Tafuta

2020.11.04 Katekesi ya Papa:Akibariki kupitia Maktaba ya Jumba la Kitume Vatican 2020.11.04 Katekesi ya Papa:Akibariki kupitia Maktaba ya Jumba la Kitume Vatican  

Papa Francisko:Bila maisha ya undani tunajitoroka sisi wenyewe!

Papa Francisko amerudi kufanya katekesi yake katika maktaba ya Jumba la Kitume ambapo tafakari yake ni mwendelezo wa sala.Kuna haja ya kukuza maisha ya undani maana bila ni kugeuka kuwa watu wa kukimbia huku na kule.Sala ni sanaa ya kufanya uzoefu bila kikomo.Sisi sote tunao uwezo wa sala ya matukio yanayozaliwa na hisia za wakati tu;Yesu anaelimisha aina nyingine ya sala,ile ambayo imejifichika katika nidhamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kabla ya kuanza katekesi yake, Papa Francisko tarehe 4 Novemba 2020 amebainisha juu ya kurudi tena kufanya katekesi katika Maktaba ya Kitume, “kwa sababu ya kuzuia maambukizi ya covid na hivyo amesema kwamba inatufundisha kuwa tunapaswa kuwa makini katika maelekezo ya wamlaka; iwe mamlaka ya kisiasa na hata ya kiafya kwa ajili  ya kujilinda na janga hili. Tumtolee Bwana umbali huo kati yetu, kwa ajili ya wema wa wote na kufikiria, zaidi wagonjwa, wale ambao tayari wanaingia wakiwa wamekweisha baguliwa, tufikirie madaktari, wauguzi, watu wa kujitolea na watu wengine wengi ambao wanafanya kazi na wagonjwa hao katika wakati huu na ambao wanaahatarisha maisha yao lakini wanafanya kwa upendo na wito wao.

Akianza tafakari yake Papa Francisko katika mwendelezo wa mada ya sala amesema kuwa “Wakati wa kuanza maisha ya utume wake kwa watu, Yesu aliongozwa na sala  kwa nguvu zote. Injili zinaonesha akiwa anakwenda  mafungo katika maeneo ya umbali ili kusali. Hii ni matazamo nyeti , wa faragha, ambao unakuacha uwaze maeneo hayo ya kusali. Maeneo hayo yanashuhudia lakini uwazi kuwa hata katika wakati mgumu wa kujitoa kwa maskini na wagonjwa, Yesu hakuacha kamwe kuzungumza  kwa undani na Baba yake. Na wakati  anakumbana  ndani ya matatizo ya watu, ndivyo alivyokuwa akihisi ulazima wa kupumzika katika muungano wa utatu”. Papa Francisko anasisitiza ni katika maisha ya Yesu kwa namna hiyo kuna siri, ambayo imejificha machoni mwa binadamu, na ambayo inawakilisha kitovu cha yote. Sala ya Yesu ni hali halisi ya fumbo, ambalo tunaweza tu kujua kitu, lakini kinachorohusu kusoma katika matarajio sahihi ya utume wake wote. Katika masaa yale akiwa pekee yake, kabla ya kupambazuka jua au katika usiku, Yesu anajikita kwa kina na Baba, hii ina maana ya kusema katika Upendo ambao kila roho inakiu. Ni jinsi anavyojikita kusali kwa undani tangu siku za kwanza ya utume wake kwa watu.

Jumamosi kwa mfano, katika mji wa Kafaranaum, ukageuzwa kuwa “Hospitali ya kambi”, baada ya jua kuzama wanampelekea Yesu wagonjwa wote, na Yeye anawaponya. Lakini kabla ya mapambazuko, Yesu anapotea. Na kwenda kwenye mafungo katika eneo la mbali na kusali. Simoni na wengine walimtafuta na walipomwona wakamwambia “watu wote wanakutafuta!” Akawajibu “ Ninapaswa kwenda kuhubiri katika vijiji vingine, kwa maana hiyo mimi nimekuja” ( Mk 1,25-38). Yesu daima ni zaidi , katika sala na Baba na zaidi , katika vijiji vingine na peo nyingine katika kuhubiri, na kwa watu. Maombi ni usukani ambao unaongoza mwendo wa Yesu. Si mafanikio ambayo yanaamuru hatua za utume wake, sio yale maneno ya kulaghai, kama vile “wote wanakutafuta”. Kinachobainisha mchakato wa safari ya Yesu ni njia ambayo siyo nzuri, lakini ambayo anatii kwa kufuata mwongozo wa  Baba ambaye Yesu anasikiliza, anapokea katika sala yake binafsi.

Papa Francisko kwa kufafanua zaidi amesema katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki, inathibitisha kuwa “Wakati Yesu anasali, tayari anatufundisha kusali (N2607).  Kwa maana hiyo kwa mfano wa Yesu tunaweza kupata baadhi ya tabia ya sala ya kikristo. Kwanza inapata ukuu kwani ni shauku ya kwanza ya siku, jambo ambalo linafanywa uzoefu wa machweo, kabla ya dunia haijaamka. Sala inarudisha roho ya kile ambacho labda kingebaki bila pumzi, kuishi siku moja bila sala ni hatari ya kugeuka na kuwa na uzoefu wa usumbufu, au uvivu, yaani kila kitu ambacho kingetokea chaweza kuwa kwetu sisi kibaya cha kuvumilia na hatima ya upofu. Yesu kinyume chake anaonesha katika hali halisi, na kwa maana hiyo katika uskivu. Sala kwanza ni usikivu na kukutana na Mungu. Matatizo ya kila siku kwa maana hiyo hayawi kizingiti, bali yanakuwa miito ya Mungu mwenyewe ili kusikiliza na kukutana na ambaye yuko mbele yako. Majaribu ya maisha yanaoongezaka kwa jinsi hiyo yanakuwa  ni  fursa ya kukua katika imani na katika upendo na hisani. Safari ya kila siku pamoja na ugumu wake, vinapata matarajio ya wito. Sala ina nguvu ya kugeuza mambo, kwa yale ambayo katika maisha yangekuwa hukumu; ina uwezo wa kufungua upeo mkubwa katika akili na kupanua moyo.

Pili, sala ni sanaa ya kufanyia uzoefu  bila kikomo. Sisi sote tunao uwezo wa sala ya matukio, yanayozaliwa na hisia za wakati tu; lakini Yesu anaelimisha aina nyingine ya sala, yaani ile ambayo imejifichika katika nidhamu, katika mazoezi na ambayo inachukua nafasi ndani ya kanuni ya maisha. Sala ya kila wakati na ambayo inazaa maendeleo ya mabadiliko, na kukufanya kuwa na guvu katika vipindi vya magumu, inatoa neema ya kujua unalindwa na kuongozwa na Yule ambaye anatupenda na kutulinda daima. Tabia nyingine ya sala ya Yesu ni ile ya upweke. Anayesali hatawanyiki katika ulimwengu, bali anaelekekea katika eneo la jangwa. Pale yenye ukimya wa dhati, inawezekana kutokea sauti nyingi sana ambazo zinajificha ndani ya moyo kama vile shauku zaidi ya majuto, ukweli ambao unazidi kutusonga. Na zaidi katika kimya ya Mungu anazungumza. Kila mtu anahitaji nafasi yake binafsi, mahali pa kukuza maisha yake ya ndani, mahali ambapo matendo yanapata maana. Bila maisha ya undani, tunageuka kuwa wenye wasiwasi, hofu: tunatoroka kiukweli hali halisi kama wanawake na wanawaume na kwa hili lazima twende kwenye maombi!

Sala inatusaidia kujitafuta usahihi wa ukuu katika uhusiano na Mungu, Baba yetu, na viumbe vyote. Ni sala ya Yesu ambayo ni kujikabidhi mikononi mwa Bwana kama Yesu alivyofanya katika bustani ya Mizeituni, kwa uchungu ule ule. “Baba ikiwa inawezekana… lakini mapenzi yako yatimie”. Kujikabidhi katika mikono ya Baba. Ni vizuri Papa amesema ikiwa sisi tunaoangaika na kuwa na wasisi wasi, Roho Mtakatifu anatubadili kutoka ndani na kutupelekea katika kujikabidhi katika mikono ya Baba, na kusema “ Baba mapenzi yako yatimie”…. Amesisitiza Papa Francisko Hatimaye sala ya Yesu ni mahali ambapo tunatambua kuwa kila kitu kinatoka kwa Mungu na kinarudi kwake. Wakati mwingine sisi wanadamu tunaamini sisi ni mabwana wa kila kitu, au kinyume chake tunapoteza kujithamini, tunakwenda kutoka upande mmoja hadi mwingine. Maombi hutusaidia kupata mwelekeo sahihi katika uhusiano na Mungu, Baba yetu, na viumbe vyote. Papa Francisko amesema tugundue tena, katika Injili, Yesu Kristo kama mwalimu wa sala, na twende shuleni kwake. Ninawahakikishia kuwa tutapata furaha na amani, amehitimisha.

04 November 2020, 15:02