Tafuta

2020.11.23 Kitabu kitwacho"Ritorniamo a sognare" (Piemme) "Turudi kuota" kilichoandikwa na Papa pamoja na mwandishi  Austen Ivereigh. 2020.11.23 Kitabu kitwacho"Ritorniamo a sognare" (Piemme) "Turudi kuota" kilichoandikwa na Papa pamoja na mwandishi Austen Ivereigh. 

Papa Francisko:Hali za covid na upweke wa aina tatu za maisha

Tutangaze kifungu kutoka kitabu kiitwacho“Ritorniamo a sognare” yaani “turudie kuota”(Piemme) kilichoandikwa na Papa akiwa na mwandishi wa habari Austen Ivereigh,kitapatikana katika maduka ya vitabu mwezi Desemba.Kifungu kilichotwaja kimetangulizwa na Gazeti la kila Siku la ‘Repubblica katika toleo kwenye vituo vya kuuza magazeti ya kila siku.

PAPA FRANCESCO

Katika maisha yangu nimekuwa na hali tatu za “Covid”: ugonjwa, Ujerumani na Córdoba.

Wakati nikiwa na miaka ishirini na moja, nilipata ugonjwa mbaya sana, nilipata uzoefu wangu wa kwanza wa vikwazo, maumivu na upweke. Ulinibadilisha kuratibu kwangu. Kwa miezi kadhaa sikujua mimi ni nani, ikiwa nitakufa au kuishi. Hata madaktari hawakujua ikiwa ningeweza kuishi. Nakumbuka siku moja nilimwuliza mama yangu, huku nikimkumbatia, aniambie ikiwa nitakufa. Nilikuwa katika mwaka wa pili wa seminari ya jimbo huko Buenos Aires.

Nakumbuka tarehe: ilikuwa 13 Agosti 1957. Mkuu wa Seminari alinipeleka hospitalini, kwa maana aligundua kuwa sikuwa na aina ya homa inayotibiwa na aspirini. Kwanza walitoa lita moja na nusu ya maji kutoka kwenye mapafu yangu, baadaye nikabaki nikipambana kati ya maisha na kifo. Mnamo Novemba, walinifanyia upasuaji ili kuondoa tundu la juu la kulia wa mapafu yangu. Ninajua kabisa kutokana na uzoefu jinsi wagonjwa  wanavyohisi wenye virusi vya corona wakati wanajitahidi kupumua kwenye mashine ya kupumulia hewa. Nakumbuka wauguzi wawili hasa kutoka siku hizo. Mmoja alikuwa muuguzi mkuu, mtawa wa Kidominika ambaye alikuwa mwalimu huko Athene kabla ya kupelekwa Buenos Aires.

Baadaye nilijifunza tu baada ya daktari kuondoka baaada ya uchunguzi wa kwanza kumalizika, aliwaambia manesi kuongeza maradufu kipimo cha matibabu aliyokuwa ameagiza  yaani penicillin na streptomycin kwa sababu uzoefu wake akamwambia anakufa. Sr.  Cornelia Caraglio aliokoa maisha yangu. Shukrani kwa mawasiliano yake ya kawaida na wagonjwa, alijua vizuri kuliko daktari kile ambacho wagonjwa wanahitaji, na alikuwa na ujasiri wa kutumia uzoefu huo. Kutokana na uzoefu huo nilijifunza jambo lingine: ni muhimu kuepuka faraja ya bei rahisi. Watu walikuja kuniona na kuniambia kuwa nitakuwa sawa, kwamba sitakuwa na uchungu wa kusikia maumivu yote tena lakini hayo yalikuwa ni maneno ya kipuuzi, maneno matupu yaliyosemwa kwa nia nzuri, lakini kamwe hayakufikia moyo wangu.

Mtu ambaye alinigusa sana, na ukimya wake, alikuwa mmoja wa wanawake waliotia alama maisha yangu. Ni  Sr. María Dolores Tortolo, mwalimu wangu nikiwa mtoto, ambaye alikuwa ameniandaa kupokea Komunio ya Kwanza. Alikuja kuniona, akanishika mkono, akaubusu na kukaa kimya kwa muda mrefu. Baadaye akaniambia: “Unaiga Yesu”. Hakukuwa na haja ya yeye kuongeza kitu kingine chochote. Uwepo wake, ukimya wake, ulinipa faraja kubwa. Baada ya uzoefu huo, nilifanya uamuzi wa kuzungumza kidogo mapama iwezekanavyo wakati nitakapotembelea wagonjwa. Mimi ninachukua mkono wao  tu kwa muda kitambo.

Ningeweza kusema kwamba kipindi cha kijerumani, mnamo 1986, kilikuwa ni “Covid” ya uhamisho”. Ilikuwa uhamisho wa hiari, kwa sababu nilikwenda huko kusoma lugha hiyo na kutafuta nyenzo za  kukamilisha utetezi ya masomo yangu (Thesis), lakini nilijihisi kama vile samaki nje ya maji. Nilikuwa nikikimbia ili  kutembelea hadi kufikia makaburi kadhaa huko Frankfurt na kutokea hapo ulikuwa unaweza kuona ndege zikipanda na kutua; Nilikuwa nikitamani kurudi nyumbani katika nchi yangu. Na ninakumbuka siku ambayo Argentina ilitwaa Kombe la Dunia.

Sikutaka kuona mchezo na nilijua tumeshinda tu siku iliyofuata, kwa kusoma kwenye gazeti. Hakuna mtu katika darasa langu la Kijerumani aliyetaja, lakini wakati msichana wa Kijapani alipoandika “Argentina hoyee” ubaoni, wengine walicheka. Mwalimu alopoingia akasema kufuta hilo neno na kufunga gumzo hiyo. Ilikuwa upweke wa ushindi peke yangu, kwa sababu hakukuwa na mtu wa kushirikishana naye; upweke wa kutokuwa mahali, ambapo unakufanya uwe mgeni. Wanakutoa mahali ulipo na kukuweka mahali ambapo hujui na kwa kuwa wakati huo huo unajifunza ni kitu gani ni muhimu katika mahali ulipoacha.

Hata hivyo wakati mwingine kuondoka katika mizizi inaweza kuwa uponyaji au mabadiliko kabisa. Ndivyo ilivyokuwa pia Covid ya tatu kwangu wakati waliponipeleka Córdoba tangu mwaka 1990 hadi 1992. Mzizi wa kipindi hiki ulirudi kwa njia yangu katika  kuongoza, kwanza twengi wetu tulipewa, na ilinifanya vizuri. Iliniongoza kukuza maoni: niliandika na kusali sana.

Karibu na kipindi hicho, leo, hii haya mambo matatu yamenigonga hasa. Kwanza, uwezo wa kusali ambao nilizawadiwa. Pili, majaribu niliyohisi. Na tatu na ni jambo la kushangaza zaidi kwamba wakati huo niliweza kusoma vitabu thelathini na saba vya Historia ya Mapapa iliyoandikwa na mchungaji Ludwig. Ningeweza kuchagua riwaya, kitu cha kufurahisha zaidi. Kutokana na mahali sasa nilipo najiuliza ni kwanini Mungu alinihimiza kusoma kazi hiyo kwa wakati huo. Pamoja na chanjo hiyo Bwana aliniandaa. Mara tu unapojua hadithi hiyo, hakuna mengi ambayo yanaweza kukushangaza juu ya kile kinachotokea katika Kanisa la Roma na katika Kanisa la ulimwengu leo. Ilinisaidia sana!

“Covid” ya Córdoba ilikuwa utakaso halisi. Ilinipa uvumilivu zaidi, uelewa na uwezo wa kusamehe. Pia iliniacha na uelewa mpya wa wanyonge na wasio na mlinzi. Uvumilivu, kuwa na uvumilivu mwingi, hiyo ni zawadi ya kuelewa kuwa vitu muhimu huchukua muda, mabadiliko hayo ni ya kiundani, kwamba kuna mipaka na lazima tufanye kazi ndani mwake na wakati huo huo tuangalie upeo wa macho, kama alivyofanya Yesu ... Nilijifunza umuhimu wa kuona ukuu katika udugu  na kuwa makini kwa vitu vidogo na katika mambo makuu. Ilikuwa kipindi cha ukuaji kwa njia nyingi, kama vile kuchipua tena mara baada ya kupunguzwa  matawi.

Lakini lazima niwe macho, kwa sababu unapoanguka katika kasoro fulani, dhambi fulani, na ujisahihishe, shetani, kama Yesu anavyosema, anarudi, na kuona nyumba imefagiliwa na kupambwa (Luka 11:25) na huenda akawaita wengine saba, roho mbaya kuliko yeye. Mwisho wa mtu huyo, Yesu anasema, ulikuwa mbaya sana kuliko hapo awali. Lazima niwe na wasiwasi juu ya hili sasa ya majukumu ya ofisi yangu katika  kuliongoza Kanisa: Ili nisije  kuanguka katika kasoro sawa na wakati nilipokuwa mkuu wa shirika. […] Hizi zilikuwa Covid zangu kuu kibinafsi. Nilijifunza kuwa unateseka sana, lakini ukiniruhusu zikubadilishe, na unainua vizuizi, unatoka vibaya zaidi.

23 November 2020, 16:30