Tafuta

2020.11.24 Mwenyeheri Padre  Mario Ciceri  2020.11.24 Mwenyeheri Padre Mario Ciceri  

Papa Francisko aridhia kuwatangaza wenyeheri wapya!

Papa ameridhia Baraza la kipapa la mchakato wa kuwatangaza wenyeheri na watakatifu utambuzi wa kuwatangaza wenyeheri wapya wa Kanisa.Hawa ni watumishi wa Mungu ambao ni wafiadini 127,walei,watawa na makuhani wa Uhispania na wenye fadhila za kishujaa kutoka Italia na Ufaransa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 23 Novemba 2020, Papa Francisko alikutana na Kardinali Mteule Marcello Semeraro, rais wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza wenyeheri na watakatifu ambapo wakati wa mazungumzo yao, Papa ameridhia baraza hilo kuwatangaza wafuatao: Miujiza  iliyotolewa kwa maombezi ya mtumishi wa Mungu Mario Ciceri, kuhani wa jimbo; alizaliwa tarehe 8 Septemba 1900 huko Veduggio (Italia) na kifo chake huko Brentana wa Sulbiate (Italia) tarehe  4 Aprili 1945;

Mfiadini, mtumishi wa Mungu Giovanni Elia Medina, kuhani wa jimbo  na wenzake 126  makuhani , watawa na walei waliouwawa kwa sababu ya chuki ya imani yao nchini Uhispania kati ya mwaka 1936 na 1939; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Fortunato Maria Farina, Askofu Mkuu wa Adrianopoli ya Onoriade, ambaye alikuwa tayari askofu wa Troia na  Foggia; Alizaliwa tarehe 8 Machi 1881 huko Baronissi (Italia) na kifo chake huko Foggia (Italia) tarehe 20 Februari  1954;

Fadhila za kijashujaa za Mtumishi wa Mungu Andrea Manjón y Manjón, Kuhani na Mwanzilishi wa Shule ya Ave Maria; Alizaliwa  tarehe 30 Novemba 1846 huko Sargentes ya Lora (Uhispania) na kifo chake huko Granada (Uispania) tarehe 10 Julai 1923; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Alfonso Ugolini, Kuhani wa jimbo; Alizaliwa tarehe 22 Agosti 1908 huko Thionville (Ufaransa ) na kifo chake huko Sassuolo (Italia). tarehe 25 Oktoba 1999; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Francesca Ticchi, Mtawa wa ndani wa Waklara wakapuchini; Alizaliwa   tarehe 23 Aprili 1887 huko Belforte ya Isauro (Italia) na kifo chake huko Mercatello ya juu  Metauro (Italia) tarehe  tarehe 20 Juni 1922;

Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Carola Cecchin mtawa wa nadhiri wa Shirika la watawa wa Mtakatifu Giuseppe Benedetto Cottolengo; Alizaliwa tarehe 3 Aprili 1877 huko Cittadella (Italia) na kifo chake akiwa njiani kurdi Italia akitokea  Kenya, tarehe 13 Novemba 1925; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Francesca Giannetto Mtawa wa nadhiri wa Shirika la Mabinti wa Maria Mkingiwa dhambi ya Asili; alizaliwa 30 Aprili 1902 huko Camaro ya juu  (Italia) na kifo chake tarehe 16 Februari 1930.

24 November 2020, 15:20