Tafuta

PAPA NA BIDEN PAPA NA BIDEN 

Papa Francisko azungumza kwa simu na rais mteule Joe Biden

Tarehe 12 Novemba 2020,Papa Francisko na Rais mteule Joe Biden wa Marekani wamepata kuzungumza kwa njia ya simu.Ni kwa mujibu wa Msemamaji wa Vyombo vya habari Vatican Dk.Matteo Bruni.

VATICAN NEWS

Ni mazungumzo yaliyofuata mara baada maaskofu wa Marekani kwa njia ya ujumbe wa Rais wa Baraza la Maaskofu hao, Askofu Mkuu José H. Gomez, wa jimbo Kuu katoliki la Los Angeles akimpongeza kama kama rais wa pili mkatoliki wa Nchi hiyo baada ya John F. Kennedy, alisema : “Tukimshukuru Mungu kwa ajili ya baraka ya uhuru, watu wa Marekani wamejifafanua katika uchaguzi huu”.

Leo hii ni wakati ambao viongozi wanaweza kuungana katika roho ya umoja wa kitaifa na kukimbilia mazungumzo na jitihada kwa ajili ya wema wa pamoja. Kama wakatoliki wa Marekani, vipaumbele vyetu na utume wetu uko wazi. Maaskofu aidha walionesha  wazi kwamba “ tupo hapa kwa ajili ya kufuata Kristo, kushuhudia upendo wake katika maisha yetu ili kujenga ufalme wake hapa duniani. Nina imani katika wakati huu wa historia ya Marekani, wakatoliki wanaouwajibu maalum wa kuwa wahudumu wa amani, kuhamasisha udugu na kuaminiana, kusali kwa ajili ya upyaisho wa roho ya kweli ya uzalendao wa taifa letu”.

Ujumbewao kwa rais mteule kutoka kwa Maaskofu wa Marekani ulikuwa unahitimishwa kwamba: “ Tunamwomba Bikira Maria, msimamzi wa taifa hili kubwa atuoembee. Atusaidie kufanya kazi kwa  ajili ya umoja ili kutimiza maono mazuri ya kimisionari na ya waanzilishi wa Marekani, katika taifa ambalo liko chini ya ulinzi wa Mungu na mahali ambamo utakatifu wa kila maisha unalindwa na kuhakikisha uhuru wa dhamiri na dini.

13 November 2020, 12:57