafanikio, nguvu na pesa ambayo inafikiriwa kama maana ya kuishi, wakati upendo, yaani kile tulichopewa, kitatokea kama utajiri wa kweli. Lazima kurudia mara nyini kuwa haitajiki kuishi na yule hasiyeishi kwa ajili ya kuhudumia. Ni lazima kutafakari juu ya hilo, amesisitiza Papa!

Baba wa Kanisa aliandika kuwa “hivi ndivyo maisha yanakuwa, baada ya kufikia kifo, tamasha linakwisha wote tunatoa barakoa za utajiri na umaskini  na wanaondoka katika dunia hii. Na wanahukumiwa kwa msingi wa matendo yao, baadhi kiukweli ni matajiri na wengine maskini (Mtakatifu Chrisostom, Hotuba juu ya maskini Lazaro II, 3). Ikiwa hatutaki kuishi maskini, tuombe neema ya kuona Yesu kwa maskini na kuhudumia Yesu katika maskini. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amewashukuru waamini wote wa Mungu ambao hawazungumzii juu yao, lakini wanaishi hivyo. Amefikiria Padre Roberto Malgesini. Na kwamba alikuwa hafanyi nadharia, bali kiurahisi alikuwa anaona Yesu katika Maskini, na maana ya maisha katika kuhudumia. Alikuwa akiwafuta machozi kwa upole na kwa neno la Mungu anayefariji. Mwanzo wa siku yake alikuwa anaanza na maombi na kupokea zawadi ya Mungu. Katikati ya siku ilikuwa ni upendp kwa jili ya kutoa matunda ya upendo aliyopokea na mwisho ulikuwa ni ushuhuda halisi wa Injili. Alikuwa ametambua kwamba lazima utoe ukarimu wake  kwa ajili ya maskini wengi ambao kila siku alikuwa anakutana nao kwa sababu katika wao alikuwa anamwona Yesu. Tuombe neema ya kuondokana na ukristowa nadahria na  kuwa wa matendo. Na ili kuweza kutoa matunda kama Yesu alivyokuwa anatamani.

15 November 2020, 14:13