Tafuta

2020.10.27 wakimbizi huko  Lesvos 2020.10.27 wakimbizi huko Lesvos 

Papa Francisko ahimizia shirika la Kijesuit kuwa sauti ya wadhaifu!

Papa Francisko ameandika barua kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Huduma ya Kijesuit kwa ajili ya Wakimbizi (JRS).Katika barua hiyo anawahimiza waendelee kutoa mkono wao wa ukaribu na urafiki kwa wale ambao wana upweke na wamebaguliwa na familia zao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameandikiwa barua katika Kituo cha Astalli cha Huduma ya Wajesuit (JRS), kwa ajili ya wakimbizi katika fursa ya kumbu kumbu ya miaka 40 tangu kuwanza kwake. Katika Barua kwa  Padre  Thomas H. Smolich SI, Mkurugenzi wa Kimataifa katika Huduma hiyo  anasema: “Leo watu wengi sana ulimwenguni wanalazimika kushikamana na boti na mipira katika jaribio la kutafuta hifadhi kutokana na virusi vya ukosefu wa haki, vurugu na vita”. Papa Francisko katika barua hiyo anasema “Mawazo yangu yanawaendea hasa watu wengi wanaume  na wanawake ambao wanakwenda katika kituo cha kijesuit kutafuta kimbilio na msaada, watambue kuwa Papa yuko karibu nao na familia zao na anawakumbuka katika sala zake”. Wakati wakipyaisha kwa kina juhudi zao katika huduma  kwa ajili ya  wahitaji wengi na magumu ya wakimbizi na waliorundikana, Papa amesema kwamba anasali kwa ajili yao pia ili waweze kutiwa moyo na hekima ya na kuiga mfano wa mwanzilishi wao wa shirika la kijeusuit.

Akikumbuka aliyeanzisha shughuli hii amesema “Mbele ya mateso ya wale wanaokimbia nchi zao kutafuta wokovu kwa sababu ya vita nchini Vietnam, Padre Arrupe alibadilisha mateso mengi katika umakini wa mazoezi kwa ajili ya wema wa kimwili, kisaikolojia na kiroho.  Hilo ndilo pia lilikuwa  shauku ya kina ya Kikristo na ya Ignatius aliyependa kutunza wema wa wale ambao walikuwa katika hali ya mahangiko na kuigwa na kuongoza kazi ya Kijesuiti kwa miaka hii 40° tangu kuanza kwa boti  ya watu  wa vietnaum miaka ya 80 hadi nyakati za sasa”. Papa amesema “ Nyakati hizi zimekumbwa na janga la virusi vya corona ambavyo vimeonekana katika familia nzima ya kibinadamu katika mtumbwi mmoja, kwa kukabiliana na changamoto za kiuchumi, na kijamii.  Ni wakati wa sala muhimu kwa ajili yao  akikumbusha sala yake ya mwezi Machi mjini Vatican (, 27 mach2020).

Hata hivyo akitoa maoni kuhusu barua hiyo Padre Camillo Ripamonti, Rais wa Kituo cha Astalli Roma, amesema Baba Mtakatifu anatuhimiza tena katika uwajibikaji wetu na ubinadamu wetu. Janga lisituondolee suala hili. Mwathirika wa hivi karibuni wa kutokujali kwetu ni mtoto wa miezi sita. “tupinge mantiki ya Kaini na tuendelea yale majukumu yanayohusu  taasisi ya kuwa sawa na kazi waliyokabidhiwa ili kuhakikisha kuheshimu hadi  na haki za kila mwanadamu. Kuruhusu wafe bila kufanua lilote kwa wale ambao wanajaribu kufikia mahali pa salama ulimwenguni ni matunda machungu ya mantiki ya kutokujali na utamaduni wa kubagua ambao Papa Francisko anatuonya dhidi yake. Na anaomba wanaume na wanawake wa dini zote watende na wasimamishe mauaji. Kuadhimisha maka 40 ni kupiaisha kwa hakika jitihadaza za kila siku karibu na wahamiaji kwa utuambuzi wa kuwa karibu na wenye haki.

12 November 2020, 15:46