Tafuta

Papa akutana na Padre Maccalli,mmisionari aliyebaki kwa miaka 2 mikononi mwa wateka nyara huko Mali. Papa akutana na Padre Maccalli,mmisionari aliyebaki kwa miaka 2 mikononi mwa wateka nyara huko Mali. 

Papa Francisko akutana na Padre Maccalli.Shukrani kubwa kuzungumza naye

Hisia za nguvu zilionekana kwa Padre Pierluigi Maccalli mara baada ya mkutano,Jumatatu tarehe 9 Novemba 2020 na Papa Francisko,mjini Vatican ambapo kwa pamoja wamesali kuombea Kanisa lote.

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baada ya mkumbatio wa Papa hakuna maelezo zaidi ya kusema asante. Ndivyo Padre Pierluigi Maccalli, mmisionari wa Shirika la Kimisionari la Afrika kutoka Cremona, Italia alivyo sema akihojiana na Vatican News. Yeye alikombolewa mikononi mwa wateka nyara mnamo tarehe 8 Oktoba 2020, baada ya miaka miwili katika kifungo kati ya Niger na Mali. Padre Maccalli na Papa wamekutana na kuzungumza mara baada ya mwezi mmoja tangu akombolewe,  tukio lililotokea nchini Mali. Ni shukrani kubwa na bila hata kuamini mbele ya mfuasi wa Kristo ambaye ameinama na kubusu mikono ya kuhani kwa mujibu wa Padre huyo.

Katika mazungumzo yao, na Papa Francisko amemesimulia jinsi alivyoishi na kumkabidhi Afrika hasa katika  eneo lake la kitume ambalo  kwas asa limebaki bila kiongozi mmisionari. Katika mahojiano hayo amesema kulikuwa na kutoamini na pia kuwa matatizo ya kujieleza hasa zawadi ya upendo aliyopokea kutoka kwa Papa, kama mmisionari wa pembezoni ambaye kwake Kanisa lote analibeba ndani ya moyo wake hasa ushauri aliopokea kutoka kwa Papa.

Padre Maccalli akisisitiza juu ya  mkutano huo aidha amesema ulikuwa mzuri  sana uliojaa hisia nyingi hasa akimsimuliza Papa kile ambacho aliishi huku akiendelea kuamini sala zake  na zaidi sala ya jumuiya zake alizokuwa akitoa huduma yake kabla ya kutekwa nyara na ambao kwa sasa wamebaki bila mmisionari au padre yoyote kwa miaka miwili.

Kwa furaha kubwa aliyokuwa nayo Padre Maccalli amesema: “Nimemweleza Papa katika sala zake aombee Kanisa la Niger. Papa alikuwa makini sana kunikiliza. Nimemweleza asante kubwa kwa sababu ya kusali kwa ajili yangu pamoja na Kanisa na baadaye hata wakati wa  sala ya Malaika wa Bwana katika  Siku ya Kimisionari Ulimwenguni,iliyopita  ambapo aliomba nipongezwe kwa makofi ya umati mzima uliokuwa kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro kufuatia na kukombolewa kwangu”. “Wakati ninamshukuru, yeye amesema “ tulikusidikiza wewe  lakini ni wewe ulisindikiza Kanisa”. Sikuwa na maneno mbele ya hayo  kama mmisionari mdogo na Yeye anasema hivyo kiukweli sina maneno” amesisitiza.

Kupokea upendo wa Papa Francisko namna hiyo wa  mkubatio wa baba na  ambaye kila siku ninamwombea.. imekuwa jambo muhimu kujikuta ninaye mbele yake! Ilikuwa ni hisia ya nguvu na shukrani kubwa. Sikuwahi kufikiria kwamba mmisionari kutoka  pembe ya ulimwengu, siku moja angejikuta mbele ya Papa mwenywewe, ambaye anahudumia Kanisa la Ulimwengu. Siyo rahisi kuelezea hisia hizo badala ya kutoa shukrani na kusema asante”, amesema Padre Maccalli. Na hatimaye akigusia  juu ya maneno na ishara ambaye atabaki mayo moyoni, anasema ni “kuhusu nilivyompatia mkono wake na yeye akaubusu, ni jambo ambalo sikutegemea…”.

09 November 2020, 17:10